Mr Magufuli atua Kivukoni, kuzuia nauli mpya?

Status
Not open for further replies.
Miafrika ndivyo tulivyo.. watu wakiamua kufanya kazi mnawazomea.. kosa la maghufuli nini hapo? Tuwe wakweli.. pamoja na ulegelege wa kukusanya mapato pale kivukoni kama mbunge na wadau wengine wanavyojaribu kutetea ila sh 100 jamani tangu 1995??!

Nchi hii watu wanapenda kuchekewa chekewa tu.. ndio maaana tupo hapa tulipo naskia na waziri mkuu kasitisha hizo bei mpya.. huu ni uendawazimu na upuuzi kuliko yote! kwa hili Pinda kakosea sana ndio maana watu wamekufa mabondeni kwa ajili ya upuuzi huu huu wa kuchekea na kutaka kumfurahisha kila mtu
 
1. Wanaosema TRC haitoi huduma nzuri, they can GO TO HELL;
2. Kila Mtu atabeba MSALABA wake;
3. NDEGE ya Rais lazima innunuliwe hata kama wananchi watakula NYASI;
4. Asiyeweza kulipa nauili mpya APIGE MBIZI.

Hizi ni baadhi tu ya KAULI za viongozi wetu hasa tunapolalamikia baadhi ya maamuzi yao. Yatubidi tukubaliane nao tusonge mbele kwani TUMESHAZIZOEA. Wa TZ hatuchelewi kusahau, tutaji-adjust accordingly.
 
nauli ya feri kigamboni ni tofauti na ushuru wa 200 ubungo bus terminal, hii hutokea mara chache kusindikiza wageni ubs, lakini feri ya kigamboni ni sawa na mtu kupita barabarani halafu unatozwa nauli, kama ni hivyo kila daraja liwekewe vizuizi ili kila mtu achangie gharama za ukarabati na watumishi wa barabarani, tufike mahali tutofautishe huduma na biashara kwenye vitu vya msingi. shame on you mapadlock

hAPO NIMEKUPATA MKUU. wATU WENGINE WANASHI KIMAPOKEO KILA WANACHOAMBIWA WANAKUBALI TU . HAWANYI "ANLYSIS' NI JUKUMU LA SERIKALI KUHAKISHA WATU WAKE WANAFIKA MAENEO YOTE MUHIMU BILA KIKWAZO. KULE KENYA MOMBASA NCHI YA KIBEPARI (SISI TUNAJIDAI NI WAJAMAA) WANANCHI WATEMBEA KWA MIGUU KUPANDA NI BURE, MAGARI NDIO YANALIPIWA. KATIKA UKURASA HUU NIMETOA MAONI YANGU ILI WENGINE WACHANGIE TANGU IJUMAA, LAKINI HAKUNA MICHANGO NADHANI SIJAELEWEKA-ILA CHA MSINGI UAFANYIKE UCHUNGUZI KUONA NI MAPATO KIASI GANI YANAPOTEA KWA YALE MAGARI YA MAAFANDE YA KIRAIA NA YA RAIA WENGINEO AMBAYO HAYALIPII NAULI HALALI YA KIVUKO BALI KITU KIDOGO KWA MAAFANDE, WAANGALIE TICKET FEKI-KWA SABABU HAKUNA UTHIBITI-(KIHASIBU KWA UJUMLA TUNAITA (WEAKNESS IN INTERNAL CONTROL) BAADA YA TICKET KUUZWA NI NYARAKA GANI ITAKUJA KUKAGULIWA NA WAKAGUZI, NA FEDHA ZIKIISHA FIKA KWA WAKUBWA WANAZI WASILISHA HAZINA KAMA ZILIVYOKUSANYWA NA NI NYARAKA ZIPI (SUPPORT DOCUMENTS) ZINAAMBATANA NA MAKUSANYO HAYO, MWISHO WANGALIE ENEO LA MANUNUZI YANAYO TOKANA NA FEDHA HIZO. SIO KUKURUPUKA TU KUPANDISHA NAULI. HAO WANAOTETEA MAAMUZI HAYO HAWAATHIRIKI. TUNGEKUWA NA MIUNDO MBINU BORA WANGEWEZA KWENDA MAKAZINI KWA KUTUMIA HELIKOPTA BADALA YA KUBANANA NA SISI KATIKA PANTONI WAKIWA NDANI YA MA-VX ,BMW N.K.
 
Watanzania tuache kulalama, nauli hata iwe 1000 pouwa mbona kwa siku tuna kunywa pombe na kuhonga wanawake zaid ya 1000.
 
Hebu acheni HOJA ZISIZO NA MSINGI dhidi ya Magufuli humu!! Kuwa eti, hakushirikisha WADAU!Loh! kwani yote yanayofanyika humu Bongo mnashirikishwa?Nani alishrikishwa kuwa ukitaka kuingia stendi ya Ubungo ulipie 200?Nani alishirikishwa katika kupandisha nauli ya Vivuko mto Ilagala maeneo ya Kigoma?Nani alishirikishwa katika nauli za vivuko vya Mwanza, Pangani, Kilombero nk? Toeni hoja zenye mvuto siyo kuja na hoja za ushirikishwaji ambao kwa TZ haupo! tuwe realistic jamani! Kwani Mwaka 1994 wakati wa gharama ya Tshs 100 wananchi walishirikishwa?Angalieni hali halisi halafu muwaachie Viongozi wafanye kazi.
Kila siku humu katika JF watu wanamlaumu JK kuwa yeye na watendaji wake hawafanyi kazi na wanashindwa kuchukua MAAMUZI MAGUMU! sasa maamuzi yamechukuliwa mnalia tena
Tuache kuhusisha maamuzi anayotoa Magufuli na siasa ya kuwa eti anafanya hivyo kwa sababu anataka URAIS! hoja kama hizo hazina mashiko. Kwani ndo mmeambiwa kuwa mtu akitaka kuwa Rais ageuke kuwa KONDOO?Halafu nynyi wa TZ kila mtu mnampakazia kuwa eti kwa sababu anataka kuwa Rais, kwani ni kosa watu kugombea nafasi ya U-RAIS?

Haya siyo mambo ya kutupotezea muda kuendelea kulumbana nayo humu ndani. Yapo mambo ambayo nadhani ni ya Msingi kuyajadili lakini siyo hili.

Japouny;
Nakubaliana na wewe kuwa sisi watz tunashabikia sana juu ya kutaka serikali kuchukua MAAMUZI MAGUMU lakini ukiangalia kiundani utabaini kuwa wananchi hatuko tayari kwa hayo maamuzi magumu.Lazima tukubali kuwa kama tunataka maamuzi magumu lazima tuwe tayari kuyatumikia.Kwa mtindo huu itakuwa ngumu sana kwa Tz kuendelea.
 
Ni aibu serikali yetu baada ya miaka 50 bado inatoza ushuru kwa wenda kwa miguu kwenye vivuko. Nauli ingetozwa kwa mikokoteni na magari lakini sio kwa waenda kwa miguu na baiskeli. Shame on us. Kwanini miaka yote hio wasijenge daraja?
 
Jamaa huyu mie najua ni mropokaji wa muda mrefu na si kiongozi mzuri sana kama watu wanavyofikiria..lakini hili la kusema nauli lazima zipande kama huwezi piga mbizi uvuke ni kauli ya aina yake inayotia shaka uelewa wa huyu jamaa.Viongozi wasiojali masilahi ya wananchi licha ya hali ngumu ya maisha yanayowakabili hawatufai, kauli hizi tata si za magufuli peke yake wapo wengi kuanzia kwa kina mramba,mkapa na wengineo je ni dharau? au ulevi wa madaraka?
 
Watanzania tuache kulalama, nauli hata iwe 1000 pouwa mbona kwa siku tuna kunywa pombe na kuhonga wanawake zaid ya 1000.
Hii ni kauli ya kutoka kwa mtu mpumbavu na mjinga na mbaya zaidi hajijui kama yeye ni mjinga na mpumbavu that means ataendelea kuwa mjinga milele.
Unapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwajumlisha kwenye upumbavu wako wa ulevi na na uzinzi. i mean it am not joking!!
 
Ndugu zangu,

Waziri wa Ujenzi amenukuliwa na Watangazaji wa habari akitamka; "Na atakayeshindwa kulipa nauli mpya Dar- Kigamboni na apige mbizi au azunguke Kongowe"- John Magufuli.

Ndugu zangu,
Siamini kama maneno haya yanatoka kwenye kinywa cha Waziri Mwandamizi mwenye dhamana ya kuwatumika WaTanzania. Na kwa vile ni kweli yametamkwa hayo na Magufuli, tena hadharani, basi, nionavyo, John Magufuli ana mawili ya kufanya; ama afute kauli yake hiyo sambamba na kuwaomba radhi WaTanzania hadharani, au apime mwenyewe kama bado anastahili kuongoza Wizara akiwa na dhamana ya kuwatumikia WaTanzania na huku akitegemea atandelea kuheshimiwa na Watanzania ambao kimsingi wamekerwa sana na kauli hiyo yenye dharau na kebehi kwa WaTanzania.

Magufuli huenda amekaa muda mrefu Serikalini kiasi cha kupoteza mguso na hali halisi za Watanzania. Kauli aliyotumia ni kelelezo cha kupoteza mguso huo na hali halis inayowakabili Watanzania walio wengi miongoni mwao ni wakazi wa Kigamboni.

Hivi, Magufuli huyu anaposema atakayeshindwa kulipa nauli mpya apige mbizi au azunguke Kongowe hajui kwamba kuna WaTanzania ambao shilingi mia tatu ni kubwa sana kwao. Kwamba wangekuwa tayari kulipa hiyo nauli lakini ukweli wengi wana hali ngumu kimaisha.

Na je, unafanyaje na Mtanzania anayempeleka mgonjwa wake kwa kutumia kivuko na hana hiyo mia tatu? Naye apige mbizi majini au azunguke kupitia Kongowe kwa miguu, maana hata nauli ya mia tatu ya Daladala hana? Ndio, wazee na wagonjwa nao wapige mbizi majini kwa kukosa nauli ya mia tatu? Na wasiojua kuogelea?

Hapana, inasikitisha. John Magufuli hawezi kujitetea kwa kauli yake hiyo. Aifute na atuombe radhi WaTanzania, basi. Na kimsingi suala hili la nauli za kivuko liangaliwe upya. Tujifunze kutoka kwa jirani zetu wa Kenya. Pale kivuko cha Likoni, Mombasa, ambacho ni sawa na cha Kigamboni, abiria wanavuka bure. Kinachotozwa kodi ya kuvuka ni vyombo vya motot u ikiwamo magari na pikipiki. Hivyo basi, gharama za kuendeshea kivuko zinatokana na kodi za vyombo vya moto.

Na Magufuli atambue kuwa kuna waliomtangulia katika kutoa kauli za ‘ kuchemsha’ na zilizowagharimu kisiasa.
John Malecela ni mmoja wa watu hao. Kuna wakati, akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi. Katikati ya kilio cha watumiaji wa njia ya reli ya kati (TRC) juu ya huduma mbaya za Shirika hilo la Reli miaka ile ya 80, Bw. John Malecela alipata kukaririwa akitamka kuwa hakukuwa na tatizo la huduma mbaya na kwamba wenye kufikiri hivyo, “ They can go to hell!”- kwamba wanaweza kwenda kuzimu.

Katika sanaa ya mawasiliano, tunaamini, kuwa sentesi moja inayotamkwa na mwanasiasa, yaweza kumjenga au kumbomoa kabisa kisiasa. Kwa John Malecela, kauli yake ile ataishi asiiahau, maana, pamoja na kuwa tulikuwa katika mfumo wa chama kimoja, redio moja ya taifa na magazeti matatu, bado wananchi waliweza kufikisha shutuma zao kwa Malecela juu ya kauli yake ile.

Na kilichotokea katika uchaguzi mkuu uliofuata wa mwaka 1985 ilikuwa ni kwa wapiga kura wa Dodoma mjini kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la kisiasa la John Malecela. Walifanya hivyo kwa niaba ya Watanzania wengine na hususan watumiaji wa reli ya kati. Malecela aliangushwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo. Hakupata ubunge na hivyo hakuweza kuwa Waziri.

Tukirudi Kigamboni, hivi, ni kwanini umtoze nauli mkazi wa Kigamboni wakati kila Mtanzania ana haki ya kuishi mahali popote katika nchi hii. Sasa basi, kama mtu na familia yake wameamua kuishi Kigamboni kwanini watozwe nauli kwa kuvuka kwenda na kurudi katikati ya Jiji kwa shughuli zao za kila siku na kama hawatumii vyombo vya moto? Mbona wanaoishi Oysterbay na Masaki akiwamo John Magufuli hawatozwi kodi ya kuvuka daraja la Sarenda?

Tunadhani ni jukumu la Serikali na Wizara ya Magufuli kuhakikisha kunajengwa daraja la Kigamboni kuwasaidia wakazi wa eneo hilo. Kama daraja hakuna ni jukumu la Serikali na wizara ya Magufuli kuhakikisha kunakuwepo na huduma, ikiwezekana ya saa 24 ya kuwavusha watu wa Kigamboni.

Na mpango mpya wa Magufuli wa kuwa na Ferry ya hadi Bagamoyo na Mtoni Kijichi ili kupunguza msongamano wa magari nao haueleweki. Kwenda Bagamoyo na Mtoni Kijichi kwa njia ya maji hakuwezi tena kuwa Ferry kwa maana ya kivuko bali ni usafiri wa majini. Ndicho tunachohitaji kwa sasa wakati kitaalam usafiri huo utakuwa wa gharama kubwa zaidi na vyombo hivyo vya majini itabidi visafiri kwenye kina kirefu cha maji.

Tulidhani kwenda Bagamoyo na Mtoni Kijichi kunahitaji miundo mbinu ya barabara iliyo bora.
Na kuvuka kwenda Kigamboni kwa harakan a ufanisi kunahitaji daraja. Na je, mapato ya kivuko ya kila siku yanatumika vipi? Na tangu yaanze kukusanywa kwanini tumeshindwa kujenga daraja? Au kivuko nacho ni mradi wa wakubwa wa kuzidi kuwanyonya WaTanzania wanyonge?

Hapana, inatosha sasa. Naungana na wakazi wa Kigamboni wakiongozwa na Mbunge wao wa Kigamboni Dr. Faustine Ndungulile wanaopambana sasa kuhakikisha nyongeza hii ya nauli inasitishwa.
Ndio, waacheni Watanzania wa Kigamboni wavuke bure kama hawavuki na vyombo vya moto. Na wana haki pia ya kujengewa daraja. Wakivuka kwa miguu au baiskeli darajani wasitozwe hata senti tano, kama wanaovuka daraja la Sarenda, akina Magufuli na wengine.

Nawasilisha.

Maggid Mjengwa,
Bagamoyo
Januari 2, 2012.
 
Kauli nyingine mara nyingi uwa zinatolewa na Viongozi bila kufikiria madhara yake kabla hawajayatamka. Katika hali ya kuelezea umuhimu wa kitu fulani wakikosa maneno fasaha ya kuelezea umuhimu wa hiko kitu hujikuta wamewatukana wananchi bila wenyewe kujua na nafikiri uwa wanajutia hizo kauli zao baadaye ingawa wanakuwa wagumu kuomba radhi au kukiri hadharani kuwa wamekosea.
 
Kwa kauli hiyo Dr. kajivunjia heshima na amejidhihirisha si kimbilio la wanyonge
mfano mwingine huu hawezekani bajaj walipe pesa nyingi kuliko BMW, Benz, Vx n.k "Hivi ni sawa, Bajaj kulipia Sh 1,800 na Gari ndogo (mfano taxi, benz, BMW, Mark X etc) kulipia sh. 1,500? "
 
Samahani dada, swali lako ni la kipuuzi

TEMESA iko chini yake na kuna jitihada za lazima za yeye kuingilia, kwani jamaa wamepandisha bei ili kufikia lengo la makusanyo badala ya kupunguza kwanza losses na wizi wanaofanya...

KIGAMBONI NEEDS A BRIDGE, NA SIO FAVOR

Kama ungefuatilia vizuri sakata hili, suala la huyu dada usingeliita ni la kipuuzi.
 
Kwa kauli hiyo Dr. kajivunjia heshima na amejidhihirisha si kimbilio la wanyonge
mfano mwingine huu hawezekani bajaj walipe pesa nyingi kuliko BMW, Benz, Vx n.k "Hivi ni sawa, Bajaj kulipia Sh 1,800 na Gari ndogo (mfano taxi, benz, BMW, Mark X etc) kulipia sh. 1,500? "

Hayo ndio maisha bora watanzania walichagua na wakazi wa kigamboni walichagua CCM kwa kishindoooooo
 
......... Kwa vyovyote vile tatizo lillilo dhahiri ni ushirikishwaji wa wadau.......hawakuwashirikisha wadau vya kutosha....ndio sasa unaona 'ubabe' unakuja kwenye utekelezaji.......

Jamani musitupe mapya, hivi tangu lini wadadu wakashirikishwa kwenye upangaji wa nauli? Jee EWURA wanashirikisha wadau wanapopanga bei ya mafuta? TANESCO wanaposhirikisha wadau, na wadau wakakataa jee bei haipandi?

Na hii taarifa si ilitoka kwenye gazeti la serikali? Silaumu raia wa kawaida, lakini hata Mbunge anashindwa kujua matokeo ya kwenye gazeti la serikali wakati yeye ndiye mtunga sheria?

Mimi nakubaliana na wadau wengine wanaoseema sisi tunapenda kulalamika, hivi kweli nauli ya shilingi 200 ambayo imepandishwa baada ya miaka 14 ndiyo issue kubwa hivyo? Na kweli mbona wengine wanalipia huko mikoani, huku Dar wajuaji ni wengi sana na wabishi ndiyo maana kila kitu kinakuwa ni issue.
 
Ndugu zangu,

Waziri wa Ujenzi amenukuliwa na Watangazaji wa habari akitamka; "Na atakayeshindwa kulipa nauli mpya Dar- Kigamboni na apige mbizi au azunguke Kongowe"- John Magufuli.

Ndugu zangu,
Siamini kama maneno haya yanatoka kwenye kinywa cha Waziri Mwandamizi mwenye dhamana ya kuwatumika WaTanzania. Na kwa vile ni kweli yametamkwa hayo na Magufuli, tena hadharani, basi, nionavyo, John Magufuli ana mawili ya kufanya; ama afute kauli yake hiyo sambamba na kuwaomba radhi WaTanzania hadharani, au apime mwenyewe kama bado anastahili kuongoza Wizara akiwa na dhamana ya kuwatumikia WaTanzania na huku akitegemea atandelea kuheshimiwa na Watanzania ambao kimsingi wamekerwa sana na kauli hiyo yenye dharau na kebehi kwa WaTanzania.

Magufuli huenda amekaa muda mrefu Serikalini kiasi cha kupoteza mguso na hali halisi za Watanzania. Kauli aliyotumia ni kelelezo cha kupoteza mguso huo na hali halis inayowakabili Watanzania walio wengi miongoni mwao ni wakazi wa Kigamboni.

Hivi, Magufuli huyu anaposema atakayeshindwa kulipa nauli mpya apige mbizi au azunguke Kongowe hajui kwamba kuna WaTanzania ambao shilingi mia tatu ni kubwa sana kwao. Kwamba wangekuwa tayari kulipa hiyo nauli lakini ukweli wengi wana hali ngumu kimaisha.

Na je, unafanyaje na Mtanzania anayempeleka mgonjwa wake kwa kutumia kivuko na hana hiyo mia tatu? Naye apige mbizi majini au azunguke kupitia Kongowe kwa miguu, maana hata nauli ya mia tatu ya Daladala hana? Ndio, wazee na wagonjwa nao wapige mbizi majini kwa kukosa nauli ya mia tatu? Na wasiojua kuogelea?

Hapana, inasikitisha. John Magufuli hawezi kujitetea kwa kauli yake hiyo. Aifute na atuombe radhi WaTanzania, basi. Na kimsingi suala hili la nauli za kivuko liangaliwe upya. Tujifunze kutoka kwa jirani zetu wa Kenya. Pale kivuko cha Likoni, Mombasa, ambacho ni sawa na cha Kigamboni, abiria wanavuka bure. Kinachotozwa kodi ya kuvuka ni vyombo vya motot u ikiwamo magari na pikipiki. Hivyo basi, gharama za kuendeshea kivuko zinatokana na kodi za vyombo vya moto.

Na Magufuli atambue kuwa kuna waliomtangulia katika kutoa kauli za ' kuchemsha' na zilizowagharimu kisiasa.
John Malecela ni mmoja wa watu hao. Kuna wakati, akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi. Katikati ya kilio cha watumiaji wa njia ya reli ya kati (TRC) juu ya huduma mbaya za Shirika hilo la Reli miaka ile ya 80, Bw. John Malecela alipata kukaririwa akitamka kuwa hakukuwa na tatizo la huduma mbaya na kwamba wenye kufikiri hivyo, " They can go to hell!"- kwamba wanaweza kwenda kuzimu.

Katika sanaa ya mawasiliano, tunaamini, kuwa sentesi moja inayotamkwa na mwanasiasa, yaweza kumjenga au kumbomoa kabisa kisiasa. Kwa John Malecela, kauli yake ile ataishi asiiahau, maana, pamoja na kuwa tulikuwa katika mfumo wa chama kimoja, redio moja ya taifa na magazeti matatu, bado wananchi waliweza kufikisha shutuma zao kwa Malecela juu ya kauli yake ile.

Na kilichotokea katika uchaguzi mkuu uliofuata wa mwaka 1985 ilikuwa ni kwa wapiga kura wa Dodoma mjini kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la kisiasa la John Malecela. Walifanya hivyo kwa niaba ya Watanzania wengine na hususan watumiaji wa reli ya kati. Malecela aliangushwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo. Hakupata ubunge na hivyo hakuweza kuwa Waziri.

Tukirudi Kigamboni, hivi, ni kwanini umtoze nauli mkazi wa Kigamboni wakati kila Mtanzania ana haki ya kuishi mahali popote katika nchi hii.
Sasa basi, kama mtu na familia yake wameamua kuishi Kigamboni kwanini watozwe nauli kwa kuvuka kwenda na kurudi katikati ya Jiji kwa shughuli zao za kila siku na kama hawatumii vyombo vya moto? Mbona wanaoishi Oysterbay na Masaki akiwamo John Magufuli hawatozwi kodi ya kuvuka daraja la Sarenda?

Tunadhani ni jukumu la Serikali na Wizara ya Magufuli kuhakikisha kunajengwa daraja la Kigamboni kuwasaidia wakazi wa eneo hilo. Kama daraja hakuna ni jukumu la Serikali na wizara ya Magufuli kuhakikisha kunakuwepo na huduma, ikiwezekana ya saa 24 ya kuwavusha watu wa Kigamboni.

Na mpango mpya wa Magufuli wa kuwa na Ferry ya hadi Bagamoyo na Mtoni Kijichi ili kupunguza msongamano wa magari nao haueleweki. Kwenda Bagamoyo na Mtoni Kijichi kwa njia ya maji hakuwezi tena kuwa Ferry kwa maana ya kivuko bali ni usafiri wa majini. Ndicho tunachohitaji kwa sasa wakati kitaalam usafiri huo utakuwa wa gharama kubwa zaidi na vyombo hivyo vya majini itabidi visafiri kwenye kina kirefu cha maji.

Tulidhani kwenda Bagamoyo na Mtoni Kijichi kunahitaji miundo mbinu ya barabara iliyo bora.
Na kuvuka kwenda Kigamboni kwa harakan a ufanisi kunahitaji daraja. Na je, mapato ya kivuko ya kila siku yanatumika vipi? Na tangu yaanze kukusanywa kwanini tumeshindwa kujenga daraja? Au kivuko nacho ni mradi wa wakubwa wa kuzidi kuwanyonya WaTanzania wanyonge?

Hapana, inatosha sasa. Naungana na wakazi wa Kigamboni wakiongozwa na Mbunge wao wa Kigamboni Dr. Faustine Ndungulile wanaopambana sasa kuhakikisha nyongeza hii ya nauli inasitishwa.
Ndio, waacheni Watanzania wa Kigamboni wavuke bure kama hawavuki na vyombo vya moto. Na wana haki pia ya kujengewa daraja. Wakivuka kwa miguu au baiskeli darajani wasitozwe hata senti tano, kama wanaovuka daraja la Sarenda, akina Magufuli na wengine.

Nawasilisha.

Maggid Mjengwa,
Bagamoyo
Januari 2, 2012.
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Majid, hakuna kuomba radhi!!! Hawa watu walimzomea. Kama hukumzomea basi wewe hauhusiki na kauli hiyo. Walikosa ustaarabu, kuzomea ni udhalilishaji mkubwa, hakuna anayeweza kuuvumilia. Najua utasema kuwa yeye ni kiongozi, lakini equally, nasema pia na waongozwaji wana wajibu kuwa na heshima na adabu.
 
Nataka kufuatilia ni lini Magufuli amewahi kuwataka radhi watu, au kufuta kauli
 
Hayo ndio maisha bora watanzania walichagua na wakazi wa kigamboni walichagua CCM kwa kishindoooooo

Alafu hapo hapo kuna wajinga wachache wanataka kutuaminishe huyu Dr.Makufuri eti anafaa kuwa mgombea wa urais kama ameamua kuwadharau waTZ waishio kigamboni atawezaje kuwathamini wananchi wa waishio Kisarawe, Namtumbo n.k?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom