Mradi wangu umefeli, hivyo hii nadharia ni sahihi au tuipuuze?

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
Habari wanajf..

Leo nahitimisha rasmi kuwa nadharia ya ANZA NA ULICHONACHO siyo sahihi baada ya mradi wangu kufeli.

LENGO:kuzalisha vifaranga 30 kwa kutumia mitetea 3

MRADI:UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

Mradi wangu niliazimia kuanza namitetea mitatu ambayo niliitunza na kuiandaa kwa ajili hiyo waliobaki wawili walikuwa ni majogoo.

MAANDALIZI YA MRADI

Niliandaa sehemu tatu tofauti za kuatamia mayai kwa aili ya kuku hawa watatu.

Nilitengeneza mfano wa box la wavu kzunguka sehemu ya kuatamia na niliweka chakula na maji, hii ililenga kuzuia kuku kutokatoka.

Banda dogo nilitengnza kwa mabox na wavu nalo lilikaa chumbani kwangu, hili lilikuwa maalum kulelea vifaranga. Lilitosha vifaranga 40 hivi.

Mahindi kwa ajli ya kutwanga ili kupta pumba za kulisha

Dawa za asili kama vile mwarubaini na magome ya mkorosho.

Chombo cha kutoa joto kwa vifaranga jiko dogo la mkaa.

UTEKELEZAJI WA MRADI

Mitetea ilianza kutaga kwa kupishana wiki moja na siku tano

Mtetea wa kwanza alianza kuhatamia akiwa na mayai 12, niliondoa mayai yote nikabakisha moja tu, mayai 11 nilihifadhi.

Mtetea wa pili alianza kuatamia akiwa na mayai 14, niliondoa yote nikabakisha yai 1, mayai 13 yalihifadhiwa.

Mtetea wa tatu alianza kutmia akiwa na mayai 9.

Kila mtetea nilimpatia mayai 10, hivyo wte watatu wakawa na jumla ya mayai 30.

MATOKEO.

Wakiiishana siku tatu hadi tano mayai 25 yalianguliwa mayai 5 hayakuanguliwa.

Vifaranga 25 walianza maisha bila mama zao.

CHANGAMOTO

Baada ya wiki tatu akiba ya mahindi ikawa imekwisha tatiz la chakula likaibuka, nililazimika kutafuta mahindi mengine hata hivyo bado ikabaki kuwa changamoto kwani fedha ilikuwa ni tatizo.

Gharama za mkaa, nililazimika kuchoma mkaa kiasi ili kuhakksha vifaranga vinapata joto nishati.

Ktokana na changamoto ya chakula vifaranga 3 walikufa,

Wa2 walikufa baada ya kuugua.

Nshati nayo bado ikawa changamoto.

MABADILIKO YA PLAN
Sasa nilijaribu kumweka mtetea mmoja ili awe anawatunza wtoto, aliishia kuwadonoa tu na kuua wawili hivyo wakabaki 18

Kila mtetea aliwadonoa hivyo nikalazmika kumrudishia kila mtetea vifaranga vyake kwani ni wazi vingekufa kwa njaa na baridi.

Changamoto ya paka na mwewe imefanya mitetea miwili kupoteza vifaranga wte kwa sasa vimebaki vitano kwa mtetea mmoja.

Mteea mmoja amefanywa supu ya iddi jana

HITIMISHO

Kuanza na ulichonacho ni nadharia dhaifu sana na inawafanya watafutaji kuonekana wazembe na wavivu kuanza hustler

Ukweli ni kwamba almost all hustler zinahitaji Fund,nadharia hii haiwezi kulikwepa hilo wala haiwezi kufanya kazi bila PESA.

PESA ni almost ufunguo wa kila kitu, mfano katika huo mradi bla pesa hakunachakula, madawa waa vifaa muhimu. Ikumbukwe nimeufanya kwa kuzingatia nilichonacho.

TUHITAHIDJ KUWEZESHANA PANAPOBIDI KWA TULICHONACHO SIO SAHIHI KUSHUSHUA NA KUWAONA WATU NI WAVIVU NA KUPAZA SAUTI "ANZA NA ULICHONACHO WEWE"

WENGINE HUSEMA UZA SIMU, ELIMU YA KIJAMII NI MUHIMU SANA, NISINGEKIUJU HUU MRADI KAMA SIYO SIMU, NA ACTUALLY SIMU HAIFIKI HATA 20 ELFU.

Miradi hii ni mepesi katika maratasi tu uhalisia ni kisanga.

Naimani wenye ndoto za ufugaji wa kuku wa kienyeji wanaweza jifunza kupitia mbinu hii.
 
Shida hapo ilikuwani
1) Uzoefu mdogo wa kutunza vifaranga waliototolewa. Niliwahi kufanya huo mradi kwa kuanza na kuku 7 na wilifika hadi 800 ndani ya mwaka mmoja. Ila batch ya kwanza ya vifaranga ilikufa kalibu yote ndo nilajifunza makosa. Baada ya kurekebisha makosa kazi ilikuwa nyepesi.
2. Kukata tamaa. Ulitakiwa ujue wapi ulikosea urekebishe na usonge mbele.
3. Mtaji. Hii kazi inahitaji nguvu ya kuanzia licha ya kuanza na kuku wawili ulikuwa na uwezo wa kuzalisha vifaranga 15 kwa mwezi na baada ya miezi 6 ndo ungeanza kupata mapato. Kwa kipindi chote hicho ni kuwekeza
3. Hukupata ushauri bora wa ufugaji ndo maana ulipoteza vifaranga kwa magonjwa, mwewe nk. Hayo yote lazima yawepo kama unataka kufanya biashara ya ufugaji kama uliokuwa umepanga. Mauzo yakiisha anza pesa yako inarudi. Na ukiwa na hizi factors hata mkopo unakuwa na uhakika wa kuuhudumia. Kilanla kheri
 
Mkuu wewe ulikurupuka Mimi mwaka Jana mwezi wanane nilinunua Kuku mmoja alitotoa kundi la kwanza chini yauangalizi wangu watoto kumi natatu wakapona Tisa mpaka Leo ninavyoongea wameanza kutaga wawili,

Kundi la pili akatotoa kumi namoja mpaka Leo ninao wote hao

Kundi latatu nikampiga double yaani alivyototoa nikachukua watoto nikamuwekea mayai hawa ninao wote
Bahati mbaya mwizi akamuiba akiwa chini yauangalizi wakutotoa kundi la nne ko Kuku mmoja akawa amenipa vifaranga 30 ko nimeamua kuwekeza rasmi kwenye huu mradi baada ya experiment kuleta majibu positive
Naaanza na hili kundi lakwanza nalifanyia modification kwakuwapa mayai yakikenya ili nitoe product yenye soko ko naamini umechemsha kidg tu unahitaji kukaa na MTU anaeweza kukutia moyo nakukufanya uendelee zaidi
 
Mkuu hoja ipo katika kuanza na ulichonacho

Mimi nimeanza na niIchokuwa nacho tu.

Je! Mradi waweza tekelezeka bila kuwa n fedha?

Unaweza kutazama hapo sikufeli kwa sababu sina plan thatbiti hapo failure zilikua kutoana na

Ukosefu wa nishati joto ya kutosha muda wote(fedha za kununua mkaa)

Fedha za dawa na chanjo(sikuwapa dawa wala chanjo kutokna na fedha)

Ukosefu wa chakula

Je! Katika mazingira kama hayo nadharia ya kuanza na ulichonacho inatekelezeka vipi?
 
Mkuu wewe ulikurupuka Mimi mwaka Jana mwezi wanane nilinunua Kuku mmoja alitotoa kundi la kwanza chini yauangalizi wangu watoto kumi natatu wakapona Tisa mpaka Leo ninavyoongea wameanza kutaga wawili,

Kundi la pili akatotoa kumi namoja mpaka Leo ninao wote hao

Kundi latatu nikampiga double yaani alivyototoa nikachukua watoto nikamuwekea mayai hawa ninao wote
Bahati mbaya mwizi akamuiba akiwa chini yauangalizi wakutotoa kundi la nne ko Kuku mmoja akawa amenipa vifaranga 30 ko nimeamua kuwekeza rasmi kwenye huu mradi baada ya experiment kuleta majibu positive
Naaanza na hili kundi lakwanza nalifanyia modification kwakuwapa mayai yakikenya ili nitoe product yenye soko ko naamini umechemsha kidg tu unahitaji kukaa na MTU anaeweza kukutia moyo nakukufanya uendelee zaidi
Mkuu unaweza elezea utunzaji wa hao vifaranga?

Waliwezaje kusurvive wote?

Na mradi wako umefikia wapi kwa sasa(expansion/dvelopmnt)
 
Mkuu cha msingi kikubwa zaidi Kuku wadg wanahitaji usafi zaidi ya mwanamke alie period hio ndo siri yamafanikio yakuku cha pili typhoid ndo inawaua sana vifaranga cha tatu jitoe Kwa hali na Mali bora ukose bando sio Kuku kukosa chakula
 
Mkuu unaweza elezea utunzaji wa hao vifaranga?

Waliwezaje kusurvive wote?

Na mradi wako umefikia wapi kwa sasa(expansion/dvelopmnt)
Ninampango wakuipiga bei hii smartphone yangu nitanue mradi maradufu nizalishe Kuku mia tu wakunipa mayai 50 kila siku tayari nimeona mradi huu unalipa Kwa kiasi kikubwa faidi ni asilimia 70 %
 
Nataka kujua unavyotunza vifaranga hadi waweze kusurvive wengi hivyo.

Ninampango wakuipiga bei hii smartphone yangu nitanue mradi maradufu nizalishe Kuku mia tu wakunipa mayai 50 kila siku tayari nimeona mradi huu unalipa Kwa kiasi kikubwa faidi ni asilimia 70 %
 
Siongei Kwa mihemko au kuvutia wengine waingie shimoni hapana naongea nikimaanisha hata Kuku wakienyeji pure akilishwa vizuri anataga ndani ya miezi minne mpaka mitano full stop ushahidi sijahadithiwa nimefanya experiment Mimi mwenyewe kundi
 
Dah aisee nimependa namna vifaranga wanavyosurvive..

Chakula na dawa nilijaribu kuanza na dawa za kienyeji na mahindi niliyovuna hapa nje.

Monthly sina uwezo wa kuearn hata 2000, hivyo kupata yale madawa ilikua changamoto, chakula nacho ni changamoto.

Bando kaka lina siri nyingi mimi hununuliwa bando la elfu mbili kwa mwezi na mtu ambae hufanyia kazi kama cotent manaer katika app yake kwa malipo ya muda wa maongezi wa 2000 tu

Kwa sasa wakat huu mitetea hajanza kutaga najaribu kuangalia namna navyoweza kuconduct hii issue licha ya changamoto hizo

Mkuu cha msingi kikubwa zaidi Kuku wadg wanahitaji usafi zaidi ya mwanamke alie period hio ndo siri yamafanikio yakuku cha pili typhoid ndo inawaua sana vifaranga cha tatu jitoe Kwa hali na Mali bora ukose bando sio Kuku kukosa chakula
 
Mkuu mitetea wangu wawili nlionao hutaga mwezi tu baada ya kuacha vifaranga, inamaanisha kuwapokonya vifaranga wiki mbili tu wanaanza kutafuta maeneo ya kutagia ni kweli kabisa tuna nafasi ya kufanya kitu na hawa kuku wa kienyeji hasa ukipata mtetea mzuri hutaga sana.
Siongei Kwa mihemko au kuvutia wengine waingie shimoni hapana naongea nikimaanisha hata Kuku wakienyeji pure akilishwa vizuri anataga ndani ya miezi minne mpaka mitano full stop ushahidi sijahadithiwa nimefanya experiment Mimi mwenyewe kundi
 
Mkuu mitetea wangu wawili nlionao hutaga mwezi tu baada ya kuacha vifaranga, inamaanisha kuwapokonya vifaranga wiki mbili tu wanaanza kutafuta maeneo ya kutagia ni kweli kabisa tuna nafasi ya kufanya kitu na hawa kuku wa kienyeji hasa ukipata mtetea mzuri hutaga sana.
Mimi simpi nafasi yakubanduka kwenye kiota akibanduka namuweka kitu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom