MPESA-TRA wanakusanyaje kodi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MPESA-TRA wanakusanyaje kodi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by saragossa, Mar 26, 2011.

 1. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Wana JF, nimekuwa nikifwatilia kwa karibu hii biashara ya VODACOM ya kutuma hela kwa njia ya MPESA, kitu ambacho nimeshindwa kuelewa au kujua kama kipo ni swala zima la ukusanyaji wa kodi ya mapato kutoka kwenye wakala wote wa MPESA. Kimsingi, na endapo nitakuwa nimekosea naruhusu kukosolewa, ni
  kwamba mpaka leo TRA imeshindwa kuweka systems in place za kukusanya kodi kutoka kwenye wakala wa MPESA.
  Je, hii ni deliberate move au ni mpango wa mtu au ni uzembe tu wa TRA au ni vipi?
  Mh Zitto kabwe juzi amezungumzia AIRTEL, je kamati yake hili hawajaliona au?
  Wana JF naomba tulidadili hili.
   
 2. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Usemacho kina mantiki. Nina mashaka kama TRA wameshafunguka macho kufuatilia nini kinaendelea au ndo wanamuachia bwana mkubwa azikusanye taratibu pasipo shida! Si unajua tena kuna wenyewe huko? Ila fungua kabiashara kako uchwara uone watakavyokushukia, kama mwewe vile!!!
   
 3. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,798
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sijui huko kufuatilia kwa karibu una maanisha nini??? weka maelelezo hapa tuone ulivyofuatilia na sio kujibanza kipembeni kwa wakala au ni vipi? Uliza vigezo na masharti ya kuwa wakala wa Mpesa ndio utajua hiyo kodi ya TRA inapatikana vipi na sio kukurupuka na kutaka kuonyesha umma una machungu na nchi yako. Huduma ya Mpesa inatusaidia sana sisi wananchi, ni vyema hata kama hailipiwi kodi inayoenda kunufaisha mafisadi, wananchi tunafaidika kwa kupata huduma.
   
 4. k

  kiche JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hapa kazi ipo!kulipa kodi hakuwezi kukuondolea huduma hii,kinachotakiwa kodi ilipwe (kama hailipwi),kwa maelezo yako ni kama hakuna umuhimu wa kodi.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu .... ninawasiwasi hujafuatilia na wala hujawahi kutumia Vodacom M-PESA .... unapotuma pesa na zikamfikia mtu na pale pesa zitakapochukuliwa na mteja as hard cash ndipo mahesabu yote yanapigwa kuanzia agency fee ya wakala, vodacom and all necessary tarrifs ..... kumbuka unapochukua (withdraw) M-PESA kuna ledger book inajazwa na wakala inayoonyesha message transmition number, kiasi ulichochukua, jina, ID na signature .... hiyo ndiyo account recording for TRA , tatizo ni mfumu mbaya wa ukusanyaji kodi wa TRA mbao hutegemea mtu kupeleka kodi mwenyewe
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  umeongea kama vile unajua jinsi TRA wanavyokusanya hizo kodi kwa M pesa.
  Ni vizuri kama unajua ila ni vizuri zaidi ukituelezea na wengine ili tuelewe badala ya kuleta dharau.
  Pia unaongea kama vile hujui umuhimu wa kodi. Ni vibaya kama hujui ila vibaya zaidi kama huulizi.
  Ahsante LAT kwa maelezo yako.
   
 7. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapa kuna issue mbili ambazo mwapaswa mzijue!
  Mosi, M-PESA ni another business line kwa kampuni ya vodacom. Mwisho wa siku revenues zitokanazo na M-PESA zinakuja kujumlishwa kwenye revenues obtained from data and voice business lines ili kupata gross income. Vivyo hivyo kwenye operating expenses, baada ya hapo gross income iliyopatikana zinaondolewa operating expenses ili kupata pre-tax profit. Pre-tax profit ndiyo inayo determine ni kiasi gani cha kodi kilipwe.
  Pili, kuna suala la TRA kukusanya kodi kupitia M-PESA system. Yaani M-pesa as a vehicle for collecting taxes from individual taxpayers. Mi nadhani hili ndo tulitakiwa tujadili, je efficiency ikoje mpaka sasa? Na taxpayer atabakiwa na evidence gani for future reference baada ya kulipa kodi?
   
 8. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Masaburi type...!!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mi nauliza kwanini tunapofanya hizi transactions kwa m pesa hatupewi source documents eg receipt?
   
 10. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Mi nadani kuna aina mbili ya receipt, electronic au hard copy. Ile message unayoipata kwenye simu yako baada ya ku-conclude transaction ndio receipt yenyewea. Maana inakuwa na reference number.
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  mbona hata hiyo electronic haijakamilika. Receipt bila muhuri wala sign! Bora watupe hardcopy.
   
 12. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wakubwa,
  naomba kuwafahamisha kuwa kila muamala (transaction) unaofanyika kwa MPESA ni unaweza kupatikana kirahisi kupitia Benki husika. Kwa ujumla kuna formula rahisi inayotumika, nayo ni:
  "Electronic" money = money in account. kwa maana Vodacom, tigo, airtel, zantel etc wana account ambamo wanaweka mapesa kuweza kuweka pesa kwenye mzunguko wa M-PESA, AIRTEL Money, etc. Nikipata nafasi nitawatumia maelezo jinsi mfumo mzima unavyofanya kazi.
  Hivyo, TRA hawana haja ya kuwatafuta mawakala waliko kijiografia, ila wanawajua "logically" na wanaweza kushughulika nao vilivyo wakiwa wameketi kwenye kiyoyozi.
   
Loading...