Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Kama ni za EPA ambazo zasemekana Zimeibiwa au Kuhujumiwa kwa kuundiwa makampuni ya mifukoni, je ni hatua gani za kisheria zitafuata?
Mchungaji, yaani hatua za kisheria zifuate baada ya makosa kusahihishwa? Hivi tunajua kuwa makosa yamefanyika na yana ushahidi kuwa yamefanyika? Kwanini mkondo wa sheria usianze kwanza? Mimi naona wamejaribu kuweka mkokoteni mbele halafu farasi nyuma! sasa yupi anamvuta yupi..
izi za CIS, mikopo inarudishwa baada ya zaidi ya miaka 10. Je wakopaji hawa wataruhusiwa kukopa tena? Je BOT na Hazina zitahakikisha vipi kuwa hawa default borrowers do not receive a positive credit rating for future loans from any financial institution? who will give them a guarantee?
Kama hawa watu walikopa, terms and conditions zilikuwa vipi? Maana kuwataka warudishe mikopo kama muda wake haujaisha inaweza kuingilia biashara za watu. Kama walitakiwa kuwa wamekwishalipa hadi hivi sasa ni jitihada gani zilifanyika kuwadai? Kama DAWASA waliweza kulikatia jeshi maji kwa kisingizio cha kudai deni, leo kwanini wanashindwa kuwakatia mitaji hawa wote?
Hata hivyo katika hayo mawili ni upande mmoja tu umeonesha kuna uhalifu umefanyika; uhalifu ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano anajua umefanyika lakini ameamua kukwepa kuushughulikia na badala yake anatumia njia ya kidiplomasia.
Hivi kama kutokana na fedha za EPA nilifanikiwa kujenga nyumba za kupanga ishirini. Kamati ya Rais inapokuja na kuzungumza nami nakubaliana nao na kuwaambia kuwa basi nitaresha 10 kati ya hizo kwa moyo mnyofu na kuonesha uzalendo. Wale watu wa Kamati wakawatangazia wananchi kuwa "mmoja wa wahusika arejesha nyumba zilizotokana na akaunti ya EPA" itakuwa imesema uongo?
Sasa hawa wanarudisha fedha na mali sawa; zote? na wanapimaje...