Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,025
- 24,999
Obama naye ni mchovu vile vile si Romney peke yake. Ukiangalia uraisi wa Obama utaona kwamba ameikanya kanyaga ile katiba ya Marekani. Kafanya mengi tuu ambayo amekiuka katiba ya Marekani. Ameivamia Libya bila ya bunge kuhalalisha, ameandika executive orders(amri za raisi) kibao ambazo zinakiuka katiba. Yaani anatawala kidikteta kidkteta tuu. Huyu Romney naye ni mchovu mwingine maana anataka kuendeleza empire ya marekani (vita kila kona ya dunia) lakini hataki kuilipia yaani anakwepa kodi.
Marakani haikuvamaia Libya, ilishiriki kama sehemu ya NATO. Usihiriki wa marekani kijeshi kwenye operations za NATO ni jambo lililolahalishwa kisheria. Rais hawezi kwenda kuomba Congress kururhus jeshi la Marekani kushiriki kwenye operations za NATO; anaweza kufanya hivyo tu anapokuwa anataka kutangaza vita na taifa jingine kama ambavyo Bushi alivyfanya.
Uwezo wa rais wa marekani kutoa executive order umehalalishwa na katiba, kwa hiyo huwezi kusema kuwaalitoa excutive order inayokiuka Katiba.