Mpenzi wangu anavuta bangi

Mpenzi wangu anavuta bangi

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
6,016
Reaction score
5,300
Habari wana JF.

Kama nilivyo andika kwenye kichwa cha habari, huu ni mwezi kama wa 8 hivi nipo katika mahusiano na dada mmoja, kwa kumuangalia kwa kweli ni dada mrembo sana na anaejitambua.

Sasa tatizo linakuja kila siku jioni alikua ananiaga anaenda kwa rafiki yake, mwanzoni niliona ni kawaida tu sababu nilikua namwamini sana, mda ulivokua unazidi kwenda nikawa napatwa na wasiwasi.

Siku mmoja niliamua kufanya upelelezi mimi binafsi, aliniaga anaenda kwa rafiki yake kama kawaida yake, nilikaa kama dk 10 baada ya kuondoka na mie nkamfata mpaka nyumbani kwa rafiki yake.

Sikuingia ndani nilichungulia tu dilishani, niliwakuta wakivuta bangi bahati nzuri awakuniona, nirudi nyumbani siku hiyo sikumuuliza kitu, umepita kama mwezi hivi.

Juzi nikamuuliza kama anatumia bangi, bahati nzuri hakua na ubishi alikubali, anasema bangi anayovuta haina matatizo yoyote kwake eti ni starehe tu kama mimi nnavyokunya pombe.

Tumegombana sana, naombeni ushauri wenu kama kweli bangi na pombe ni sawa na kama anafaa japo tabia nyingi nyingi za ajabu kwa sasa bado sijaziona.

Najua yupo jamii forum na najua atausoma huu uzi na najua ataanzisha mtiti mwingine, poa tu mi natafuta ushauri tu.
 
Huyo demu wako nshamjua, alinambia hana mpango wa kuacha bangi. Alinambia ana mpenzi wake JE, kumbe ndo wewe?
mkuu huyu uwa sio sana kupost japo uwa anasoma sana post na commets za watu.atakua sio yeye japo kweli bangi anavuta
 
We umemkuta anavuta na ulimpenda na hajakudanganya na unasema hana tabia ya hovyo sasa shida nini????!!!
Si umesema ni muelewa pia ni mrembo???!!!

Purity ianze na wewe uache pombe naye aache smokie muwe watu sober! !!!
 
Mbona wanaume wanavuta,wanawake wanavumilia,ni wakati wako sasa kumshauri na kumkanya aache hiyo tabia ya kutumia madawa ya kulevya ni HATARI!
Ntajirahidi nione kama ataacha bangi ni mbaya sana.
 
mkuu huyu uwa sio sana kupost japo uwa anasoma sana post na commets za watu.atakua sio yeye japo kweli bangi anavuta

Usijipe sana uhakika mkuu. Watu wanamiliki ma İDs kibawa...
 
We umemkuta anavuta na ulimpenda na hajakudanganya na unasema hana tabia ya hovyo sasa shida nini????!!!
Si umesema ni muelewa pia ni mrembo???!!!

Purity ianze na wewe uache pombe naye aache smokie muwe watu sober! !!!
Kwani mkuu pombe inaondoa upurity wa mtu?bange sio nzuri mkuu nadhani ilo halina ubishi.
 
Back
Top Bottom