Mradi wa bandari ya Tanga ulifia wapi?

Tanga ilikufa mwaka 90 na kitu kweny miaka 2000 na kitu wagosi wa kaya waliimba ile kunani pale tanga mbona kila kitu kimekufa

Baadhi ya viwanda na wawekezaji walikimbia kenya hata anjari aliambiwa ahame dar akakataa akasema bora asiwekeze izi zote ni juhudi na hujuma

Inashangaza barabara ya kwanza ya lami ,shule ya kwanza, mahakama ya kwanza kila kitu kule ila nyerere alikuja kuua kabisa sababu tunajua aliona kule ni waislamu wengi kama Zanzibar

Na kupandikiza propaganda za kuwaita wavivu tunajua sisi wa ukanda wa bara tuna imani zetu na tamaduni zetu ndo maana leo wengine hawamtaki rais samia kisa mzenji
 
Msimsingizie Nyerere watu wa Tanga uvivu umewazidi. Na kupenda fitina zaidi kuliko kutanguliza ubinadamu, nongwa nyingi sana Tanga mjini.
 
Hakuna asiyeujua umuhimu wa bandari kwa maendeleo mapana ya nchi yoyote iliyojaliwa kuwa nayo.

Tunaweza kushabihisha umuhimu huo kwa kuangalia mifano halisi ya bandari zilivyochochea uchumi wa mataifa kama Singapore, Vietnam, Malaysia (bandari ya Klang), China (bandari za Dalian, Xiamen, Guangzhou na hata Shenzhen), Korea ya Kusini (bandari ya Busan) na hata Ujerumani (bandari ya Bremen na Hamburg) na hata Marekani yenyewe (angalia bandari ya New Jersey kama mfamo mojawapo).

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana nchi zote duniani ambazo zimejaliwa bandari hujitahidi sana kuboresha ufanisi wa bandari zao ili kuvutia biashara, mapato na uwekezaji mkubwa zaidi wa kimkakati katika nchi zao na hivyo kuchochea maendeleo zaidi katika mataifa yao.

Kutokana na taarifa zinazoendelea kusambaa kuhusu kumpatia bandari ya Dar es Salaam mwekezaji binafsi aiendeshe kwa kibwagizo kwamba itakuwa na ufanisi zaidi imenifikirish sana na kuikumbuka bandari ya Mwambani, Tanga na kunifikirisha zaidi kuhusu mradi wake wa uendelezaji kwa manufaa mapana zaid ya taifa letu.

Sitataka sana kuijadili bandari ya Dar es Salaam na umuhimu wake kwa uchumi wa taifa letu siku ya leo (hii ni mada ya siku nyingine na nitaieleza kwa kirefu) licha ya ukweli kwamba ni bandari ambayo zaidi ya asilimia 95 ya biashara ya nchi hupitia hapo, lengo langu mimi kwa siku ya leo ni kuijadili bandari ya Tanga.

Kwa nini nimeikumbuka sana bandari ya Tanga tena enzi za serikali ya awamu ya sita?

Tuwekane wazi, ukiwauliza wataalamu wa maritime au shipping kiujumla watakueleza kwamba bandari ya Tanga ni kati ya potential ports tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu katika taifa letu kwa sababu ni moja ya bandari za asili kabisa (usiifananishe na bandari ya Dares Salaam ambayo kwa kiasi kikubwa imechimbwa sana) na ndio maana ina kina kirefu sana kiasili ukilinganisha na ile ya Dar es Salaam.

Pamoja na hayo eneo lake la uendelezaji ni kubwa sana ukilinganisha na lile la Dar es Salaaam kwani sehemu kubwa ya bandari ya Dar es Salaam imeshazungukwa na makazi na site za biashara za watu mfano matenki ya mafuta na maghala ya uhifadhi ya makampuni binafsi.

Hivyo kama litaendelezwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kupokea container ships kubwa maarufu kama small feeders, feeders, feedermax na baadaye panamax na ultra-large vessels baada ya uendelezaji mkubwa baadaye (labda phase three na phase four ya kuendeleza Tanga port). Meli hizi huwa na uwezo wa kubeba kontena 300 - 1000 kwa meli moja na nyingine hubeba mpaka kontena 3000 kulingana na mzigo uliopo.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba Tanga port inaweza kuizidi bandari ya Dar es Salaam uwezo wa kupokea mizigo na meli kubwa zaidi yake hivyo tunaweza kuwa na container terminal kubwa zaidi kuliko ile iliyopo bandari ya Dar es Salaam inayoendeshwa na TICTS kwa sasa (fursa nyingine mpya kabisa kwa sekta binafsi na hata wakazi wa mkoa wa Tanga). Hatua hiyo itaongeza mapato zaidi kwa serikali na hata ajira na biashara kwa wakazi wa jiji la Tanga (hoteli, migahawa, makazi, uhifadhi, usafirishaji na hata viwanda hasa ukizingatia Tanga ina potential kubwa sana ya kuwa industrial city kubwa zaidi Tanzania.

Lakini pamoja na potentialities zake kama nilivyoeleza hapo awali sijasikia kabisa bandari hii ikizungumzwa tangu awamu ya nne ya H. E. Jakaya Kikwete baada ya kubadili upepo na kwenda bandari ya Bagamoyo. Sintofahamu iliendelea tena pale awamu ya tano chini ya Hayati Magufuli kutokuiongelea kabisa.

Awamu ya sita chini ya mama SSH (Chief Hangaya) haijalisemea hili jambo kabisa na badala yake imeisemea zaidi bandari ya Bagamoyo licha ya mradi huo kuendelea kusua sua mpaka sasa.

Taarifa za tamko (uvumi) la kuibinafsisha bandari ya Dar es Salaam iendeshwe na mwekezaji binafsi zimeniibua nikitaka kujua kwa mapenzi mema tu (kama mtanzania mwingine) ni kitu gani kimeikumba hii bandari ya Tanga kiasi cha kuifanya isiendelezwe na kupigwa dana dana na kila awamu na hata kupotezewa kabisa (kama ilivyo sasa).

Napenda kujua ni nini kinaendelea kuhusu bandari hii. Mbona tumeitupa kiasi hiki wakati inaweza kuhudumia wateja wetu kama Rwanda, Burundi, Uganda na hata Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ?
Sio mafuta, malighafi za viwanda na hata bidhaa adimu kama cement na nondo zinaweza kupatikana na kusafirishwa kwenda kwa hawa jirani zetu kupitia bandari hii ya Tanga.

Kwa nini haiendelezwi ? Mbona kama imetupwa vile ? Mradi huu umefia wapi ?

Naomba tujuzane wakuu.

Nawasilisha
Mnataka bandari ili muende wap ,tutawakuta huko huko TANGA
 
Umeelezea habari muhimu sana,kwa uchumi wa Taifa.
 
Msimsingizie Nyerere watu wa Tanga uvivu umewazidi. Na kupenda fitina zaidi kuliko kutanguliza ubinadamu, nongwa nyingi sana Tanga mjini.
we mshamba wa wapi🤣🤣🤣 unajiongelea tu kule watu wamestaarabika wakarimu hakuna tanzania bila ya watu wa pwani we na mzee wote mngekuwa na magovi the more unakaa far kutoka pwani the more unakuwa hauna ustaarabu ushawai kusikia ukeketaji tanga tangu uzaliwa na kizazi chako

hakuna mvivu kule watu wana dili na uvuvi wanaingia shift za usiku sasa we jaribu kuingia zile kazi kama hautokufa
kwanza mpaka unaongea ni chuki ebu wacha majungu na umbea tafuteni maji safi kwanza ndo maana meno ynaharibika
 
Tanga sio wavivu,wanalisha visiwa vya Zanzibar,Pemba,Comoro,Siyeshels,Madagascar,Mombasa kwa viazi,vitunguu maji,vitunguu saumu,nyanya,mboga mboga,nafaka aina zote,maharage,mahindi,mpunga,nk.
 
we hupajui ukisikia raha roho inakuuma jiangalie kama wakiume ukiwa na chuki za ivi utakuja kufa mapema na umaskini punguza ushamba kule ubaguzi no ,majungu huko kwenu tafuteni maji safi n salama muache kunywa maji yanawhaaribu meno milele unaleta shobo
 
Watu wa Tanga sio wavivu.Ni wakulima,Wafugaji,Wavuvi wa samaki.Tanga wanalisha visiwa vya Zanzibar a,Comoro,Siyeshels,Madagascar,Mombasa na Tanga yenyewe kwa Viazi,nyanya,vitunguu maji,vitunguu saumu,mbogamboga,Karoti,pilipili hoho,mihogo,nk na nafaka aina mbali mbali kuanzia mahindi,maharage,mahindi,mtama,mpunga,nk.Hakuna mtu wa Tanga,aliye ombaomba.Kativu uvuvi,wanavua samaki,wanauza na kusafirisha mikoani.Ufugaji wa ng'ombe,mbuzi,Kondoo,Kuku na samaki wa kufuga pia wanafuga.Mbali na kilimo cha mkonge,kilimo cha biashara.
 
Ni vile wametawaliwa kiujanja ujanja tu,
Siku akili zikiwakaa sawa, wataendelea kupitiliza, wana bandari, border, ardhi safi, madini, vyanzo vya utalii, mafuta na hata gas
Kwamba wewe sio Mtanzania na kwenda huko unahitaji Passport ?

Kwanini usiende ukafanye hayo yote ?
 
we hupajui ukisikia raha roho inakuuma jiangalie kama wakiume ukiwa na chuki za ivi utakuja kufa mapema na umaskini punguza ushamba kule ubaguzi no ,majungu huko kwenu tafuteni maji safi n salama muache kunywa maji yanawhaaribu meno milele unaleta shobo
Nimeishi Tanga 2004- 2007 ninapajua sana na aina ya watu wake ninaifahamu pia. Nimeamua kuwa mkweli tu.
 
Tanga sio wavivu,wanalisha visiwa vya Zanzibar,Pemba,Comoro,Siyeshels,Madagascar,Mombasa kwa viazi,vitunguu maji,vitunguu saumu,nyanya,mboga mboga,nafaka aina zote,maharage,mahindi,mpunga,nk.
Unaongelea nje ya mji, wilaya zingine. Wapo Wasambaa ndio wanaoibeba heshima ya mkoa.
 
we mshamba wa wapi🤣🤣🤣 unajiongelea tu kule watu wamestaarabika wakarimu hakuna tanzania bila ya watu wa pwani we na mzee wote mngekuwa na magovi the more unakaa far kutoka pwani the more unakuwa hauna ustaarabu ushawai kusikia ukeketaji tanga tangu uzaliwa na kizazi chako

hakuna mvivu kule watu wana dili na uvuvi wanaingia shift za usiku sasa we jaribu kuingia zile kazi kama hautokufa
kwanza mpaka unaongea ni chuki ebu wacha majungu na umbea tafuteni maji safi kwanza ndo maana meno ynaharibika
Tanga unakwenda dukani saa tano asubuhi kununua soda, unakuta mtoto mdogo anakwamba kaka Juma alalaaa.

Yaani Juma alivyokuwa mvivu kafungua tu duka halafu karudi kulala!. Unabaki kushangaa huyo mtu analalaje wakati muda huo ni joto kali.
 
Back
Top Bottom