Galadudu
JF-Expert Member
- Jun 23, 2014
- 2,304
- 780
Siku chache baada ya kupita sikukuu ya Pasaka niliwaelezea hapa jinsi nilivyokutwa zero distance na mke wa mtu, nyumbani kwa rafiki yangu.
Jamaa mwenye mke ni dereva bodaboda na mke wake ni Mnyarwanda mzuri sana yule dada. Nikasema kuwa jamaa baada ya kunikuta vile hajawahi kuniuliza chochote na mkewe pia hajawahi kumuuliza kitu kuhusu hiyo zero distance.
Mshtuko wangu sasa;
Mida ya jioni huwa napenda sana kutembea kwa miguu, labda tu kama cku hiyo kuna mvua, sasa jana nikiwa katika matembezi yangu hayo ya hiyari ikiwa ni saa moja za jioni, ghafla mbele yangu ikapaki pikipiki, kucheki vizuri ni ya yule jamaa.
Halafu akaniambia kiungwana kabisa 'twenzetu kaka nikusogeze mbele' nikamshukuru tu kwa lift yake halafu nikamwambia 'kuna ananipitia na gari kwa hiyo hapa nanyoosha tu miguu' eti jamaa akaanza kunibembeleza nipande pikipiki yake.
Baada ya majibishano ya hapa na pale akaondoka, sasa nikabaki najiuliza hivi ile lift ni ya heri kweli, kitu kingine nikajiuliza saa moja jioni huwa kigiza kimeanza, sasa yeye alinionaje akanifahamu na kama mnavyojua uendeshaji wa hawa jamaa huwa inakuwa ngumu kukutambua akiwa mwendo kasi.
Ikanifunukia akilini kwamba jamaa anafuatilia nyendo zangu kwa siri na nikaenda mbele zaidi kwa kujiuliza, hivi ningekubali kupanda pikipiki yake nini kingetokea mbele ya safari. Kuna hayo na mengi sana niliyokuwa najiuliza kuhusu huyo jamaa.
Waungwana hebu nisaidieni utatuzi wa hili