Mrejesho: Binti wa Sengerema aliyepotea

Mrejesho: Binti wa Sengerema aliyepotea

0f944f8b98fc7c28941b089be61d367c.jpg
Siku chache zilizopita nilileta habari ya kupotea kwa mtoto (binti) aitwaye Prisca kutoka Sengerema sehemu iitwayo Mchangani. Hadi leo sijapata mawasiliano pamoja na baadhi ya wanajamii forum kuniahidi kunipatia mawasiliano ya mkuu wa shule Mchangani. Polisi waliniambia nikute namtunza kwa siku chache wakiwa wanafanya mawasiliano lkn siku zinazidi kusonga pasipo mafanikio. Huyu binti tangu nimchukue tulishauriana na wife awe analala na watoto wangu kitanda kimoja kwani sipendi kabisa ubaguzi kulingana na maisha niliyopitia. Sasa tangu nimchukue nimegundua ni mtu mwenye akili timamu na mtu ambaye anapambanunua mambo kama mtu mkubwa. Kuanzia ninapomuaga kwenda kwenye shughuli zangu na ninaporudi kwani mara nyingi anakuwa karibu sana na mtoto wangu mdogo 3yrs na 9 months. Lakini tabia ambayo imenifanya nirudi tena kwenu ni huyu binti kutokula chakula cha usiku (dinner) huku chakula cha asubuhi (kifungua kinywa) na kile cha mchana akila tena kwa furaha. Jana wakati tunakula ilibidi nimuulize kwa nini usiku hataki kula akanijibu wamezoea kula mchana tu tangu azaliwe na hadi umri huu alionao kitu ambacho hakiingii akilini tena anakujibu akiwa flexible kabisa (anatabasamu)!!! Kumbuka mimi mwenyewe nimezaliwa na kukulia kijijini pamoja na maisha magumu lkn ilikuwa sharti kila familia tupate chakula cha usiku hata kama nichakugombania. Jana hadi tunaanza kula na kumaliza binti alikuwa busy tu kucheki video. Nilijaribu kupiga picha kisiri pasipo frash.
cf8447c89a2b0aa57b09ee2248608d30.jpg
8d63dd2245d7c4784d692e2d659fcb58.jpg
Hata sura ya huyo binti yaonesha ukomavu na uhodari katika mambo Fulani, nahisi kama unajaribu kudanganya janvi, haiwezekani binti huyo apotee na jamaa zake wasimtafute. Nasubiri mrejesho usiomtamu
 
Kaka umefanya mambo mengi, watu wengine wamechangia kwa almost Negative side, Je VIPI MTOTO huyu Kama labda ni malaika kaingia NYUMBANI MWAKO?? utajilaumu mpaka uzeeni yoote waliyosema watu hapa JF yanawezekana.

Lakini ulimwengu una surprise nyingi sana kwa Imani yangu MTOTO huyo ni NEEMA katika NYUMBA yako na SIO makosa wala laana mpende fanya chochote hapo NYUMBANI kwa kadri ya uwezo wako na Mungu atakubariki.
Tia moyo konde something good is coming on your way!!
 
Ndugu ningefurahi sana kumkabidhi kwa wazazi ama ndugu zake. Kuna watu nimewaelezea lkn mmoja amenishtua sana kwa kuniambia usije kuta usiku kanaenda kula uchawini!! Nimeogopa sana ila namwachia mungu
Mpeleke kwenye maombi wewe
 
Mwenzangu acha tu ndo maana tukaitwa wanawake tunaona vitu vingi kwa wakati mmoja....ila nimekasirika mke wa mleta mada food production and presentation negative kabisa
Hahah sio mchezo
 
mleta uzi ongera kwa ukarimu mkuu ila kuhus huyo mtoto kutokula ucku mmh..hilo c jambo la kawaida km wewe ni mkristo hakikisha mnasali pamoja kabla kulala ikowezekan mwalike mtumishi yyte wa kanisani kwako au unayemfaham afanye maombi kwa ajili ya familia ...bwana Yesu akurinde wewe na familia yko mkuu..

Safi sana mkuu,

Endelea kutoa fadhila, Mungu atakulipa, epukana na maneno yanayoweza kukuingiza katika dhambi.
Nimepeleka maelezo kituo cha polisi tayari, tumekuja na askari kitengo cha polisi jamii. Kesho namkabidhi polisi (mikono salama)
429b7fd4750727a8b1cc520e705389ff.jpg
 
Mkuu huyu mtoto mbona anaonekana kama mkubwa kuweza kujieleza kwa kirefu? Ameshindwa kukutajia wazazi wake ni kina nani? wanaishi wapi, yeye amefikaje hapo na maelezo mengine ya kina? Tafadhali jaribu kumbana kwa maswali ya kimtego unaweza kujua mengi. Anaonekana mpaka amepaka kucha rangi halafu asijue kujieleza! Halafu kuwa na tahadhari kwani siku hizi kuna utapeli wa aina nyingi.

Nimewaza hivyo pia, ukute ana malengo maalumu huyo binti, kamwe asiachwe mwenyewe na watoto. Hata kulala asingelala na watoto kwa kipindi hiki ambacho bado hawajamjua vizuri. Dunia ya leo usimwamini yeyote, hata kama mdau hapendi ubaguzi ni muhimu achukue tahadhari. Trust no one, even a devil was an angel.

Nakushauri usisubir jumatatu, fanya hima haraka sana. kuna jambo lilimtokea mwanangu mdogo baada ya kumwacha na dada wa kazi tena huyo house girk ni binti mdogo!!!!! Alipogundua nimejua aliruka ukuta na kutoroka.
Nimetoa maelezo kwa polisi idara ya polisi jamii bahati zuri amekuja hapa kijijini na nimempatia maelezo yote, kesho namkabidhi mikononi salama. (Polisi)
edcaed689807540466a86147dd7a39d0.jpg
 
Nikushauri tu ndugu yangu unakaa na mtu ambaye anatumika na watu ktk ulimwengu wa roho za kimajini mpeleke kanisani au msikitini utapata jibu na utashangaa hata watoto wako watapelekwa anakokwenda kula usiku bila wewe kujua na hao watu wanakula viapo sana ukishindwa hilo leta kwako walokole waliozama kiroho walaĺe hapo na usiku wafanye maombi utapata majibu.hongera kwa moyo wa huruma ila una mgeni ndani ya nyumba yako

Unamlaza stranger na watoto wako?
Hata kama ni huruma hiyo imezidi.

Kuwa makini zaidi na watoto, binadamu hatueleweki
Asanteni kwa ushauri wenu. Kesho tamsafirisha hadi kituo cha polisi. Maelezo yote nimeyatoa ya kutosha. Japo nimepewa kazi ya kumpata mtu wa kwanza kumuokota (kumchukua) na bahati zuri namfahamu. Kesho sitakuwa nae
 
Siku nyingine usirudie kosa la kulaza watoto wako na mtu baki
Evelyn nashukru sana kwa mawazo yako. Unajua dada maisha niliyokulia nilikuwa naona pale nyumbani wageni wanapokelewa (zamani sana) harafu tunalazwa pamoja na kula pamoja huku baba na mama akitufundisha kuishi kwa kujishusha na kutokubagua mtu. Nakumbuka siku moja mama alimpikia chakula mpita njia aliyekuwa anasafiri kwa mguu safari ya kwenda mbali. Miaka kibao ikapita yule mtu akaja nyumbani na zawadi nyiiiingi ikiwemo miko ya kusongea ugali na vitu vingi, sasa kila mtu alikuwa hakumbuki ndipo yule mzee akaelezea A-Z na akaomba kuwa ndugu na familia yake. So tangu siku hiyo huwa maisha ya duniani nayaona hayana maana yoyote na kila binadamu ninapomuona anateseka huwa nawaza hata wanangu yanaweza kuwapata na huwa nina ndoto kama kuna siku tatajirika nijenge kituo cha watoto yatima na wasiojiweza. Kuna miaka kazaa nilikuja Dar kununua bidhaa kariakoo asubuhi nawahi bus ubungo nikaona watoto wamejifunika maboksi kwenye mavaranda ya maduka!! Aisee niliwaza sana
 
Ni kweli lakini binadamu wa sasa tumekua hatari Sana kuliko unavofikiria, wasaidie tu ila watoto uwalinde ni heri ulale na wanao umwachie mgeni chumba, kwa kufanya hivo haimaanishi umembagua..
 
Ni kweli lakini binadamu wa sasa tumekua hatari Sana kuliko unavofikiria, wasaidie tu ila watoto uwalinde ni heri ulale na wanao umwachie mgeni chumba, kwa kufanya hivo haimaanishi umembagua..
Uko sahihi
 
Huyo mkeo mbona hajui kupika???mchuzi mweupe nyanya zinaelea...hazijaiva....uje sasa sahani hata kukupambia baba sahani kashindwa hata kuubanda....tu anyway huyo dogo panda nqe bus hadi sengerema mchangani mpeleke kwao kabla hujaja na mengine hapa...
Watu tunatofautiana aisee, kwani chakula umepikiwa wewe?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni kweli lakini binadamu wa sasa tumekua hatari Sana kuliko unavofikiria, wasaidie tu ila watoto uwalinde ni heri ulale na wanao umwachie mgeni chumba, kwa kufanya hivo haimaanishi umembagua..

Usifanye hivyo tena.
Japo wanangu wamezoea kama unavyomuona hapa(aliyesuka) (wakicheki tamthiliya) lakini kesho ndo basi tena
f044ba4ffd2b6f2340214d451eb871f9.jpg
 
Ni wanawake ambao hata majirani huwa wanajuta kuishi nao mtaa mmoja.
Achana changu asiye na adabu, chukua mawazo yanayokufaa mengine tupa kuleee, suala la chakula halina uhusiano na lengo la uzi huu
 
Back
Top Bottom