Mradi wa maji Butimba kukamilika December mwaka huu badala ya februari 2023

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la msingi Mradi wa chanzo cha Maji Butimba Ujenzi wenye kiasi cha Shilling Bilion 69.3.
Katika hatua nyingine ametembelea Mradi huo na kuzungumza na wananchi pamoja na Wafanyakazi katika eneo la Mradi Butimba leo Tarehe 14 September 2022.

Aidha, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi kuwa mradi huu utakamilika December mwaka huu badala ya February mwaka 2023 kama ilivyokuwa imepangwa awali akisisitiza kuwa wakandarasi watafanya kazi usiku na mchana pamoja na kuongeza nguvu kazi ili dhamira na malengo hayo yaweze kutimia.

 
Back
Top Bottom