Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?

Hahaha calm down..hiyo pesa ameiwekeza muda mrefu alianza na 7millon akawanairudisha mdogo mdogo.kwenye biashara(reinvestment in the project).mpaka..ikakua hadi 52 million.

Watu ambao sana comment negatively ni kwa sababu ya kutokua na uelewewa..na concept mpya ya crowd farming.

Crowd farming ni kuanzisha kilimo aidha cha matunda au ufugaji wa kuku au ngombe nk.lakini kwa kushirikisha wadau wa kawaida kama Mimi na wew ambao hatuna muda wa kusimamia ufugaji na pia uwezo binafsi wa kipesa ni mdogo kuanzisha biashara ya ufugaji.

According to google:Crowd farming is a model where a number of investors share risks and own shares in a farming venture.
The origins of the "crowd" concept can be traced to crowd sourcing where a large number of people are invited to participate in a project.

Aina hii ya kilimo...imeshika kasi sana Nigeria...
Huku Nigeria inaitwa crowd farming au online farming...(najua hili neno watu hawapendi kulisikia kilimo cha mtandao).Lakini ukijifunza kufatilia vitu kwa undani sidhani kama utakua ni mtu wa kupelekwa na mawambi ya watu..

Kuna makampuni mengi sana ambayo yanatumia huu mfumo.huko Nigeria na south Africa.Na pia hii concept bado ni ngeni sana kwahiyo watu wanakua negative kisa tu ni kitu kigeni...

Nimefatilia makampuni Mengi ambayo yanatumia mfumo huu.Na faida kwa wawekezaji ni kuanzia 10%-50%.
Baadhi ya makampuni ni yafutayo..(Nigeria)

1.thriveagric.com
2.farmcrowdy.com
3.farmkart.ng
4.porkmoney.com
5.efarms.com.ng/end
6.payfarmer.com
7.agropartnerships.co
8.tradersofafrica.com
9.farmfunded.com
10.ez-farming.com
11.menorahfarms.com
12.farmagric.com
13.farmbuddy.ng
14.groupfarma.com.ng
15.greenfoldfarmprojects.com
16.smartfarm.com.ng
investment cycles kwa nyingi naona ni kuanzia miezi 4 hadi 12.

Anyway nirudi kwa Mr Kuku anatumia the same mode of operation yaani crowd farming...investment cycle yake ni miezi 4 hadi 6.Na pia soko LA uhakika analo..(contract farming)unaingia mikataba awali ya kusupply kuku constantly kwa muda maluum ili mwishoni mwa huu muda ndo ulipwe malipo.(Hii Ina maana unahitaji capital kubwa sana ya kuweza kuendesha mradi bila kuaffect supply ya kuku.Meaning investors au crowd farmers that's where they come in)

Simple facts mt kuku farms
Ana kuku 90,000+
Ana chinja 3000+ every week

Kuhusu masoko ngoja nikupe scenario...
Acacia/barrick wanaotumia 2500-3000 chickens per week
American embassy/washirika 1000+ chickens per month
Geita gold mine wanahitaji 3000 chickens per week
Bado hizi hotel kubwa,na masupplier wadogo.. Wanaopelekea masokoni etc.


Advantages ziko hivi..
Mfano Mimi nimeajiriwa natoka kazini SAA mbili usiku nafanya kazi hadi jumapili.Muda wa kuanzisha na kusimamia mradi sina.Na hata ulisema mkopeshe MTU pesa mtaishia kugombana...

Kwahiyo pesa zangu ambazo nimesave naziwekeza huku kama investor.nakua kama vile nimenunua shares ambazo zitamature ndani ya muda Fulani.Kwahiyo nakua ufugaji unafanywa wa kuku unafanywa kwa niaba yangu.

Ni kama kununua shares kwenye kampuni LA cocacola au vodacom..wakutumia pesa yako kuendesha biashara mwishoni mwa muda Fulani aidha mwaka miezi sita au Tisa ukalipwa profits in form of dividends...

Mimi binafsi na kusanya pesa zangu naenda kuziweka huko...
By the way kama kuna mtu amesikia kuna crowd farming nyingine mbali na Mr kuku...please anijulishe....

Risks
Ofcoz just like any other business.. Kuna risks za kuconsider kabla hujaweka pesa yako huku kwenye hii miradi...Its your job to determine whether you can accept the risks or not.Kitalaam inaitwa Risk appetite. Is your risk appetite high or low..mfano Mimi am willing to risk 5 million..mwingine na risk 7million etc.

i Mr kuku farms hii concept yeye ndo kaintroduce Tanzania kwasasa hivi bado hajapata competition yoyote....naona kuna huyu jamaa mwingine anaitwa Weku enterprises....

Mwaka juzi kama sikosei kuna Tender mmoja ilitangazwa na US embassy au International school of Tanganyika walikua wanataka supplier mkubwa wa kuku at least 1000 per month na hawataki excuses...sio unaanza mwezi huu mara mwezi ujao una anza kuleta sababu mara sijui mtaji umekata nk.

Kwa kutumia crowd farming Mr kuku anaweza supply US embassy...

Pia kuna huyu jamaa wa south Africa anasema unanunua ngombe...na kumuhudumia mpaka anakua hadi kummuuza for a profit...livestock wealth.com

Kwahiyo jamani ndugu zangu tusipende kuhukumu vitu bila kufanya research...Tusipende kujibu kwa mihemko kwasabab tu uliwahi poteza fedha zako sijui ukaliwa pesa zako...



TUJIFUNZE KUSOMA NA KUFATILIA VITU KIUNDANI KABLA HATUJA KATISHA TAMAA WATU.TUKIENDELEA HIVI KILA SIKU TUTABAKI NYUMA SIKU ZOTE.






Sent using Jamii Forums mobile app
Crowd farming imejuaje mkuu
 
Kwanza kulikuwa hakuna haja ya huu uzi kwa sababu umeshatoa hukumu tayari kwenye kichwa cha uzi ila unatafuta watu wa kuja kujumuika nao muwakatishe tamaa wengine.

Pili wewe sio muwekezaji unapendeza zaidi ukiwa umeajiriwa kwa sababu unaonekana una woga mwingi kupita kiasi kitu ambacho hakitakiwa katika uwekezaji.

Mkiletewa fursa za kilimo mnasema hakuna uhalisia ni kilimo cha instagram, ufugaji nao hamuutaki, biashara mnaleta vitisho kwamba hakuna mzunguko wa hela, mkiletewa fursa za mitandaoni mara kina ontario.

Sent using Jamii Forums mobile app



Mkuu uliwekeza kiasi gani?
 
Haya sasa, wale watu waliowakandia wenzao wanaogopa uwekezaji, wao wanaendeleaje huko walipo?
Mkuu, clip jamaa anawavuta kawekeza 7mil kavuna 52Mil kimasihara...
Nilicheka sana!

Aisee, tusubirie serikali ije ivunje kibubu na kuzibeba kama zile hela za DECI..

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
Kwanza kulikuwa hakuna haja ya huu uzi kwa sababu umeshatoa hukumu tayari kwenye kichwa cha uzi ila unatafuta watu wa kuja kujumuika nao muwakatishe tamaa wengine.

Pili wewe sio muwekezaji unapendeza zaidi ukiwa umeajiriwa kwa sababu unaonekana una woga mwingi kupita kiasi kitu ambacho hakitakiwa katika uwekezaji.

Mkiletewa fursa za kilimo mnasema hakuna uhalisia ni kilimo cha instagram, ufugaji nao hamuutaki, biashara mnaleta vitisho kwamba hakuna mzunguko wa hela, mkiletewa fursa za mitandaoni mara kina ontario.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole mkuu kwa kupigwa pesa. Jamaa kakamatwa tayar uliekua unamtetea
 
Aisee dada Tabutupu kwanza nikupongeze kwa kuwa na tahadhari, kutaka ushauri kabla yakuingia..

Binafsi nimekutana nayo sana matangazo yao wanayorusha kwenye sponsored huyo anaejiita Mr.kuku, kwa mara ya kwanza nilipokutana nalo tangazo lake, nilifanya kauchunguzi kidogo maana nina kauzoefu kidogo kwenye hizi biashara za mitandaoni..

Kwa huyo Mr.kuku ni tapeli kama matapeli wengine, narudia tena hapo kuna utapeli! Tujiulize haya maswali:-

• Ikiwa mtu umeweza kuwekeza kwenye ujenzi wa mabanda makubwa ya kuku, sidhani kama utaweza, wala kuwa na muda wakutumia nguvu kushawishi watu wawekeze 150K ili wavune faida . Hii ni ishara ya kwanza yakupigwa.

• Katika post zake nyingi huyu jamaa huwa ana ignore / zuia sehemu ya comment, yaani akipost basi anaondoa ile sehemu ya comment. Hii maana yake hapo kuna watu walishapigwa, kwaiyo anaondoa sehemu ya comment ili wale waliopigwa wasije ku comment shutuma zake nakusababisha ambao hawajui wakajua ukweli ulivyo nakupelekea kukosa wateja wapya. Kwaiyo hapo anafuta comment ili tu ambao hawajui wasijekupata info za utapeli nakuwaogopesha kuingia.

Pia kwenye kutoa ushuhuda hapo usitilie maanani sana, anaweza hata kula njama na watu akawalipa 20k akawapanga namna ya kuongea, akawarekodi kisha mnapostiwa pale instagram, Na vile wabonho wanavyopenda mtelezo na short cuit basi anaweza kutuma hela hata kwa Mpesa kwa sababu yupo mkoani kisha aje kuvuna mil 8 (hahahaaa, wabongo baana )

Hebu jiulize kwanza, hivi yeye Mr.kuku haitaki hiyo mil 8? Ikiwa anatumia nguvu kubwa kwa kuitaka 150K yako vipi mil 8? My guy think twise..

Sent from my iPhone using JamiiForums
Yaani mimi nikifanya biashara na mtu kisha akanipa namba naangalia whatsapp kama kaset usione last seen au usiione read receipt aisee sifanyi naye biashara au kama nikifanya nae yaani ni ile ngwadu kwa ngwadu jicho kwa jicho hatua kwa hatua yaani simuachii space.

Issue za kupanga watu kwa kuwalipa ishafanywa sana na wachungaji,kuwapanga watu kwamba wagonjwa wanaenda kuombewa kisha wanatoa ushuhuda kama wamepona ,kumbuka kuna dada alikamatwa kwamba freemanson imemtoa akaonyesha magari na nyumba kapata kwa ajili ya freemanson kumbe alilipwa elfu 30 tu kufanya ile clip.

Na kweli ukiona mtu kapost kitu halafu kahide watu wasicomment kama ni biashara hapo stuka,maana comment ndio inatoa ushuhuda halisi hata ukipanga watu w kukusifia lazima watajitokeza watu ambao wataongea ukweli sasa ukiona mtu anaficha comment jua ni tapeli,watu ambao sio matapeli hawawezi kufanya hivyo ndio maana haujawahi kuona voda au tigo wanatangaza bando zao kisha wakaficha watu wasicomment.
 
Kuna jamaa wanaitwa Mr Kuku Farms, wanasema wanafanya ufugaji wa kuku na wanahkmiza watu kuwekeza kwa ahadi kwamba unavuna mara 2.

Nimeona wamepost na shuhuda mbalimbali motomoto kama zile za kwa mwamposa. Mmoja anasema aliwekeza sh laki 3.5 na anategemea kuvuna 8M.

Swali nalo jiuliza kwanini iwe rahisi kupata fedha kiasi hiki kwa muda mfupi kuliko bank yeyote au soko la hisa?

Napata wasiwasi isije kuwa ni DESI imerudi kiani maana huwezi pata mara 2 kirahisi hivi wakati kuna makampuni yanafuga kuku nanyanapata hasara.

Naomba kwa yeyote anaye jua hawa Mr kukus ni wafugaji kweli wa kuku?

Je, kama kuna mtu amesha fanya nao uwekezaji , atupe ushuhuda wake motomoto?

Je, kwanini kama ni biashara ya uwekezaji wasifanyie soko la hisa DSE?

Serikali ipo wapi kutoa ufafanuzi wa jambo hili walau watu tufuse million kwa myda mfupi.

Kwa wale ambao mnataka kuona shuhuda motomoto tembelea instagram Mr_kukus

Nataka nijitose kwa kuwekeza mil 2 ili zikisha komaa nihune kama mil 80 ndani ya miaka 2.

Sent using Jamii Forums mobile app


UPDATES 10 August 2020

Mfanyabiashara Tariq Machibya maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za umma zaidi ya Shilingi 17 bilioni. https://t.co/9Ik6wUGj55
Ahh vitu vingi .....Ishakwisha hiyoooo!!!
 
Kwa mtu aliyefanya biashara ya kuku wa kisasa..anajua Mr kuku yupo sahihi...mbona wanafanya wengi huu utaratibu yeye tu kajitangaza lakini
 
Back
Top Bottom