Mkuu wewe ndio umetuleta kwenye somo lenyewe.. big up.
Naamini kuna watanzania wengi sana wamesha pigwa na natabiri atafuta matangazo yake na kutokomea kusiko julikana.
Cha kushangaza, wizara husika zinawaachaje watu kama hawa wanafanya utapeli kwa leseni za serikali?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Wizara utakuta hazina hata taarifa, istoshe hapo inavyoonekana sio utapeli wa moja kwa moja, kwamba unampa tu hela kisha anakimbia, hapana... Huo ni utapeli wa kitaalamu, kuna mikataba utasainishwa wakati wa kuinvest hiyo 150k yako.
Sasa kwenye ile mikataba kutakua na vipengele vitamlinda sana yeye Mr. Kuku, na wewe mbongo kwakua akili yako yote ilikua ikiwaza kuvuna mil 8 basi hata hautajishughulisha kuusoma mkataba kwa kuuelewa, utasoma ili umalize kusoma tu.
Mfano kwenye mkataba kunaweza kua na kipengele kinachosema... "Endapo mradi ukapata hasara nakupelekea investor kushindwa kulipwa return yake, basi investor atarudishiwa return yake ndani ya miaka 5 ijayo baada ya tarehe husika ya return". Mzee baba hapo itakuta mkataba upo kwa lugha ya malikia basi mbongo unajikuna unaambukia this is na that [emoji3]..
Kimbembe kitakuja siku ambayo unatakiwa kupata return yako.. Kwanza watakaa kimya tu, utapowakumbusha hapo ndipo zitapokusa sababu za hapa na pale... Mfano unaweza kuambiwa "Kuku waliugua ugonjwa wa gafra na kupelekea kufa hivyo mradi uliingia kwenye hasara, investor wote wamepata hasara kwaiyo return yako tunatarajia kuirudisha baada ya miezi 6 mingine kwenye mradi ujao" hapo ndio bye bye hio mkuu..
Ukianza kulalamika utaambiwa nenda mahakamani [emoji3]... (Hapo umesha sahau kama ulisign mkataba, na huo mkataba hukuusoma na kuuelewa wote).. Hapo hesabu ushapigwa tayari.
Nakumbuka mwaka jana kuna jamaa alitapeli sana watu huko instagram... Watu walinyooshwa sana, alikua anajiita "PIKIPIKI MTUMBA" [emoji16]... Alikua anapost zile bikes kali kali za dede, kama honda, enduro, ktm kuanzia cc 250 hadi zingine za cc 1000 kwa bei sawa na bure. Utakuta honda ya cc 450 anauza kwa 2.5 milioni. Kumbe jamaa alikua na strategy pendwa kwamba "Tunatuma jadi mkoani, kwa uaminifu mkubwa"
Basi baada ya kuvutiwa na bei zake nikasema hebu ngoja nimuibukie whatsap (maana alishaweka namba kwa BIO pale juu )... Basi nikaeleza shida yangu pale, kwawamba nimeipenda pikipiki fulani bei yake ikoje? Nikatajiwa mil 3, nikamwambia mimi nina mil 1.8, naomba unisaidie kaka... Akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akajibu sawa lete hiyo. Nikamuuliza utaratibu ukoje?... Hapa ndipo aliponihakikishia kwamba yeye tapeli though nilishaana kuhisi harufu ya utapeli kabla [emoji3].
Jamaa akanambia "tuma hiyo pesa kwa namba hii kisha mzigo wako utatumwa na ndani ya siku 2 itakufikia popote ulipo"[emoji16] Yaani biashara ya mamilioni ifanyike kama biashara ya nyanya geengeni? Na hapo hapohajui hata nipo mkoa gani... Nikastaajabu! Nikamwambia bro kwani ofisi / store yenu iko wapi? Akasema tupo Arusha, nkamwqmbia sio kesi mimi nipo dar naomba namba yako ya simu kisha nipe location ntakuja hadi hapo store kwenu. Baada yakumwambia hivyo hakujibu tena txt na akanibloku kabisa. Ikabidi jicheke tu [emoji16].
Nikarudi kwenye page yake nika comment aache utapeli afanye kazi, alafu nikamwambia kajifunze mbinu za kitapeli sio hii, hii itakukamatisha fasta... Ndani ya dakika tu comment ikafutwa nikalambwa na block kabisa [emoji3].
Sema jamaa alipiga dana hela yule maana nilkua naona malalamiko kwa watu, kwamba "mimi numeagiza helment ila week ya pili hii sijapata"! Comment ukirudi baada ya muda unakuta imefutwa, Pia jamaa alikua anaushamba kidogo na mtandao wa instagram maana hata comment alikua anaachia tu.. Angejua ku ingore comment kwma Mr.kuku angepigahela nyingi sana. Sasaivi ile page siioni kabisa, sijui imefutwa au amebadili jina..
TUWENI MAKINI MAZEE
Sent from my iPhone using JamiiForums