Mpinzani wa Obama nae aficha fedha zake Uswiss

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Wanabodi na Moderators heshima mbele,
Wakati harakati za uchaguzi Mkuu nchini marekani zikiendelea, Mpinzani mkubwa wa Barack Obama, Bwana Mitt Romny anakabiliwa na tuhuma nzito kama tuhuma zinazowakabili baadhi ya Viongozi waandamizi wa CCM za kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha nchini Uswiss. Pia anatuhumiwa kumiliki vituo vya mafuta ambavyo amevipata kwa njia ya mashaka.

Taarifa hizi zimebandikwa kwenye website ya
Barack Obama inayoratibu kampeni nchini humo hivi sasa. Baadhi ya tuhuma anazokabiliwa nazo ni kama ifuatavyo:-

It's a pattern of secrecy, and this is just the latest example of him trying to hide the truth from voters. There are a number of issues in play right now -- and voters deserve answers:

1) Mitt Romney refuses to release multiple years of taxes, ignoring decades of precedent.

2) He won't disclose his "bundlers," the people raising millions for his campaign.

3) He is the sole owner of a questionable shell corporation in Bermuda.

4) Until recently, Romney kept cash in a Swiss bank account.

5) According to the Globe, he hasn't been honest about when he was running Bain Capital, even though legal documents refute his claims.

Stephanie Cutter
Deputy Campaign Manager
Obama for America

Kwa tuhuma hizi ni wazi kabisa chama cha Republican cha Bwana Romney hakina tofauti na Chama cheti kinachotawala, CCM kwa sababu wanachama wao wana hulka zinazofanana.

Source:-

[SUP]1 [/SUP]Barack Obama

[SUP]2[/SUP] Barack Obama

TUMBIRI (PhD, HULL Univeristy - HULL City),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Ana akiba ya USD 200,000,000 mali yake yeye mwenyewe kwa mujibu wa BBC jana
 
Duh!kumbe mlikuwa hamjapata taarifa?hili ni mojawapo ya mambo yatakayo mcost Romney,yote wanasema kwanini azifiche huko uswisi?watu wa Obama wame capitalize kwenye hilo kwasababu wenye kuweka fedha huko wanajulikana ni some dirty hands na corrupt figures ie madikteta na matajiri wakwepa kodi.
 
Hahaaaaa kwanza mwandishi mwenyewe ni Stephanie Cutter...former campaign spokeswoman wa the haughty John Kerry.

Hiyo bi dada hana credibility yoyote.

Halafu, kila kitu walichomrushia Romney hakuna hata kimoja kilicho stick

Majuzi hapa walitaka kumlink na yule senatorial candidate wa Missouri lakini sasa hiyo habari ishakuwa history na kwa mujibu wa poll moja niliyoiona jana inasema kuwa asilimia 77 ya wana Missouri wameshamsamehe huyo jamaa.

Team Obama wapo kwenye panic mode. Hawataki kabisa kudebate mambo ya uchumi. Wako radhi wamshikie bango Romney kuhusu pesa zake na distractions nyingine kama huyo Akin.

Democrats wameshikwa pabaya.

They gonna put y'all back in chains.

NB: Halafu Romney hajaficha pesa zake huko kwa sababu hakuna kilicho unlawful alichokifanya. Na pia sio unlawful kuwa na Swiss accounts. So what's the big deal?
 
Romney kwa hili kashikwa vibaya na hawezi kutoka.

Utasema nani kasema au kaandika ila wengi wanalijadili hili.

Angalia hii Video na yenyewe nafikiri itakuwa imeandaliwa na Obama team.

Bashir: What Mitt Romney

Bwa ha ha ha....Martin Bashir ni commentator wa MESSNBC ambao ni propaganda wing ya team Obama.

Hiyo stesheni inashika namba za mwisho mwisho katika tv ratings. Maana yake ni watu wachache sana wanaoitazama.

Zaidi ya hao kina Bashir, Rachel Maddow, Chris Matthew na Al Sharpton....kwa wengine limeshakuwa a thing of the past.

Hata mainstream media ya Marekani kwa ujumla wake hawaizungumzii tena.

This year's main election issue is the economy and not Mitt Romney's tax returns.
 
Sister Kaunga, huyu Mami Ng'wana Ngabu anatuangusha wakati mwingine.

Ila sitashangaa kama atakuwa ni MNYANTUNZU maana Wanyantuzu (Bariadi, Shinyanga) huwa wakorofi kiaina.

Wanapenda kujifanya SAMAKI kwa sana kwa kwenda kinyume na mkondo wa maji :)

Yaani kaka kama ulikuwa kwenye kichwa changu, the moment i saw the title nikamfikiria Nyani Ngabu.
 
Last edited by a moderator:
Sister Kaunga, huyu Mami Ng'wana Ngabu anatuangusha wakati mwingine.

Ila sitashangaa kama atakuwa ni MNYANTUNZU maana Wanyantuzu (Bariadi, Shinyanga) huwa wakorofi kiaina.

Wanapenda kujifanya SAMAKI kwa sana kwa kwenda kinyume na mkondo wa maji :)

Nyinyi mnamuunga mkono Obama kwa sababu baba yake ni mweusi.
 
Pamoja na kwamba mimi siyo mshabiki wa Romney lakini inabidi tuelimishane kidogo.

Kuna tofauti kubwa kati ya jinsi Romney anavyoshutumiwa kuficha pesa Uswisi na jinsi viongozi wetu wanavyoshutumiwa.

Romney anashutumiwa kukwepa kodi kwa sababu ukiwa na offshore account huzilipii pesa kodi kama ambavyo pesa hizo zingekuwa bank ya Marekani. Kosa hapa ni kukwepa kodi.

Viongozi wetu wanashutumiwa kuiba pesa za umma na kuzificha Uswisi. Hapa kuna makosa mawili, wizi na kukwepa kodi, lakini kosa kubwa zaidi ni wizi.

Oneni tofauti kati ya pesa za wizi na pesa zilizochumwa kihalali.

Ifahamike kuwa kukwepa kodi kuko kwa aina nyingi na kwingine kunakubalika kisheria. Hakuna wizi unaokubalika kisheria.
 
Ok, Bloomberg nayo ni watu gani?

[h=1]Romney Tax Returns Show Strategy For Moving Money To Kids[/h]Republican presidential candidate Mitt Romney and his wife, Ann, have used sophisticated estate- planning techniques for more than a decade to minimize taxes and amass at least $100 million for their family outside of their estate.......

Romney Tax Returns Show Strategy for Moving Money to Kids - Bloomberg
Bwa ha ha ha....Martin Bashir ni commentator wa MESSNBC ambao ni propaganda wing ya team Obama.

Hiyo stesheni inashika namba za mwisho mwisho katika tv ratings. Maana yake ni watu wachache sana wanaoitazama.

Zaidi ya hao kina Bashir, Rachel Maddow, Chris Matthew na Al Sharpton....kwa wengine limeshakuwa a thing of the past.

Hata mainstream media ya Marekani kwa ujumla wake hawaizungumzii tena.

This year's main election issue is the economy and not Mitt Romney's tax returns.
 
Njomba hilo tunalijua. Ndiyo maana Denmark hadi leo wanashauriana na Wazee wa MELI KUBWA za mizigo duniani MAERSK & LLOYD kuwa mwaka huu alipe kodi kiasi gani. Wanaogopa kuwa wakiwaudhi, watahamishia HQ yao huko North au South Pole na ikibidi hata mwezini ambako hawatalipa kodi. Hapo bado hujagusa visiwa vya watunza hela Chafu.

Sasa wewe unataka kuwa Rais wa Marekani na pesa zako zipo jengo moja na Mafia wa Columbia, CCM Team, Moboutou family, Bongo Family, Russian Mafia, na wachafu wengine wengi? Pia unajua kuwa kupeleka kazi na pesa nje, unaliuwa taifa lako mwenyewe.

Angalia walivyomwijia juu jamaa wa POLO kwa kushonea suti za OLYMPIC huko China kwa team ya USA.
Pamoja na kwamba mimi siyo mshabiki wa Romney lakini inabidi tuelimishane kidogo.

Kuna tofauti kubwa kati ya jinsi Romney anavyoshutumiwa kuficha pesa Uswisi na jinsi viongozi wetu wanavyoshutumiwa.

Romney anashutumiwa kukwepa kodi kwa sababu ukiwa na offshore account huzilipii pesa kodi kama ambavyo pesa hizo zingekuwa bank ya Marekani. Kosa hapa ni kukwepa kodi.

Viongozi wetu wanashutumiwa kuiba pesa za umma na kuzificha Uswisi. Hapa kuna makosa mawili, wizi na kukwepa kodi, lakini kosa kubwa zaidi ni wizi.

Oneni tofauti kati ya pesa za wizi na pesa zilizochumwa kihalali.

Ifahamike kuwa kukwepa kodi kuko kwa aina nyingi na kwingine kunakubalika kisheria. Hakuna wizi unaokubalika kisheria.
 
Bwa ha ha ha....Martin Bashir ni commentator wa MESSNBC ambao ni propaganda wing ya team Obama.

Hiyo stesheni inashika namba za mwisho mwisho katika tv ratings. Maana yake ni watu wachache sana wanaoitazama.

Zaidi ya hao kina Bashir, Rachel Maddow, Chris Matthew na Al Sharpton....kwa wengine limeshakuwa a thing of the past.

Hata mainstream media ya Marekani kwa ujumla wake hawaizungumzii tena.

This year's main election issue is the economy and not Mitt Romney's tax returns.

Hata Morning Joe sio mainstream?
 
Hahahaaa, Mami kwa hili la Bloomberg mtu hatoki. Haya sema ni MEDIA gani unaiamini nikuletee habari hii kutoka kwao.

Kwanza haeleweki, tells all. Weekeend Mami imekolea, ngoja niwahi Visungura uchochorni :)

Usiku ni mwendo wa Nyama Choma. Wanyaturu wanaimba "Pembi mora tumle Sungura, pembi mora tumle Wamanyanga".
Bloomberg siyo solid conservative huyo. Kwanza haeleweki.
 
Wanabodi na Moderators heshima mbele,
Wakati harakati za uchaguzi Mkuu nchini marekani zikiendelea, Mpinzani mkubwa wa Barack Obama, Bwana Mitt Romny anakabiliwa na tuhuma nzito kama tuhuma zinazowakabili baadhi ya Viongozi waandamizi wa CCM za kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha nchini Uswiss. Pia anatuhumiwa kumiliki vituo vya mafuta ambavyo amevipata kwa njia ya mashaka.

Taarifa hizi zimebandikwa kwenye website ya
Barack Obama inayoratibu kampeni nchini humo hivi sasa. Baadhi ya tuhuma anazokabiliwa nazo ni kama ifuatavyo:-

Kwa tuhuma hizi ni wazi kabisa chama cha Republican cha Bwana Romney hakina tofauti na Chama cheti kinachotawala, CCM kwa sababu wanachama wao wana hulka zinazofanana.

Source:-

[SUP]1 [/SUP]Barack Obama

[SUP]2[/SUP] Barack Obama

TUMBIRI (PhD, HULL Univeristy - HULL City),
tumbiri@jamiiforums.com

Obama naye ni mchovu vile vile si Romney peke yake. Ukiangalia uraisi wa Obama utaona kwamba ameikanya kanyaga ile katiba ya Marekani. Kafanya mengi tuu ambayo amekiuka katiba ya Marekani. Ameivamia Libya bila ya bunge kuhalalisha, ameandika executive orders(amri za raisi) kibao ambazo zinakiuka katiba. Yaani anatawala kidikteta kidkteta tuu. Huyu Romney naye ni mchovu mwingine maana anataka kuendeleza empire ya marekani (vita kila kona ya dunia) lakini hataki kuilipia yaani anakwepa kodi.
 
Back
Top Bottom