MPESA Faida na Figisu Figisu za VodaCom 2016/2017

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,710
2,587
Imekuwa ni desturi kwa makampuni ya simu kugawana faida na wateja kutokana na matumizi ya huduma. Last week walianza Tigo na leo Voda wameenda hewani kwa kuanza kugawia faida watumiaji wa huduma za simu, na mie nimepokea Tshs 2,009.00 kutoka 219777 MPESA Faida tarehe 30/1/17 saa 8:27.

Kiukweli sikubaliani na faida hii kutokana na volume ya transactions kwa maana ya thamani ni bora wasiwe wanagawa manake itaonekana tumewapa watu faida kumbe pesa tume pigwa.

Kama ilivyo desturi JF ni paa la bati kwa maana halikai na maji, naanzisha mjadala kwa maana wajuvi wa mambo waingie chaka kujua hawa jamaa wanatafutaje hiyo faida na wanaigawa vipi ili TCRA watuokoe na kupigwa kila eneo kama kodi tunalipa wenyewe kwa kila transaction inapofanyika vipi na faida iwe ndogo kwa kiasi hiki.

Wasiwasi ndio akili, zile namba za kuzisoma isijekuwa zimeingia na huku nakumbuka 2016 faida nilipata Tshs. 45,000 na mwaka huo nilifanya transactions chache kuliko za mwaka jana. Manake leo jioni lazima watatinga katika media na ujumbe kwamba wamegawia raia billioni kadhaa kama faida kumbe sanaa tu.

Kama hali ni mbaya, watu waseme upfront na window dressing sio poa katika kizazi hiki cha 4G. haina maana kwamba nimetolea jicho hiyo faida ni katika kuweka kumbukumbu sawa na harakati za bumper to bumper.
 
Heri yako. Mwenzio nimepokea 1000.00 nilitoa macho nikaanza kuzihesabu zero kwa sindano. Nikidhani ni ka laki duuu kilinishuka shuuuu
Nami nimeambulia buku..teh teh
 
hatuna kampuni ya hovyo kama vodacom,
ni mwaka na kitu sasa, laini yao ninayo ila inaingia kwenue simu kwa nadra sana!
mwisho wataifunga!
 
wafanyiwe auditing kwa hili kwa kweli ni wizi ni uliotukuka...nmefanya transactions constant laki 2 kila mwezi na nyingine kibao...nmepata faida 1000
 
Aisee nimeshangaa,eti nimepokea tsh.2006 faida,faida gani hata kilo ya sukari haitoshi,kipindi kijacho wasinipe tena
 
Heri yako. Mwenzio nimepokea 1000.00 nilitoa macho nikaanza kuzihesabu zero kwa sindano. Nikidhani ni ka laki duuu kilinishuka shuuuu
Undermanned na yangu, hata mie asbuhi hii nimekuta msg ya m-pesa nikajua laki kumbu buku acha nirudie kuhakiki tarakimu
 
Imekuwa ni desturi kwa makampuni ya simu kugawana faida na wateja kutokana na matumizi ya huduma. Last week walianza Tigo na leo Voda wameenda hewani kwa kuanza kugawia faida watumiaji wa huduma za simu, na mie nimepokea Tshs 2,009.00 kutoka 219777 MPESA Faida tarehe 30/1/17 saa 8:27.

Kiukweli sikubaliani na faida hii kutokana na volume ya transactions kwa maana ya thamani ni bora wasiwe wanagawa manake itaonekana tumewapa watu faida kumbe pesa tume pigwa. Kama ilivyo desturi JF ni paa la bati kwa maana halikai na maji, naanzisha mjadala kwa maana wajuvi wa mambo waingie chaka kujua hawa jamaa wanatafutaje hiyo faida na wanaigawa vipi ili TCRA watuokoe na kupigwa kila eneo kama kodi tunalipa wenyewe kwa kila transaction inapofanyika vipi na faida iwe ndogo kwa kiasi hiki.

Wasi wasi ndio akili, zile namba za kuzisoma isijekuwa zimeingia na huku nakumbuka 2016 faida nilipata Tshs. 45,000 na mwaka huo nilifanya transactions chache kuliko za mwaka jana. Manake leo jioni lazima watatinga katika media na ujumbe kwamba wamegawia raia billioni kadhaa kama faida kumbe sanaa tu.

Kama hali ni mbaya, watu waseme upfront na window dressing sio poa katika kizazi hiki cha 4G. haina maana kwamba nimetolea jicho hiyo faida ni katika kuweka kumbukumbu sawa na harakati za bumper to bumper.
Nataka nikujibu lakini je unawadai?
 
Wanachokifanya hawa voda wanawagawia kila mteja wao kati ya bujut au jero

Ova
 
Back
Top Bottom