Mradi wa mabasi wa DART jijini Dar-es-Salaam,2015 uliipatia CCM ushindi wa kata na majimbo mangapi dhidi ya wapinzani?


S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
31,735
Likes
64,602
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
31,735 64,602 280
Mradi huu wenye mabasi makubwa na miundombinu ya barabara inayojumuisha madaraja ya wapita kwa miguu,nakumbuka ulianza kufanya kazi/kutumika mwishoni mwa mwaka 2015 kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Nakumbuka mabasi ya DART yalianza kuonekana yakifanya safari za majaribio kipindi cha mwezi wa 8 au wa 9 na hapo baadhi ya jamaa zetu wakajua mradi huu ungeweza kuwapa ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 katika mkoa wa Dar-es-Salaam.

Kilichotokea mwaka 2015 kila mtu ni shahidi kuwa kwa mara ya kwanza jiji liliongozwa na upinzani baada ya wapinzani kushinda viti vingi vya udiwani na hata ubunge tofauti na chaguzi za miaka ya nyuma.

Nachotaka kuwaambia hawa wenzetu kuwa miradi mikubwa pamoja na umuhimu wake kwa wananchi,haiwezi kuwafanya wananchi kusahau matatizo yao ya msingi na zaidi watambue vitu hivi baada ya muda huzoeleka machoni pa watu na kuonekana kuwa ni vya kawaida tu.

Njia pekee ya kukubalika kwa wananchi ni kutatua kero hasa za kiuchumi zinazogusa wananchi moja kwa moja kama vile kudhibitii mfumuko wa bei,kuondoa kodi ambazo ni kero,n.k

Mambo mengine ni kudhibiti rushwa kwa vitendo na bila kuangalia sura, kutatua kero za upatikanaji wa maji, kuboresha huduma za afya,kutatua matatizo ya elimu kama vile utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu,n.k..

Mengine ni kutatatua kero za watumishi wa umma kama vile kupunguza PAYE,kuongeza mishahara ya watumishi wa umma na kulipa madai ya watumishi.

Matatizo mengine ni kama yale ya kunyanyasa wamachinga, wafanyabiashara,kutotatuliwa kwa migogoro ya wakulima na wafugaji, kuporomoka kwa bei ya mazao, wakulima kuzuiliwa kuuza mazao yao nje ya nchi,kukosena kwa pembejeo za kilimo,n.k

Hiyo ni mifano michache ya mambo ambayo ndio yanagusa wananchi moja kwa moja na ambayo yakitekelezwa vizuri chama kilichoko madarakani kinakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi.

Wasichoelewa hawa ndugu zetu ni kuwa, haya mambo mengine yote yana effect ya muda tu machoni pa watu na baada ya muda huzoeleka na yanakuwa hayana influence tena kwa wapiga kura wanaoteseka na kuumizwa na matatizo ya kiuchumi na kukosekana kwa huduma za msingi za kijamii kama vile afya,elimu,maji,umeme,n.k

Mwananchi anaeteseka na shida ya maji hawezi akakupa kura kwasababu tu akifika mjini anapita kwenye daraja la juu au anakutana na fly-over.

Mwananchi ambae mazao yake yanaharibikia shambani kwa kukosa soko na mwenye kujitambua hawezi akakupa kura kwasababu tu amesikia umenunua ndege.

Mwanafunzi aliekosa mkopo na anaehangaika na maisha mtaani na mwenye kujitambua, hawezi kukupa kura kisa anasafiri kwa reli ya kisasa.

Mwananchi aliekosa ajira na asie na matumaini hawezi kuvitiwa na maendeleo ya vitu ili hali mfukoni mwake hana kitu.

Jitahidini ku-balance mambo vinginevyo mtakuja kujilaumu na kusema hawa watu huenda hawana shukrani.

Asie sikia la mkuu,huvunjika guu.
 
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
4,003
Likes
1,443
Points
280
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
4,003 1,443 280
Tatizo kubwa tulilonalo ni KUJISAHAULISHA
 
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
3,466
Likes
4,313
Points
280
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
3,466 4,313 280
Yule msemaji wao si aneshaanza kusema kuna mengine yaliingia Maji juzi kazi kati kwenye ile mvua kama robo dumu tu. Yamesitisha safari mpaka yatengenezwe. Sasa unashindwa kuelewa wao eneo lile walihamisha wana nchi kwa kigezo hicho sasa sikuwaelwa walipohamia wao?
 
MOTOCHINI

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Messages
24,483
Likes
13,108
Points
280
MOTOCHINI

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2014
24,483 13,108 280
Hii nayo Mada!!
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
21,586
Likes
63,394
Points
280
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
21,586 63,394 280
Duh
Kweli umeishiwa..
Subiri 2020 mkione cha moto na kufifia kwenu kwa kutokuwa na nondo za kuvutia watu.
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
29,051
Likes
75,249
Points
280
Age
18
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
29,051 75,249 280
Walishasema hatuna ajenda ngoja tuwaache na drama zao.
 
Isanga family

Isanga family

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Messages
6,080
Likes
5,804
Points
280
Isanga family

Isanga family

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2015
6,080 5,804 280
ila kuhusu usafiri kwa kiasi fulani wamejitahidi kutatua hiyo kero ilikua ni siku unamaliza kutoka kimara mpaka Kkoo na kurudi kwa hilo tuwape pongezi tuu...na kama njia zote watafanya hayo ni jambo jema sana...
 

Forum statistics

Threads 1,235,892
Members 474,827
Posts 29,239,679