Mpenzi wangu hataki tushirikiane katika maswala ya dini

Mpenzi wangu hataki tushirikiane katika maswala ya dini

Totos Boss

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
5,454
Reaction score
1,569
Wana jamvi naomba ushauriwenu juu ya kinachonisibu.

Ni muda wa mienzi 7 sasa toka nibahatike kuwa na mpenzi wangu ambae tunatofautiana dini. Kwa kipindi chote nimekua nikimpa kampani katika shughuli zake za kuabudu kama kuenda nae kanisani. Mimi ni muislam na hivi sasa nimo katika mwenzi mtukufu wa RAMADHANI nilimuambia anipe kampani nae afunge akaniambia hawezi sasa hata hili la kunipa kampani kwa kunipikia futari na kuniacha huru wakati wa mchana (asinidai penzi ) pia hataki.

Natanguliza shukurani zangu kwa michango yenu
 
Nitumie namba yake ya simu nimuonye kwa kweli sio tabia nzuri anavyofanya. Nataka nijue ni kwa nini hakupi ushirikiano katika kipindi hiki kugumu cha mwezi mtukufu
 
sasa ambacho huelewi n nn? Kama kusoma hujui hata picha huoni?
 
Mkuu
Unaweza Kuwa Na Tatizo Wewe Mwenyewe
Dini Yako Hujui Imekataza Zinaa Halafu Mwezi Huu Unapiga Game Mchana Duh. Una Shida Sana Umeamua Kushinda Njaa Wewe Kabisa Mambo Ya Dini Kuna Kupeana Kampani?
Kizazi Chetu Hiki Kazi
 
We una matatizo sio bure, akuache huru mchana tu, halafu usiku kama kawaida, kwani umefunga naye ndoa, we utakuwa sio muislam, kwanza huruhusiwi kupikiwa futari na demu wako hatasiku moja.No research, no right to argue
 
Hapo duniani haupo na ahera unatafutwa,, leo kanisani kesho msikitini halafu ni mtoto wa kiume, ukitegemea ending iwe nini??

My take, mwache akatae kukupa ushirikiano maana kwa kufanya hivyo anakusaidia wewe katika kufunga kwako,, huyo siyo mkeo kiasi cha kudai rights za kukupikia katika mwezi mtukufu.
 
Watu kama nyie wenye undumilakuwili ndio mnaturudisha nyuma kimaendeleo,Sio siri wazazi wako wanakazi kubwa sana ya kukupa elimu ya kujitambua!
 
Mkuu
Unaweza Kuwa Na Tatizo Wewe Mwenyewe
Dini Yako Hujui Imekataza Zinaa Halafu Mwezi Huu Unapiga Game Mchana Duh. Una Shida Sana Umeamua Kushinda Njaa Wewe Kabisa Mambo Ya Dini Kuna Kupeana Kampani?
Kizazi Chetu Hiki Kazi

umeongea point sana. dini zote zimekataza zinaa. mchana afunge usiku duuh
 
Vijana wa siku hizi wanakuwa miili na vimo lakini akili zao zinabaki pale pale....
 
Watu kama nyie wenye undumilakuwili ndio mnaturudisha nyuma kimaendeleo,Sio siri wazazi wako wanakazi kubwa sana ya kukupa elimu ya kujitambua!

Huyo naye ni mjenzi wa taifa...ndio maana taifa linadumaa kimaendeleo....
 
Nitumie namba yake ya simu nimuonye kwa kweli sio tabia nzuri anavyofanya. Nataka nijue ni kwa nini hakupi ushirikiano katika kipindi hiki kugumu cha mwezi mtukufu

Ah! mkuu namba ya simu. Sina hofu sana nawe ila Uchipukaji wako vipi?
 
Mkuu
Unaweza Kuwa Na Tatizo Wewe Mwenyewe
Dini Yako Hujui Imekataza Zinaa Halafu Mwezi Huu Unapiga Game Mchana Duh. Una Shida Sana Umeamua Kushinda Njaa Wewe Kabisa Mambo Ya Dini Kuna Kupeana Kampani?
Kizazi Chetu Hiki Kazi

Nashkuru kwa kinizindua mkuu.
 
Ndege wafanano huruka pamoja. mara nyingi mapenzi ya wawili wakiwa na dini tofauti husumbua sana kuanzia wao wenyewe mpaka pande zote mbili.
 
mwezi wa kushinda na njaa!
madrasa tunazipuuza, matokeo ndo haya.
 
Back
Top Bottom