Choosen85
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 562
- 1,363
Wakuu kuna rafiki yangu alikuwa anafanya kazi mkoani Mbeya sasa alipigiwa simu na kaka ake kwamba kuna mradi upo Mwanza huko atalipwa vizuri sana.
Huyo kaka mtu akamwambia anatakiwa awe na passport ya kusafiria, achome chanjo ya manjano jamaa akapambana akakopa mpk kwa jamaa zake ili akamilishe hayo mambo maana ndugu yake alimwambia vinahitajika haraka sana. Na siku si nyingi anatakiwa akaripoti huko mwanza tyr kwa kazi.
Jamaa mkataba wa kazi ulipoisha huko Mbeya hakuongeza mkataba zaidi alifunga safari kwenda Mwanza akafikia kwa rafiki yake wakati akisubiri kuanza kazi huku akiwa kauza kila kitu alichokuwa nacho Mbeya. Huo mradi ofisi zao zipo maeneo ya Mecco Mwanza inasemekana eti ni mradi wa mgodi wa madini pia mambo ya watoto na wamama pia mambo ya ukimwi.
Cha ajabu toka mwaka 2019 mpaka leo hii jamaa hao hapo ofisini wamekuwa wakitoa taarifa zisizoeleweka kabisa jamaa anateseka sana anajuta kutoongeza mkataba huko alikotoka kwani huo mradi hapo Mwanza miaka inakatika hakuna jipya zaidi ya sound tu mara waambiwe kuna hela za makabiziano mara kuna hela za uzinduzi wa mradi mara kuna magari ya mradi yapo Mombasa yaani ni ujinga ujinga tu hakuna cha maana.
Mara waambiwe siku fulani watakuwa wamewekewa pesa kwenye akaunti zao siku ikifika kinatafutwa kisingzio hapo inapita miezi tena jamaa ni mwaka wa tatu anateseka huko Mwanza kashaomba msaada kwa jamaa zake mpaka wamemchoka anaona aibu hata kurudi Mbeya.
WAKUU MLIOKO MAENEO YA MEKO MWANZA HAPO JE NI KWELI KUNA KUNDI LA WATU HUWA WANAONEKANA HUKO AU MITAA HIYO WAKISUBIRI KUANZA KWA MRADI HUO MIAKA NENDA RUDI. TUONE ABC za kinachoendelea hapo maana nasikia wengine walichomwa chanjo ya covid kwa lazima ili tu wawe kwenye mradi.