Mrejesho: Kanikataa, je nimchomee kuwa ana vyeti feki?

Dec 5, 2015
6
4
Wadau,

Jana niliwaeleza kuhusu jipu moja linalohitaji kutumbuliwa
Jipu hilo ni msichana wangu ambae amepiga u turn ghafla na kuamua kuolewa na mwingine, akisahau kuwa mimi najua siri yake ya kughushi vyeti.

Baada ya ushauri wenu nimefikia hitimisho la kumchomea kazini kwake kuwa anatumia vyeti feki kwa sababu zifuatazo;

(1) Mimi sio muumini wa ile slogan ya kwamba " Mungu atanilipia tu"" mimi ni muumini wa ile slogan ya titi for tati, huwezi kumtendea mtu ubaya ukategemea yy akutendee mema.

(2) Nimejiridhisha kuwa sina hatia yoyote katika dhambi hiyo kwa kuwa nilitoa fedha tu ambapo mtu anaweza kuomba fedha anachokwenda kufanyia ni juu yake, yy alipomaliza kazi hiyo alinionesha vyeti hivyo na kunieleza alipotengeneza Basi,

(3) nimeamua kuindikia barua kampuni hiyo from unknown address and source, kuwa whistle blower hakuhitaji ujitokeze, unaweza tu ukaandika hata barua isiyo na jina au email, wawe wenyewe watashughulikia kwa undani
Kampuni kufuatilia cheti feki ni raisi tu, wanapiga tu simu kwenye taasisi husika na kusoma namba ya cheti na majina, kazi inaishia hapo

(4) Kuna waliosema sitafaidika na kitu nikimchoma hasa wanawake, nitafaidika
Roho yangu itakua na furaha na revenge ni sehemu ya Tiba,
Mtu amenifanya na sasa anachekelea then mnasema sitafaidika na kitu?
Nikiacha kusema nafaidika na nn kwa mfano?

Atafukuzwa kazi na kuajiriwa mtu anaestahili, mbona yeye wakati ananifanyia ubaya hakuniweka kwenye consideration? Iweje mimi nimuweke kwenye consideration?

Hatanirudia nisiposema na hatanirudia nikisema, zaidi ya yote hivi kweli naweza mrudia mtu wa namna hiyo?

Nasema hivi nitatekeleza mpango huu soon, labda ajiongeze arudishe hela yangu laki nne na nusu, hapo kwa mbaali tunaweza kutakiana maisha mema, akirudisha naweza kufikiria upya uamuzi wangu ingawa sina uhakika.

Nataka ajifunze, ajutie tabia mbaya ya usaliti, asirudie tena kumfanyia mtu mwingine akafikiri ata get away with it.

Mrejesho huu ni aina ya taarifa kwa kuwa Jana sikujibu chochote kwa yote mliyonishauri.
 
Umeshamuomba akirudishie hiyo pesa? Na kama umemwambia utamchomea unalo nae atahakikisha na wewe hauishi kwa furaha pia.
 
sasa huu mrejesho au mambo uliyopanga kufanya kwa huyo aliyekuwa msichana wako
 
Aisee, mimi bado nakusihi utumie busara kutibu mareha yako kuliko kulipa visasi, kunawatu wameishalipishana visasi mpaka kufikia kulishana sumu. Aidha, ukishafanikiwa kutekeleza matakwa yako itakubidi uwe makini sana na wadada kuna uwezekano akatumwa mmoja kukufutilia mbali haijalishi utakapokuwa.
 
Embu mtafute kwanza umueleze mpango wako huu. Anaweza timiza matakwa yako.
 
Wanawake wengine wana roho ngumu sana, huwa hawaamini km wanaume na sisi huwa tunaumia#

Uamuzi wa kumsamehe au kumchomea uko mikononi mwako, as well as unakuwa na amani ya moyo#
 
Maisha haya mafupi sana kuishi kwa visasi na ukimlipizia unaonyesha ulikwazika sana ama alikuwa ni mwanamke mzuri sana kiasi kwamba huwezi pata mwingine kama huyo.....Wachana nae tena labda amekuepushia tatizo kubwa mno maishani mwako kwa kuwa mbali na wewe....
 
  • Thanks
Reactions: Art
the best revenge is to move on and get over it. Don't give someone the satisfaction of watching you suffer!!!
 
Basi sawa..ngoja tuone na yeye atakuja na lipi..sijui kama bagamoyo wataiweza hii kazi namshauri aje huku Tanga
 
huyo shetani anaekumiliki kipindi hiki, ana power mno......ahakikishe unamvuruga uleyekuwa wampenda....ok go on boy....
 
Safi kijana jist go ahead tena wala usiongee nae...she has to know kuwa u dnt mess around na a mans heart nd just walk away.
 
Niliapa kushindana / kubishana na jinsia ya kike kwangu mwiko.....
 
may the lord grant someone a son who will be as dumb as the father! sijataja jina! khaa karma is a bitch watchout usije ukawa the next profound......
 
usisahau kuleta mrejesho part III ukishakinukisha na kusikia yanayojiri huko kazini kwake
 
Back
Top Bottom