Mrejesho: Binti wa Sengerema aliyepotea

Mrejesho: Binti wa Sengerema aliyepotea

anasemaje Huyo bnti?
Yaani ndg mimi niliamini kuwa kwa vile kapotea basi haitachukua siku chache ndg zake watapatikana kwa vile huku si mjini kama Dar, Mwanza ama Kahama mjini. Naomba ikiwezekana nijulishwe gharama za ITV kumtangaza nione kama tamudu. Yaani nimejikuta hadi ratiba zangu zinachange kutokana na hili. Jana hadi anarudi alikuwa hajala chakula maji niliyompatia kamaliza japo nilimpa vijisenti kidogo vya njiani.
 
Huko unakokaa hakuna karismatiki kama wewe ni mkatoliki. Mpeleke kwa hao kama kuna kitu kitalipuka. La mpeleke kwa walokole
Ipo mkuu lkn kumbuka tofauti na kutokula usiku hana tatizo lolote la kiafya.
 
Ipo mkuu lkn kumbuka tofauti na kutokula usiku hana tatizo lolote la kiafya.
hutuendi kwa maombi kwa vile tunamatatizo tu. Lkn ni mara nyingi tunafikiri hatuna matatizo ilhali yanetufika hadi kooni. Au umefungwa usilione hili ambalo kila mtu analiona? Au unaogopa huenda yakaibuka hata kwako? Sikuelewi sana
 
Teh teh teh teh teh!! Anyway asanteni lkn hata mimi nasali kila siku ndugu zangu leo ni siku ya sita tangu nimchukue kama kumbukumbu zangu ziko sawa best.
 
Ni kweli jaribu kumpeleka kwenye maombi siku 2 aombewe kama hamna tatizo ishi nae kama mtoto wako kama bado umri wa kusoma unamruhusu mpeleke shule anaweza kuja kuwa Waziri huwezi jua, Mungu humtuma malaika wake kwa njia nyingi sana pengine hilo ni zali kutoka Mungu! Kingine cha muhimu cha kuzingatia ni afya yake kwenda kumpima kama anamagonjwa au laa!! Mungu akutangulie pamoja na familia yako!
 
Huyo mkeo mbona hajui kupika???mchuzi mweupe nyanya zinaelea...hazijaiva....uje sasa sahani hata kukupambia baba sahani kashindwa hata kuubanda....tu anyway huyo dogo panda nqe bus hadi sengerema mchangani mpeleke kwao kabla hujaja na mengine hapa...
Duh.....JF haiishiwi vituko
 
Mkuu nashukru sana kwa ushauri wako, mimi nilifanya vile nikiamini muda si mrefu tapata ndugu zake ukizigatia hata mimi ni mwenyeji wa Kanda ya ziwa (Shinyanga, Mwanza, Geita, Sengerema n.k). Ni kweli binti anaweza kuja aidha kunishutumu kwa kuweka picha zake lkn naweka kwa nia njema kabisa ya kumrudisha katika mikono salama. Ndugu haya maeneo tunayoishi 75% ni watu wanaotegemea madini kuendesha maisha hivyo nawafahamu tabia zao A-Z. Jumatatu nampeleka kituo cha polisi na kumkabidhi hapo. Taongea na polisi kama wazazi wake wakipatikana iwe huko Sengerema ama popote na wakilizia niishi nae mimi tampeleka tu shule hizi hizi za watu maskini ili angalau aje kufahamu umuhimu wa elimu, ni vigumu sana kuishi na mtoto wa watu pasipo kufahamu historia yake, hicho tu ndicho kinanisumbua akilini mkuu. Nasikitika sana watu wa Sengerema walioko hapa Jamii forum kushindwa kunisaidia hata namba za ofisi ya mbuge wao ili tu nipate mawasiliano na uongozi wa Mchangani. Kama ningepata nilipanga niwapate ndugu zake harafu nimkatie tiketi wampokee na tungeanza mawasiliano aidha wamuache kwangu asome ama wamsomeshe wao. Huku mgodini kama mtoto ana uwezo na wazazi hawapo huwa mgodi unawasomesha ngazi ya secondary hadi level zingine na uongozi wa hapa wasingekataa kupitisha jina lake maana nimemtoa mikononi mwao baada ya kukosekana mtu wa kumchukua siku hiyo.

kambagasa , kuwa mwangalifu. Jumatatu ni mbali sana. Mrejeshe huyo mtoto polisi haraka. Kuna mama mmoja miezi miwili iliyopita amepoteza mtoto wake kwa binti wa kupotea kama huyu. Alimpokea akamtunza kwa siku kadhaa. Siku moja alipomtuma dukani yule binti, mtoto wake akamlilia . Mwisho wakaondoka naye na ndo ukawa mwisho wa uhai wa yule mtoto. Huyo Binti unayekaa naye ana kila dalili ya kutumwa maovu na ndiyo maana ni mpole na jasiri.
 
0f944f8b98fc7c28941b089be61d367c.jpg
Siku chache zilizopita nilileta habari ya kupotea kwa mtoto (binti) aitwaye Prisca kutoka Sengerema sehemu iitwayo Mchangani. Hadi leo sijapata mawasiliano pamoja na baadhi ya wanajamii forum kuniahidi kunipatia mawasiliano ya mkuu wa shule Mchangani.

Polisi waliniambia nikute namtunza kwa siku chache wakiwa wanafanya mawasiliano lkn siku zinazidi kusonga pasipo mafanikio. Huyu binti tangu nimchukue tulishauriana na wife awe analala na watoto wangu kitanda kimoja kwani sipendi kabisa ubaguzi kulingana na maisha niliyopitia. Sasa tangu nimchukue nimegundua ni mtu mwenye akili timamu na mtu ambaye anapambanunua mambo kama mtu mkubwa.

Kuanzia ninapomuaga kwenda kwenye shughuli zangu na ninaporudi kwani mara nyingi anakuwa karibu sana na mtoto wangu mdogo 3yrs na 9 months. Lakini tabia ambayo imenifanya nirudi tena kwenu ni huyu binti kutokula chakula cha usiku (dinner) huku chakula cha asubuhi (kifungua kinywa) na kile cha mchana akila tena kwa furaha.

Jana wakati tunakula ilibidi nimuulize kwa nini usiku hataki kula akanijibu wamezoea kula mchana tu tangu azaliwe na hadi umri huu alionao kitu ambacho hakiingii akilini tena anakujibu akiwa flexible kabisa (anatabasamu)!!! Kumbuka mimi mwenyewe nimezaliwa na kukulia kijijini pamoja na maisha magumu lkn ilikuwa sharti kila familia tupate chakula cha usiku hata kama nichakugombania.

Jana hadi tunaanza kula na kumaliza binti alikuwa busy tu kucheki video. Nilijaribu kupiga picha kisiri pasipo frash.
cf8447c89a2b0aa57b09ee2248608d30.jpg
8d63dd2245d7c4784d692e2d659fcb58.jpg
Huyo binti si amekueleza anapotoka? kwanini husichukue hatua ukaenda nae mguu kwa mguu ukaujua ukweli? Use your Brain. Haya mambo ya huruma bila kutumia akili yamewafikisha wengine pabaya. Husikae na mtu husiyemfahamu kiholela, kama umepanga kumsaidia nenda atokapo jua ukweli A-Z then chukua hatua.
 
Ukiwa na hofu ya Mungu huku ukiamini kuwa yeye ndiye kila kitu katika maisha yako huwezi kuchukulia kwa umakini mkubwa baadhi ya michango ya wanachama. Tambua kuwa ni sehemu ngapi amepita? ni mangapi amekutana nayo? kwa nini Hili la kumsaidia Mungu alielekeze kwako? hutambui kuwa Mungu anamakusudi yake?
a
Michango baadhi ya wanajf inaakisi roho zao na jinsi gani wasivyomuamini MUNGU. Kwa mzazi yoyote hawezi kutishwa na kuaminishwa ushirikina. Endelea kuishi naye huku ukifanya mawasiliano na ndugu Zake. Hao wanaokwambia kuhusu UCHAWI nadhani Hawana IMANI na aliyewaumba
 
Kuwa makini zaidi na watoto, binadamu hatueleweki
Dunia yenyewe hii imevaa bikini hata kusaidia sasa tunaogopa maana mpaka watu kutoa tahadhali yamewakuta kama thawabu atafute kwa njia nyingine ila hiyo simuungi mkono ndo maana wahenga husema "wema unaponza "
 
Huyo binti si amekueleza anapotoka? kwanini husichukue hatua ukaenda nae mguu kwa mguu ukaujua ukweli? Use your Brain. Haya mambo ya huruma bila kutumia akili yamewafikisha wengine pabaya. Husikae na mtu husiyemfahamu kiholela, kama umepanga kumsaidia nenda atokapo jua ukweli A-Z then chukua hatua.
Nauli ya kutoka Dar hadi Sengerema
 
kambagasa , kuwa mwangalifu. Jumatatu ni mbali sana. Mrejeshe huyo mtoto polisi haraka. Kuna mama mmoja miezi miwili iliyopita amepoteza mtoto wake kwa binti wa kupotea kama huyu. Alimpokea akamtunza kwa siku kadhaa. Siku moja alipomtuma dukani yule binti, mtoto wake akamlilia . Mwisho wakaondoka naye na ndo ukawa mwisho wa uhai wa yule mtoto. Huyo Binti unayekaa naye ana kila dalili ya kutumwa maovu na ndiyo maana ni mpole na jasiri.

Ukiwa na hofu ya Mungu huku ukiamini kuwa yeye ndiye kila kitu katika maisha yako huwezi kuchukulia kwa umakini mkubwa baadhi ya michango ya wanachama. Tambua kuwa ni sehemu ngapi amepita? ni mangapi amekutana nayo? kwa nini Hili la kumsaidia Mungu alielekeze kwako? hutambui kuwa Mungu anamakusudi yake?
a
Michango baadhi ya wanajf inaakisi roho zao na jinsi gani wasivyomuamini MUNGU. Kwa mzazi yoyote hawezi kutishwa na kuaminishwa ushirikina. Endelea kuishi naye huku ukifanya mawasiliano na ndugu Zake. Hao wanaokwambia kuhusu UCHAWI nadhani Hawana IMANI na aliyewaumba
Nimempeleka tena leo baada ya jana kuwa safarini katika mihangaiko yangu.
 
Attachments

  • 1468998815336.jpg
    1468998815336.jpg
    78.5 KB · Views: 39
  • 1468998986386.jpg
    1468998986386.jpg
    87.1 KB · Views: 46
  • 1468999082210.jpg
    1468999082210.jpg
    59.1 KB · Views: 43
Breaking news : Prisca Michael kapata ndugu zake!!!

Nawashukru sana ndugu zangu hapa Jamii forum lakini namshukru sana wife na Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kuwapata ndugu wa Prisca.

ILIKUWAJE:
Leo nilimchukua tena Prisca hadi kituoni, nguo nilizokuwa nimemwandalia nilizificha kwenye kikapu kama vile naenda nae sokoni kuhemea chakula hata nguo aliyokuwa ameachiwa na wife bila kumtaarifu alikuwa amejifunga kama unavyomuona kwenye boda boda baada ya kupita tena ofisi ya kijiji na nikalipia usafiri hadi kituoni na baadae akachukuliwa wakiambatana na mtendaji (mshkaki). Baada ya lisaa limoja nikapigiwa simu kuwa Prisca kajulikana na ndugu zake na anatokea eneo la Nkome visiwani!! Baada ya maelezo nikiyoacha juzi kituoni na mwanzo kabisa wa kutoa taarifa Polisi wakitumia askari kitengo cha polisi jamii walifanikiwa kupata namba za mwalimu mkuu, mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kitongoji na baadae dada yake, mama yake, kaka yake na jirani yao kwa jina la Lutandula.
Prisca alitoroshwa yeye na rafiki yake na mama mmoja mfanyabiashara ya samaki hadi Kakola machimboni tangu mwezi wa pili mwaka huu!!
Ndugu zake wamepigwa butwaa na kuchanganyikiwa kutokana na maelezo na namna walivyokuwa wanaongea kwa sauti za juu huku Prisca akifurahi na kuzungumza namna walivyotoroshwa.
Ndugu zake walitaka kutuma nauli huku dada yake akisema abaki hapo hapo kituoni apande basi kumfuata!! Baadae tumeelewana nimchukue kwangu hadi kesho watakapofika kumchukua lakini ni baada ya polisi kuwaomba na hadi sasa nawasubiri polisi wanampitia huyu binti awapeleke kwa huyo mama kwani amedai anapafahamu na ndiko alimwacha mwezake baada ya kuteswa sana na yule mama aliyewatorosha. Hivyo Prisca si mchawi wala katumwa kwa ajili ya kunifanyia ubaya ila nashkru kwa tahadhari zenu maana wote hatukujua chochote. Kesho taongea na ndugu zake ili wakikubali niishi nae na aanze shule mara moja. Picha chini Prisca akiongea kwa simu na ndugu zake
1469006056340.jpg
 
Attachments

  • 1469006077914.jpg
    1469006077914.jpg
    75.3 KB · Views: 40
  • 1469006093800.jpg
    1469006093800.jpg
    75.3 KB · Views: 39
Breaking news : Prisca Michael kapata ndugu zake!!!

Nawashukru sana ndugu zangu hapa Jamii forum lakini namshukru sana wife na Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kuwapata ndugu wa Prisca.

ILIKUWAJE:
Leo nilimchukua tena Prisca hadi kituoni, nguo nilizokuwa nimemwandalia nilizificha kwenye kikapu kama vile naenda nae sokoni kuhemea chakula hata nguo aliyokuwa ameachiwa na wife bila kumtaarifu alikuwa amejifunga kama unavyomuona kwenye boda boda baada ya kupita tena ofisi ya kijiji na nikalipia usafiri hadi kituoni na baadae akachukuliwa wakiambatana na mtendaji (mshkaki). Baada ya lisaa limoja nikapigiwa simu kuwa Prisca kajulikana na ndugu zake na anatokea eneo la Nkome visiwani!! Baada ya maelezo nikiyoacha juzi kituoni na mwanzo kabisa wa kutoa taarifa Polisi wakitumia askari kitengo cha polisi jamii walifanikiwa kupata namba za mwalimu mkuu, mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kitongoji na baadae dada yake, mama yake, kaka yake na jirani yao kwa jina la Lutandula.
Prisca alitoroshwa yeye na rafiki yake na mama mmoja mfanyabiashara ya samaki hadi Kakola machimboni tangu mwezi wa pili mwaka huu!!
Ndugu zake wamepigwa butwaa na kuchanganyikiwa kutokana na maelezo na namna walivyokuwa wanaongea kwa sauti za juu huku Prisca akifurahi na kuzungumza namna walivyotoroshwa.
Ndugu zake walitaka kutuma nauli huku dada yake akisema abaki hapo hapo kituoni apande basi kumfuata!! Baadae tumeelewana nimchukue kwangu hadi kesho watakapofika kumchukua lakini ni baada ya polisi kuwaomba na hadi sasa nawasubiri polisi wanampitia huyu binti awapeleke kwa huyo mama kwani amedai anapafahamu na ndiko alimwacha mwezake baada ya kuteswa sana na yule mama aliyewatorosha. Hivyo Prisca si mchawi wala katumwa kwa ajili ya kunifanyia ubaya ila nashkru kwa tahadhari zenu maana wote hatukujua chochote. Kesho taongea na ndugu zake ili wakikubali niishi nae na aanze shule mara moja. Picha chini Prisca akiongea kwa simu na ndugu zake View attachment 367990
Hakukuwa na haja ya kumcholesha mtandaoni, ungeweka maelezo tu yanatosha.
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Iyo mtoto atakuwa muongo sana alishindwa nn kusema ayo yote toka mwanzo? Kumbe alikua anapakumbuka mpaka kwao (uyo mama alie muiba) kuwa makini bado binafsi simwamini

Ushauri kama ndugu wamepatikana acha achukuliwe na ndugu zake hope kwenye ukoo wako kunawatu wengi tu wakusomesha
 
Mwaka 2003 nikiwa naishi mkoa shinyanga wakati huo, nikiwa naelekea sokoni, nilikutana na mtoto mwenye miaka kama mitatu hivi, akilia kwa uchovu akionekana kutokwa na jasho la uchivu wa simanzi na kilio, nikabaini kuwa amepotezana na ndugu zake sokoni, nikaenda nae hadi polisi kulipoti tukio, polisi nikaambiwa "huwezi jua bahati kwako italetwa na nani, sisi hapa hatuna mahali tunapoweza kumtunza mtoto, nenda kakae nae, ndugu zake wakipatikana tutawaleta kwako.
Nilikaa na yule mtoto wiki tatu, nishamnunulia mavazi mazuri pea kadhaa, ndugu zake walipatikana, walipokuja kwangu walikuja na vitisho kuonesha kana kwamba niliwapora mtoto niliwakabidhi mtoto bila jasho kuepuka kurefusha maada isiyi na maana. Tenda wema tu ila usigeuke nyuma,zaidi kuwa makini na matukio kama hayo huwa yana mauzauza!
 
Back
Top Bottom