Mrejesho: Baada ya kuujaribu uchawi wa "Chuma Ulete"

 August 15, 2017  Deusdedit Mahunda
BAADA ya kusikia simulizi mbalimbali kuhusiana na ‘chuma ulete’ kwa muda mrefu, nikaamua nijaribu ili niweze kurahisisha maisha. Nilitamani sana zile hadithi za ‘chuma ulete’ ziwe kweli juu yangu. Ninunue bidhaa kisha fedha zinirudie, zikiwa nyingi zaidi. Nile bila jasho.
Baada ya mawazo hayo, siku chache zilizopita nikaamua kwenda kwa mganga mmoja wilayani Bagamoyo ambaye alisifika kwa kutengeneza utaalamu huo.
Nilifika kwa mganga, nikavua viatu kisha nikaingia ndani. Kama kawaida mganga alinikaribisha kwa mapambio ya ‘kilozi’. Zilipigwa chafya nyingi zilizosindikiza maneno yasioeleweka.
Kabla sijamweleza shida iliyonipeleka pale, mganga akaanza kubashiri: “Kijana una matatizo makubwa, mambo yako hayaendi kuna watu wanakuchezea… umekuja kumtambua anayekufanya ushindwe kupiga hatua… “
Mganga mtaalamu, mlozi aliendelea kuongea mambo mengi ambayo sikuhusiana nayo, nilipoona anazidi kupotea, nikamweleza shida iliyonipeleka: “Mzee nimekuja kwa shida moja tu, nataka unipe uchawi wa chuma ulete, nipate pesa bila jasho.”
Mtaalamu alicheka sana, kabla hajatoa tiba akaniomba niweke shilingi laki mbili ndani ya bakuli kubwa lililokuwa umbali mdogo kutoka usawa wa mapaja yake. Nilitembea na fedha ya kutosha, nikaweka kiwango alichotaka.
Alifurahi alipokiona kitita cha fedha, akatamka maneno ambayo sikuyaelewa, kisha akachukua kitu mfano wa kunde, akakimeza. Akajitikisa kidogo akakitapika, akachukua kipande cha mti, akanuia maneno fulani, baadaye akatoa kitambaa chekundu kilichokuwa na unga mweupe. Alipomaliza hayo, akachanganya vitu vyote katika kitambaa chekundu, akakifunga vizuri na kukishona kwa sindano ya mkono.
“Chukua dawa yako!” alinikabidhi kwa sauti ya kukoroma, “dawa hii nakupa, ukienda dukani, ukitoa noti ya shilingi elfu kumi, mwenye duka atakurudishia elfu ishirini, ukitoa elfu tano, utarudishiwa elfu kumi, pia baada ya muda, fedha zake zitaanza kuhamia kwako. Nenda kijana.”
Niliagana na mganga nikiwa na furaha ya kutoka kimaisha. Nilifika nyumbani usiku, nikalala nikiwa na shauku ya kuanza mkakati wa utajiri asubuhi.
Asubuhi ilifika, nikaenda dukani nikiwa na noti ya shilingi elfu kumi. Nikanunua vocha ya elfu mbili. Nilitegemea mwenye duka angenirudishia elfu ishirini kama nilivyoelezwa na mganga. Haikuwa hivyo, nilipewa fedha kamili, elfu nane!
Nilijaribu duka jingine bila mafanikio. Hakuna fedha iliyozidi. Nikachoka, nikarudi nyumbani kulala.
Mpaka sasa nimejaribu kununua vitu katika maduka mengi bila kile nilichoahidiwa na mganga kutokea. Na sasa nimeamini kuwa nilitapeliwa na siamini tena kama kuna kitu kinaitwa ‘chuma ulete.’ Huu ni uongo tu! Mjinga mimi, mganga kala laki mbili yangu bure!
Mamaayakoangeona haya angekutoa tumboni miezi minne
 
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14]
 
Peleka mrejesho kwa mganga. Kakinukishe, mfuate na panga, mchimbe mkwara mzito, mwambie dawa zako feki rudisha pesa yangu!
 
BAADA ya kusikia simulizi mbalimbali kuhusiana na ‘chuma ulete’ kwa muda mrefu, nikaamua nijaribu ili niweze kurahisisha maisha. Nilitamani sana zile hadithi za ‘chuma ulete’ ziwe kweli juu yangu. Ninunue bidhaa kisha fedha zinirudie, zikiwa nyingi zaidi. Nile bila jasho.
Baada ya mawazo hayo, siku chache zilizopita nikaamua kwenda kwa mganga mmoja wilayani Bagamoyo ambaye alisifika kwa kutengeneza utaalamu huo.
Nilifika kwa mganga, nikavua viatu kisha nikaingia ndani. Kama kawaida mganga alinikaribisha kwa mapambio ya ‘kilozi’. Zilipigwa chafya nyingi zilizosindikiza maneno yasioeleweka.
Kabla sijamweleza shida iliyonipeleka pale, mganga akaanza kubashiri: “Kijana una matatizo makubwa, mambo yako hayaendi kuna watu wanakuchezea… umekuja kumtambua anayekufanya ushindwe kupiga hatua… “
Mganga mtaalamu, mlozi aliendelea kuongea mambo mengi ambayo sikuhusiana nayo, nilipoona anazidi kupotea, nikamweleza shida iliyonipeleka: “Mzee nimekuja kwa shida moja tu, nataka unipe uchawi wa chuma ulete, nipate pesa bila jasho.”
Mtaalamu alicheka sana, kabla hajatoa tiba akaniomba niweke shilingi laki mbili ndani ya bakuli kubwa lililokuwa umbali mdogo kutoka usawa wa mapaja yake. Nilitembea na fedha ya kutosha, nikaweka kiwango alichotaka.
Alifurahi alipokiona kitita cha fedha, akatamka maneno ambayo sikuyaelewa, kisha akachukua kitu mfano wa kunde, akakimeza. Akajitikisa kidogo akakitapika, akachukua kipande cha mti, akanuia maneno fulani, baadaye akatoa kitambaa chekundu kilichokuwa na unga mweupe. Alipomaliza hayo, akachanganya vitu vyote katika kitambaa chekundu, akakifunga vizuri na kukishona kwa sindano ya mkono.
“Chukua dawa yako!” alinikabidhi kwa sauti ya kukoroma, “dawa hii nakupa, ukienda dukani, ukitoa noti ya shilingi elfu kumi, mwenye duka atakurudishia elfu ishirini, ukitoa elfu tano, utarudishiwa elfu kumi, pia baada ya muda, fedha zake zitaanza kuhamia kwako. Nenda kijana.”
Niliagana na mganga nikiwa na furaha ya kutoka kimaisha. Nilifika nyumbani usiku, nikalala nikiwa na shauku ya kuanza mkakati wa utajiri asubuhi.
Asubuhi ilifika, nikaenda dukani nikiwa na noti ya shilingi elfu kumi. Nikanunua vocha ya elfu mbili. Nilitegemea mwenye duka angenirudishia elfu ishirini kama nilivyoelezwa na mganga. Haikuwa hivyo, nilipewa fedha kamili, elfu nane!
Nilijaribu duka jingine bila mafanikio. Hakuna fedha iliyozidi. Nikachoka, nikarudi nyumbani kulala.
Mpaka sasa nimejaribu kununua vitu katika maduka mengi bila kile nilichoahidiwa na mganga kutokea. Na sasa nimeamini kuwa nilitapeliwa na siamini tena kama kuna kitu kinaitwa ‘chuma ulete.’ Huu ni uongo tu! Mjinga mimi, mganga kala laki mbili yangu bure!
Umekutana na tapeli zamani sana kunamzee aliwahi kunifundisha ila sikutilia maanani ninachokumbuka alikua na kitabu kidogo cha uganga unatafuta paka mweusi asie na doa unamchinja na kumchuna ngozi yake unaanika unakata kipande kidogo kwakutumia kile kitabu kuna maandishi unaandika kwenye ilengozi unifunga kwenye azima unavaa kichwani unaenda kwenye kioo kikubwa unanuia mpaka taswira yako inapotea kwenye kioo hujioni hapo ndio unatoka unaweza kuingia duka lolote ukafungua droo na kutoa hella mashart yake hutakiwi kuchukua hella yote kama kuna laki unachukua 30. Maaajabu nilio wahi kushuhudia mzee huyu tulikua tunaenda kama klmt 3 kwa mguu mvua kubwa ikaanza kunyesha kuna maalifa anafanya nvua anakaa pembeni peke yake ananuia ile mvua inaruka mnakua kama mnaifuata mpaka mnafika hadi watu wanauliza vp mbona hamjanyeshewa wakati huo mlipo toka ni pori tu hamna nyumba. Miaka ya nyuma simba walikua wengi simba wanalia ye anatoa baiskeli kwenda kijiji jirani kunywa pombe wakati huo nyunba za nyasi onaona kamasimba anaweza kuchomoa ndani ni babu yangu r.i.p
 
Tumejifunza katika huu utunzi wako kuwa hauko makini. Maana kama mganga alikosea utabiri wa shida iliyokupeleka kwake dhahiri ni tapeli na ulikubali kutapewa kwa hiari yako.

La pili tulilojifunza ni kuwa uko na fedha za kutosha atleast kwa mtazamo wako. Sijui hela/fedha za kutosha huwa ni ngapi?

Halafu unabahati sana kuingia kwa kuvua viatu tu, kwa wataalamu wengine sharti ni kuvua nguo zote na ubaki kama ulivyozaliwa na ungie kwa kutanguliza makalio. Na hayo makalio anayashughulikia kwa kutumia jini wake, aka popobawa. Una bahati maana ungekuwa sio riziki mantashari tena.
 
Kwa tamaa uliyonayo, nakuapia utaua watoto ili upate pesa.

Nakushauri ukatupe punje ileje ili mwisho ufe mwenyewe.
 
BAADA ya kusikia simulizi mbalimbali kuhusiana na ‘chuma ulete’ kwa muda mrefu, nikaamua nijaribu ili niweze kurahisisha maisha. Nilitamani sana zile hadithi za ‘chuma ulete’ ziwe kweli juu yangu. Ninunue bidhaa kisha fedha zinirudie, zikiwa nyingi zaidi. Nile bila jasho.
Baada ya mawazo hayo, siku chache zilizopita nikaamua kwenda kwa mganga mmoja wilayani Bagamoyo ambaye alisifika kwa kutengeneza utaalamu huo.
Nilifika kwa mganga, nikavua viatu kisha nikaingia ndani. Kama kawaida mganga alinikaribisha kwa mapambio ya ‘kilozi’. Zilipigwa chafya nyingi zilizosindikiza maneno yasioeleweka.
Kabla sijamweleza shida iliyonipeleka pale, mganga akaanza kubashiri: “Kijana una matatizo makubwa, mambo yako hayaendi kuna watu wanakuchezea… umekuja kumtambua anayekufanya ushindwe kupiga hatua… “
Mganga mtaalamu, mlozi aliendelea kuongea mambo mengi ambayo sikuhusiana nayo, nilipoona anazidi kupotea, nikamweleza shida iliyonipeleka: “Mzee nimekuja kwa shida moja tu, nataka unipe uchawi wa chuma ulete, nipate pesa bila jasho.”
Mtaalamu alicheka sana, kabla hajatoa tiba akaniomba niweke shilingi laki mbili ndani ya bakuli kubwa lililokuwa umbali mdogo kutoka usawa wa mapaja yake. Nilitembea na fedha ya kutosha, nikaweka kiwango alichotaka.
Alifurahi alipokiona kitita cha fedha, akatamka maneno ambayo sikuyaelewa, kisha akachukua kitu mfano wa kunde, akakimeza. Akajitikisa kidogo akakitapika, akachukua kipande cha mti, akanuia maneno fulani, baadaye akatoa kitambaa chekundu kilichokuwa na unga mweupe. Alipomaliza hayo, akachanganya vitu vyote katika kitambaa chekundu, akakifunga vizuri na kukishona kwa sindano ya mkono.
“Chukua dawa yako!” alinikabidhi kwa sauti ya kukoroma, “dawa hii nakupa, ukienda dukani, ukitoa noti ya shilingi elfu kumi, mwenye duka atakurudishia elfu ishirini, ukitoa elfu tano, utarudishiwa elfu kumi, pia baada ya muda, fedha zake zitaanza kuhamia kwako. Nenda kijana.”
Niliagana na mganga nikiwa na furaha ya kutoka kimaisha. Nilifika nyumbani usiku, nikalala nikiwa na shauku ya kuanza mkakati wa utajiri asubuhi.
Asubuhi ilifika, nikaenda dukani nikiwa na noti ya shilingi elfu kumi. Nikanunua vocha ya elfu mbili. Nilitegemea mwenye duka angenirudishia elfu ishirini kama nilivyoelezwa na mganga. Haikuwa hivyo, nilipewa fedha kamili, elfu nane!
Nilijaribu duka jingine bila mafanikio. Hakuna fedha iliyozidi. Nikachoka, nikarudi nyumbani kulala.
Mpaka sasa nimejaribu kununua vitu katika maduka mengi bila kile nilichoahidiwa na mganga kutokea. Na sasa nimeamini kuwa nilitapeliwa na siamini tena kama kuna kitu kinaitwa ‘chuma ulete.’ Huu ni uongo tu! Mjinga mimi, mganga kala laki mbili yangu bure!
Wewe sio mjinga, ni ktk kupambana na maisha, lolote linaweza kutokea. Kwani hujawai kuona mtu anainvest mamilioni ya pesa ktk biashara na hafaanikiwi? Sembuse laki mbili!, Mimi nakushauri hivi simamia unachoamini mpaka ufaànikiwe usikatishwe tamaa na wajinga wachache wanaotaka wakitaka kitu wapate muda huohuo. Uchawi huo upo, haiwezekani vizazi na vizazi wawewanazungumzia au kulalamikia uchawi huo, alafu nyie vijitu vya dotcom eti mjifanye mnaakili kuliko babu na mabibi yaliyopita. Ni ile hali ya mu Africa tu, ya kutojikubali, lkn Mimi naamini lazima utakuepo, tu.
 
Nikiwa mdogo, niliwahi kuonyeshwa Mzee mmoja Mtaani, ambae yeye ni mpigaji ktk maduka ya watu kwa kutumia CHUMA ULETE! Mzee yule alihama mtaa baada watu wote kugoma kufanya na mihamala!
 
Duuuh akili yko kma yule jamaa anaeshangaa mtu kwenda likizo nje ya nchi na familia yke,yani anaroho ya umaskini kma wewe
 
Uchawi uwa haupo ispokuwa uwa kuna ujanja ujanja tu hapa duniani.....pole sana kamanda
uchawi upo kaka hata kwenye vitabu vya dini umeainishwa, pia ukumbuke uchawi ni uwezo unawezeshwa na shetani,so huenda huyo jamaa alitapeliwa ila uchawi upo na watu wengi wenye maduka hasa ambao hawana ulizi wa kiimani husumbuliwa na hiyo chuma ulete
 
Chuma ulete ipo ilikupata wewe na imefanikiwa si hivyo umechuma ukapeleka kwa mganga ndio Chuma ulete yenyewe hito
 
Back
Top Bottom