Mradi wa kuulinda uoto wa asili jiji la Dar es Salaam

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
2,606
3,399
Hapa Muhimbili kitengo cha tiba asili. CHIPE nikihudhuria semina kuhusu kongamano la ku zisema urejeshaji wa uoto wa asili katika mij hii inayokua kwa kasi, mada ikitolewa na manguli wa tasnia china ya ICLEI.

Kwa nini katika majumba yetu kila mtu asianze kupanda miti katika eneo lake ya asili ya eneo hilo ya matunda? Katika mashule yetu kusipandwe tu miti isiyokuwa na faida miashok mfano, ipandwe miti ya matunda mfano mienmbe, mizambarau miukwaju kwanza itatunza uoto wa asili pili watoto watafaidika.

Katika mipango miji katika majiji kutengwe maeneo yatayokuwa na mimea ya kila aina ya asili inayopatikana pale kuwekwe utulivu mabench watu wawe wanaenda kurelax, mjeruman wakat wa ukolon alianzisha kitu kinaitwa botanical garden ile kitu ilikua muhimu sana sana. Leo botanical garden sijajua zipo maeneo mangap.

Ndege wa asili wamefukuzwa na haya makunguru wezi wa vitu. ila Dar ilikua ni eneo la ndege wa asili kabisa. Kila mtu aweke nia panda mipera kwako, panda muembe panda ukwaju panda komamanga kulingana na eneo lako tubadilike mfano ndege Basra Red water anatoka Syria anakuja had Kunduchi.

Muhimu kuwe na miti ya asili inayowapa ndege mazingira yao.
 
Back
Top Bottom