Habari wakuuuu, na changamoto kidogo na mpenzi wangu, nimekuwa nae kwa mahusiano Kama miaka minne ivi mpaka Sasa, time naanza nae mahusiano alinikuta Niko vizuri kiuchumi, kifupi nilikuwa namgharamia Kama ambavyo mwanaume upaswa kumjali mpenzi wake kwa kila kitu, Hali ya kwamba uyo mpenzi wangu Ni muajiliwa serikalini Tena kazi nzuri tu na mshaara wake Ni zaidi ya Million. Katikati apa mipango yangu imeyumba kidogo, nikamuomba aniazime pesa kidogo ambayo nitaongezea kwenye Kodi ya nyumba ambayo hata yeye uwa anafikia akija Dar, kwakuwa kituo chake Cha kazi Ni nje ya Dar, akanijibu Hana pesa wakati najua kwenye account yake mpaka kiwango alicho nacho, Tena kwenye Kodi nilipungukiwa laki mbili tu kwa kwa maaana nilikuwa na million Moja na laki sita yeye aniongezeee laki mbili tu, akadai Hana pesa, dahhh nikaona isiwe tabu nikaongea na mwenye nyumba, Ana nieshimu namieshimu kanielewa Sana na kumbe wasi wasi wangu tu. Baaada ya kulipa iyo Kodi nikawa mweupe Sina hata senti, kwakuwa na miradi yangu mikubwa nje ya mkoa wa Dar nayo ikawa imekaaa vyema ivyo ikanibidi nauli tu niende uko Mkoani nikamuomba elfu 30 tu akanijibu Sina na kuniambia unadhani kila mda Mimi na pesa tu, wakati najua mshaara wake na najua kwenye account Ana kiwango gani??
Nikafanya yangu Mimi nikaenda Mkoani, kaja Dar kafikia kwenye nyumba ile ile aliyogoma kuniazima laki mbili ya Kodi, gari yangu anatumia na mafuta naweka Mimi, chakula changu anakula, starehee naampa, pesa ya matumizi naampa nikikwama yeye mgumu, nampenda ila rohoo ya kumuacha inanijia kwakuwa uyu naona Ni mbinafsi wa kiwango Cha lami....nimfanyeje uyu kiumbe Kama namchoka ivi.