Mpenzi wangu kaniibia kila kitu, katoroka

Mtumie ujumbe kuwa unamkatia RB na kutoa tangazo (pamoja na picha zake) kwenye magazeti na mitandao ya jamii kuwa anatafutwa kwa wizi, atarudi mwenyewe tena kimya kimya kama alivyoondoka.

Kuna ndugu yangu alikuwa anamdai mtu pesa zake akatumia hii mbinu, karudishiwa pesa zake zote ndani ya siku mbili tu.
 
huyo piga kimya usimtafute wala nini assume ndo umemaliza shule anza maisha tulia kama maji ya mtingini japo ni ngumu , usikurupukie mwanamke yeyote kwanza halafi hasira zikiisha jipime upya. huyo anategemea utamtafuta umlilie lilie ndo maana angekuwa yeye hana makosa kwanini asichukue nusu ya vitu vingine aache? siku/mwaka akikutafuta mpe shart la kuridisha vitu vyote na avipange kama vilivyokuwa na ukiwa haupo then umbane akuambie alimaanisha nini alivyovibeba
 
Sharo,ina maana hyo binti humjui kwao? huwajui ndugu zake? umesema ni mke? basi nenda kwao...nijuavyo mimi mke akiondoka na vitu vyako amekusudia umfuate alipo,bado anakupenda huyo> ila unaonekana wewe ni tatizo,yaani badala ya kulilia kua kaumiza moyo wako wewe unalilia vitu....

mmeibiana.:blah:
 
habari wanajukwaa,

labda nianze kwa kusema haya sasa ni mapenzi au wizi? Mnamo juzi kati siku ya jumapili tuligombana na mke wangu lakini ulikuwa ni ugomvi wa kawaida tu, kama mnavojua katika mapenzi lazima iwepo mitafaruku ya hapa na pale, tukanuniana siku nzima lakin kufikia jumatatu kila mtu akawa kama ameshapotezea hivi.

Jana kaniandalia chai vizuri, nikanywa nikaondoka zangu kazini, cha ajabu jioni narudi kazini nakuta hakuna mtu wala hakuna kitu cha aina yoyote mule ndani kwa maana nyingine (ametoroka) kabeba kila kitu kilicho chake na kisicho chake, na hapa nilipo nilienda kulala kwa rafiki yangu sijaenda kazini na sielewi nifanyenini.
huyo kweli ni mke au changu?
Mkome kuokota okota wanawake
 
Kweli mjini tunatofautiana changamoto. Hahaha sipati picha kabeba godoro, kitanda, masufuria. Atakuwa na undugu na lawrence masha. Alipokosaga ubunge mwanza alibeba hadi madekio
 
He he he.......pole sana.......
Naelekea Bunda kutatua matatizo ya walimu .......nikirudi nitakwambia cha kufanya.........

Naomba nitaftie mke, hasa hawa walioajiriwa mwaka huu, asiwe na mtoto plse.
 
Nakupa ushauri mkuu, utakapoamua kupata mwanamke mwingine hakikisha ana dhamana kama mkopo wa benki ili akikuibia tena unalipwa na dhamana yake. Hapo utakuwa na amani vinginevyo utashindwa kwenda kutafuta hela kwani muda wote utakuwa na hofu ya kuibiwa tena!
 
Duh.!! pole bro hata mimi yalinikuta yaani cwezi kusahau mwezi Juni 2011 nikiwa kazini nilibebewa na my X-wife kila kitu mpaka kopo la chooni.!! ckujua nifanye nini.!! we achana nae anza upya cha msingi omba uzima maisha yatasonga tu.!!
 
Mtumie ujumbe kuwa unamkatia RB na kutoa tangazo (pamoja na picha zake) kwenye magazeti na mitandao ya jamii kuwa anatafutwa kwa wizi, atarudi mwenyewe tena kimya kimya kama alivyoondoka.

Kuna ndugu yangu alikuwa anamdai mtu pesa zake akatumia hii mbinu, karudishiwa pesa zake zote ndani ya siku mbili tu.

asante kwa ushauri
 
He he he.......pole sana.......
Naelekea Bunda kutatua matatizo ya walimu .......nikirudi nitakwambia cha kufanya.........

Nimebaki kustaajabu.....maana yaliyowakuta wale maticha , hakika hawatakaa wasahau mpaka wanaingia kaburini.
 
Back
Top Bottom