MPOKI wa orijino komedi na misemo ya ajabu

Kuku kuku jogoo jina
Mkuki haupigwi konzi
Mwili si hoja kikubwa virutubisho
Choo cha treni hakina chemba
Ndimu changa haina maji
 
Kuku kuku jogoo jina
Mkuki haupigwi konzi
Mwili si hoja kikubwa virutubisho
Choo cha treni hakina chemba
Ndimu changa haina maji
Mpoki kichwa bana! Mnakumbuka enzi za mambo hayo Mpoki alivyoigiza hana mikono alafu akawa anamtongoza demu huku joti amejificha nyuma yake akawa anatongoza alafu joti anatumia mikono yake kufatilizia maneno ya Mpoki ili demu asijue Mpoki hana mikono! joti alikuwa anafatilizia maneno ya Mpoki bila kukosea! Binafsi ni komedi iliyowahi kunichekesha mno na huwa naomba wairudie siku moja!
 
Mbona sijaona msemo wowote wa kusisimua hapo. Isitoshe hii misemo hajatunga yeye na badala yake huwa anakopi tu kutoka kwa Gea Habib yule wa kipindi cha ''Kwa Raha Zako'' cha Clouds Fm.

Kwa hiyo huyo unaemsema wewe ndio mtunzi wa hiyo misemo?
 
Mpoki kichwa bana! Mnakumbuka enzi za mambo hayo Mpoki alivyoigiza hana mikono alafu akawa anamtongoza demu huku joti amejificha nyuma yake akawa anatongoza alafu joti anatumia mikono yake kufatilizia maneno ya Mpoki ili demu asijue Mpoki hana mikono! joti alikuwa anafatilizia maneno ya Mpoki bila kukosea! Binafsi ni komedi iliyowahi kunichekesha mno na huwa naomba wairudie siku moja!

kamanda naikumbuka hiyo imetulia sana
 
Mhogo mchungu ndiyo baba lao anawapita wote akina Mpoki, Gea Habibu, Bonge na hata Mrisho Mpoto. Bahati mbaya yake ni kwamba yeye siyo muuza sura kama hao hapo
 
Mpoki yupo juu sana huyu ana kipaji sana,akimuigiza cpt.john komba au prof. Lipumba hahaaaaa ni balaaaaaa
 
mbona sijaona msemo wowote wa kusisimua hapo. Isitoshe hii misemo hajatunga yeye na badala yake huwa anakopi tu kutoka kwa gea habib yule wa kipindi cha ''kwa raha zako'' cha clouds fm.

kaaaazi kweli kweli.... Watu bana mh!
 
Mhogo mchungu ndiyo baba lao anawapita wote akina Mpoki, Gea Habibu, Bonge na hata Mrisho Mpoto. Bahati mbaya yake ni kwamba yeye siyo muuza sura kama hao hapo

yeye ni mtu wa methali na sio mineno ya shombo kama mpoki..
 
Mbona sijaona msemo wowote wa kusisimua hapo. Isitoshe hii misemo hajatunga yeye na badala yake huwa anakopi tu kutoka kwa Gea Habib yule wa kipindi cha ''Kwa Raha Zako'' cha Clouds Fm.

we nae kwenye sifa sifia khaa, mbona chuki live live hivo ehhhh
 
hii misemo hata kama hajaianzisha mpoki ila kwajinsi mpoki anavyoitoaga inachekesha kwani huitoa katika maongezi ambayo hutarajii kama atatoa huo msemo!.....
 
Wakubwa kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine tume kuwa tukifuatilia vipindi vya original komedi nadhani mtakubaliana nami kwamba huyu sylvester mjuni aka MPOKI amekuwa na misemo ya ajabu ambayo nashindwa kuelewa kwamba amesomea au kipaji binafsi tu.Baadhi ya misemo yake ni kama
1.nyoka hana kiuno ndo maana havai shanga
2kukaa karibu na godauni si kupata kazi
3.usimsifu babako kwamba anajua kukimbia bali msifu na baba wa mwenzio aliyemkimbizia baba yako
4kukaa karibu na shule sio kujua kusoma
5kukaa karibu na mahakama sio kujua sheria
6kama akili ni nywele basi watu wasingenyoa siku ya mtihani na mengine mingi

wakubwa naomba kutoa hoja

ngoja niongeze
leo ndo utajua kwamba redio call haiwekwi vocha
utanieleza kwa nini bata anaharisha maisha yake yote
 
mpoki yuko vizuri pia,jaman mnasubili hadi afe ndo mwanze kumsifia.... anasema eti kama unaona maisha magumu kafanye kaz nyingne
 
Back
Top Bottom