Mrejesho kuhusu huduma ya kituo cha wateja

Mrejesho kuhusu huduma ya kituo cha wateja

TRA Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
132
Reaction score
376
Mpendwa Mlipakodi,

Asante kwa mrejesho wako kuhusu huduma ya kituo cha wateja.

Tunasikitika kwa usumbufu uliopata, hasa katika matumizi ya mfumo na module ya remission. Tumeanza kuchukua hatua za kuboresha huduma kwa kuwajengea watumishi uwezo stahiki wa mifumo ili kukuhudumia kwa haraka na ufanisi zaidi.

Pia tutaendelea kutunza usiri wa taarifa za walipakodi wote nchini hivyo ukiitwa ofisini usisite kufika kwa huduma zinazohitaji kufanya hivyo.

Kwa msaada wa haraka kuhusu ombi lako la remission, tafadhali wasiliana na meneja wa ofisi unayohudumiwa na mawasiliano yanapatikana kwenye tovuti ya www.tra.go.tz

Tunathamini mrejesho wako.

Asante kwa kushirikiana nasi.

Pia Soma: KERO - Responded - TRA waboreshe Kitengo cha “Customer Care”, siyo kila kitu hadi kwenda ofisini kwao
 
Sawa mkuu, kwanini usiweke hayo malalamiko hapa ili nasisi wasomaji tulinganishe na majibu uliyo yatoa??
 
Back
Top Bottom