mcrounmj
JF-Expert Member
- Feb 26, 2016
- 380
- 885
Habari za mda huu mabilionea wa sasa na wajao. Tumaini langu mnaendelea vema na harakati za kutimiza ndoto zenu.
Ni kama mwezi nilikuja kuomba msaada kwa wajasiliamali wenzangu juu ya biashara ya dhahabu. Nishukuru watu walitoa uzoefu wao, wapo walionitaadhalisha juu ya songombingo zilizopo kwenye biashara hiyo.
Wa kukatisha tamaa hawakosekani nao hawakuwa haba, ila tu nishukuru wapo memba walonitia moyo kwa kunishauri nini hasa nikifanye nikiwa mgeni kwenye kada hii ya madini.
Kwa sababu mtaji wangu ulikuwa around 5ml, niliamua kuanza na million 2 kwanza ili niusome upepo nikiwa najifunza. Kusema ukweli katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia nilipoanza hali ya kibiashara siyo mbaya.
Nimeweza kuisogeza milion 2 hadi 3 ndani ya mwezi. Hivyo nimepata faida ya million moja. Hii ni hatua nzuri kwangu kwa siku za mwanzo.
Pamoja na hayo tahadhar mimeweza kuichukua na naendelea kuichukua. Nimejiwekea sheria sinunui mawe, bali nanunu dhahabu iliyochomwa na kui-grade, hivyo probability ya kupoteza hela ni ndogo.
Changamoto pia nakutana nazo kama kupungua sana uzito ukipeleka jikoni kuyeyusha, asilimia ya dhahabu kusoma chini na wachimbaji wanaokuja kuchukua advance kisha wanapotea mazima hivyo hela kupotea.
Karibuni mabroker wenzangu tu share ups and down za hii biashara.
Biashara ya madini ya dhahabu.