GE2025 Mpina akwama Ugombea Urais ACT Wazalendo, Mahakama yatupilia kesi yake mbali

GE2025 Mpina akwama Ugombea Urais ACT Wazalendo, Mahakama yatupilia kesi yake mbali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,608


Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma imeitupa kesi ya Luhaga Mpina na ACT-Wazalendo, ikieleza kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) haipaswi kuingiliwa na chombo chochote kwa jambo ambalo ilifanya kwa nia njema.

Mpina alikuwa akipinga kuenguliwa katika nafasi ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 15, 2025 mbele ya mahakama hiyo na kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo Jaji Fredrick Manyanda.

Majaji wengine waliosikiliza kesi hiyo ni Sylvester Kainda na Abdallah Gonzi. Kwa uamuzi huo, Mpina hataweza kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu, ambao kwa sasa vyama vya siasa vinavyoshiriki vinaendelea na kampeni
 
Mpina aende kumuuliza mkewe Membe alichofanyiwa na Dalali 2020 😁😁, dalali lishavuta mpunga limetia mfukoni then anamchora anavyohangaika😁
 
.. haipaswi kuingiliwa kwa jambo lolote ambalo inafanya kwa nia njema ...
 
What if NIA sio njema ? na who is to decide kwamba NIA sio Njema au Lah!????
 
Back
Top Bottom