Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
Hivi sasa ndiyo kwanza nimemaliza kusikiliza tarifa muhimu kwamba ile Tume ya Rais ya EPA ya kuchunguza ubadhirifu wa fedha za malipo ya akaunti ya madeni ya nje pale BoT imeeleza kuwa imefikia mahali pazuri kutoa taarifa yake.
Tume hiyo katika taarifa yake imesema imeweza kusaidia kurejeshwa kwa kiasi kikubwa cha fedha zilizolipwa kitapeli kwa kampuni za kisanii.
Imesema kuwa mali zisizohamishika zimekamatwa maeneo mengi ya Dar na miji mingine, kuhusu mali zilizo ne ya Tanzania, tume hiyo imesema kuwa nazo zitapatikana karibuni kabla ya kukabidhi ripoti kamili kwa Rais Jakaya Kikwete..
Mwenyekiti amesema wananchi wote wanaombwa kutoa taarifa kwa tume hiyo kwa kutumia namba za simu zifuatazo
+255 784 994881
+255 784 231928
+255 784 785742
Haya jamani mambo yetu yale, kama mnafahamu mali za mafisadi wale wa BoT semeni ili turejeshe serikalini na ziuzwe kama hazihamishiki ili pesa zinazopatikana zikajenge barabara, kununua dawa, kuboresha elimu na dawa hospitalini.
Nawatakieni kila jema.