Mr Magufuli atua Kivukoni, kuzuia nauli mpya?

Status
Not open for further replies.
Nice point mkuu kwani pale ferry ni bora hata kwa ndugu tega wa TFF kwa jinsi wanavyotuibia. Labda leo hii huyo Dr wenu akusanye mapato yeye mwenyewe then jioni atupe hesabu kapata kiasi gani.
Shilling mia kimsingi haiwatoshi watumishi wote wa pale(Mkatisha tiketi, mchana tiketi, mfungua geti la abiria, yule mdada kwenye microphone, mfungua mnyororo,polisi, suma jkt, mafundi,,,,,,,,,) yaani ni wengi mmno na wanaushirikiano sana yaani huwezi sikia kerere yeyote pale jamaa wanaishi kwa upendo mno na wala hawazurumiani. Ili mgao uwatoshe labda waongeze nauli mpaka buku mbili


Kingine hata mkisema waenda kwa miguu walipe sh 500 bado haitawatosha pale ferry kuna watu zaidi ya 4 wote wanalinda hiyo sh 100 pale kuna Temesa,askari polisi,suma jkt security guard,wanajeshi yaani ulinzi wa pale ni zaidi hata ya wizarani
 
Bora Dr magufuli aingilie kati,kama ni swala la makusanyo tatizo c bei ya naul ila ni wizi unaofanywa na wao wenyewe.for instance kwa siku they collect more than 12mill but they submit less than 8mill.huo ni wizi hatukubali nauli kupanda.
 
Yaani wakiacha nauli mpya kwenda kigamboni ni anasa kabisa....bajaj 1,300/ baiskeli 1000/ Pick up 2000/ yaani hatari sana

Mkuu baiskeli ndizo zinatuletea madafu huku mjini sasa kama nauli itakuwa 1000 ina maana jamaa hawataki tule madafu? Manake ikiwa hivyo bei za.madafu nazo zitaongezeka!
 
nilifikiri ni kazi ya waziri wa uchukuzi

waziri Nundu
Mkuu vivuko vipo chini ya TEMESA ambayo ipo chini ya Wizara ya Ujenzi, hivyo waziri mwenye dhamana ya vivuko ni Waziri wa Ujenzi. Lakini cha kujiuliza inakuwaje hao jamaa wanapandisha nauli za kivuko bila waziri kuwa na taarifa? Suala la kupandisha nauli ya vivuko ni suala la kisera hivyo wakala hawezi kuamua kupandisha bila wizara kuwa na taarifa. Nashangaa kwamba waziri hakuwa na taarifa na sasa ameenda kuzuia mbele ya vyombo vya habari!
 
Suluhisho pekee pale ni DARAJA tu.
Kwanini ujenzi wa daraja unasua sua kila kukicha!
 
Updates!

Taarifa iliyotolewa hapa nikuwa Waziri mkuu Mh Pinda ni kuwa amesitisha nauli mpya za vivuko!
Hii ni kwa mujibu wa mr Magufuli PM
 
by MTIMUAVUMBI
Njia mojawapo ya kudhibiti wizi hapo ferry ni kuweka mashine inayotoa tiketi kwa kutumbukiza pesa.Wasafiri ni lazima waje na chenji kamili inayo lingana na nauli yake.Pesa yote itakuwa inakusanywa ndai ya mashine. Mashine inapo kuwa imejaa pesa, zinaondolewa na kupelekwa Bank.
 
tatizo sio nauli mpya. Ni udhibiti wa mapato yenyewe. Hata watoze laki kama mapato hayadhibitiwi ni upuuzi kuongeza bei. Badala ya kukata mti wanakata matawi!
 
Mb wa kigamboni aliweka wazi wizi unaofanyika pale
1.Mafuta wanauza kwa wenye maboti madogo
2.Wanakua na Ticket bandia hela inaenda mifukoni mwao
3.Kuna watu pale wanavuka kama VIP(wanapita geti la kutokea mda wowote kwa ajili ya kukwepa foleni na kuvuka haraka) hela wanapeleka kwa mwezi
 
Waziri wa ujenzi John Magufuli amekwenda kivukoni kutuliza hali ya hewa baada ya uongozi wa vivuko hivyo kupandisha nauli zaidi ya asilimia miamoja bila sababu za kueleweka!
Nitawajuza habari zaidi baadae!

Updates!

Taarifa iliyotolewa hapa nikuwa Waziri mkuu Mh Pinda ni kuwa amesitisha nauli mpya za vivuko!
Hii ni kwa mujibu wa mr Magufuli PM

Huyu jamaa si anajifanyaga anajua gharama, urefu, muda wa kuisha etc wa kila daraja hapa nchini??
basi na atuambie lile daraja letu la kigamboni litaisha lini!!!!!!!!
 
mia mbili tu ndo wanalalamika? sasa maisha bora kwa kila mtanzania yatatoka wapi?
 
hacheni utoto, sh. 200 mnalia nini? mbona sisi uku sengerema kwenye kivuko tunalipa sh.300? hacheni utoto lipeni nauli kama hamtaki vukeni kwa kuogelea
 
Jaman, gharama za uendeshaji zimeongezeka. Mia 2 sio haba. Mia hata chumvi hupati. Sehemu nyingine wanalipa zaid za mia mbili. Tusiwe watu wa kulaumu kila kitu
 
Mimi nipo kigamboni na leo tumelipa 200 hakuna kusitishwa kwa bei mpya mbunge jana kaongopewa na waziri mkuu pamoja na mkuu wa mkoa kuwa bei itabaki ya zamani!!!
 
Waziri wa ujenzi John Magufuli amekwenda kivukoni kutuliza hali ya hewa baada ya uongozi wa vivuko hivyo kupandisha nauli zaidi ya asilimia miamoja bila sababu za kueleweka!
Nitawajuza habari zaidi baadae!

Updates!

Taarifa iliyotolewa hapa nikuwa Waziri mkuu Mh Pinda ni kuwa amesitisha nauli mpya za vivuko!
Hii ni kwa mujibu wa mr Magufuli PM
Kilichompeleka ni kuweka mkazo kuwa nauli mpya zianze kutumika na sio kusitisha
 
Magufuli jana aliamua kuwabwatukia walalahoi wa kigambon kuwa endapo wanahisi nauli ya kivuko ni kubwa basi 'wapige mbizi',
Sosi:mwananchi newspepa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom