MPESA Faida na Figisu Figisu za VodaCom 2016/2017

MPESA Faida na Figisu Figisu za VodaCom 2016/2017

wafanyiwe auditing kwa hili kwa kweli ni wizi ni uliotukuka...nmefanya transactions constant laki 2 kila mwezi na nyingine kibao...nmepata faida 1000
Naomba kupata uelewa toka kwako kuhusu hili gawio;
1. Hili gawio ni kwa ajili ya watoa
huduma za m pesa au watumia
ji wa mtandao wao?
2. Ikwa ni kwa watoa huduma,
makubaliano ni asilimia ngapi?
3. Ikiwa ni kwa wateja, kwanini
watu walalamikie?
 
Naomba kupata uelewa toka kwako kuhusu hili gawio;
1. Hili gawio ni kwa ajili ya watoa
huduma za m pesa au watumia
ji wa mtandao wao?
2. Ikwa ni kwa watoa huduma,
makubaliano ni asilimia ngapi?
3. Ikiwa ni kwa wateja, kwanini
watu walalamikie?
Ni kwa wateja wa Mpesa na hakuna makubaliano yoyote
 
Imekuwa ni desturi kwa makampuni ya simu kugawana faida na wateja kutokana na matumizi ya huduma. Last week walianza Tigo na leo Voda wameenda hewani kwa kuanza kugawia faida watumiaji wa huduma za simu, na mie nimepokea Tshs 2,009.00 kutoka 219777 MPESA Faida tarehe 30/1/17 saa 8:27.

Kiukweli sikubaliani na faida hii kutokana na volume ya transactions kwa maana ya thamani ni bora wasiwe wanagawa manake itaonekana tumewapa watu faida kumbe pesa tume pigwa. Kama ilivyo desturi JF ni paa la bati kwa maana halikai na maji, naanzisha mjadala kwa maana wajuvi wa mambo waingie chaka kujua hawa jamaa wanatafutaje hiyo faida na wanaigawa vipi ili TCRA watuokoe na kupigwa kila eneo kama kodi tunalipa wenyewe kwa kila transaction inapofanyika vipi na faida iwe ndogo kwa kiasi hiki.

Wasi wasi ndio akili, zile namba za kuzisoma isijekuwa zimeingia na huku nakumbuka 2016 faida nilipata Tshs. 45,000 na mwaka huo nilifanya transactions chache kuliko za mwaka jana. Manake leo jioni lazima watatinga katika media na ujumbe kwamba wamegawia raia billioni kadhaa kama faida kumbe sanaa tu.

Kama hali ni mbaya, watu waseme upfront na window dressing sio poa katika kizazi hiki cha 4G. haina maana kwamba nimetolea jicho hiyo faida ni katika kuweka kumbukumbu sawa na harakati za bumper to bumper.
wezi wakubwa hawa hata mimi asubuhi nimekutana na buku jero wakati mwaka jana nimefanya miamala ya milioni milioni kama mara sita ukiachana na vilaki laki na hizo za kawaida na meseji zote bado ninazo watueleze kanuni wanayotumia kukotoa ili na sisi tujihakikishie kama ni kweli au tumepigwa changa la macho, mi nadhani ni bora waaache tu unafiki wa kujifanya wanagawa faida wezi wakubwa hao yaani nauchukia huu mtandao
 
Hata mimi nimepata 1000, ngoja tusubiri kama atatokea mtu kapata zaidi ya elfu mbili
Nimepata 3500 .ila mwaka jana nilipata 57000.na mwaka huu transaction nimefanya nyingi sana kuliko mwaka jana
 
Tigo pesa nimepata sh.89 sina tatizo nao maana kwa mwaka jana nilifanya transactions si zaidi ya nne, ishu ni kwa voda nnafanya transactions kila mwezi za kati ya sh. laki2 hadi 5 lakini nimepata sh.1000 Ngoja nijitathmini kwa mwaka huu kuhusu mpesa.
 
Nimepata 3500 .ila mwaka jana nilipata 57000.na mwaka huu transaction nimefanya nyingi sana kuliko mwaka jana
Mkuu inategemea na fungu lililotolewa kwa shughuli hiyo. Kama mwaka jana ilitolewa 50m na mwaka huu imetolewa 10m mgao lazima ushuke si unajua tena awamu hii[emoji23] [emoji23]
 
Me naamka nakuta msg nimepewa hongera kwa kupokea faida M-PESA 1,000/=
 
[QUOTE ="demi, post: 19507464, member: 400157"]Nami nimeambulia buku..teh teh[/QUOTE]

Hata mimi nimeambulia 1,000/=
 
Hataa Mimi nmeamka na muamala wa Tsh 1000.00 ! Ubabaishaji mtupu bora wasitoe kitu
 
Kwa kweli toka wanipigie simu kushinda 1M ya nogesha upendo, nawakubali sana. Na waliniwekea siku hiyo hiyo.
 
Mimi nimepata shs 1373, pamoja na kwamba huwa nafanya transactions nyingi sana kwa M-PESA, kuna ndugu yangu yeye hata hatumii sana line yake ya voda na hivyo hivyo transaction zake M-PESA ni ndogo sana maana alihamia halotel, yeye kavuta laki moja ya M-PESA faida, sasa sijui huwa wanagawaje faida au huwa wanafanya lottery
 
Wanagawa bils 15 watumiaji wa mpesa ni zaidi ya milion moja na kuendelea.
Sasa mlitegemea mpate kiasi gani kila mmoja?
Hali imekuwa ngumu kias kwamba waty wanategemea mgao wa mpesa utatue baadhi ya shida zao
 
Back
Top Bottom