Surya
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 8,379
- 12,574
Mimi sio mwandishi mzuri lakini naomba niende moja kwa moja kwa mada husika. Dhumuni naomba ushauri kwenu wakuu nini cha kufanya.
Mimi nina umri wa miaka 24 (male) nimeanza kazi mwaka huu mwezi wa 7 katika zahanati (private sector). Then mwezi uliopita mwishoni ndio nilianza mahusiano rasmi na mpenzi wangu ambae nilionana nae miaka 8 iliyopita yeye kwa sasa ana miaka 21. Kazi anayofanya ni hotel magemenent, according to professional yake.
Tupo mikoa tofauti mimi kanda ya ziwa huku mashariki yeye yupo mikoa ya kaskazini. Alikuja nilipo first lakini sijamtambulisha bado kwa wazazi, lakini mimi nilipo kwenda kwao alinitambulisha kwa wazazi wake.
For sure she is sexually active. Just why anadai sana maisha ya peke yake hayataki, na pia ana heshima na ni mwanamke anayependa kusema kweli muda wote. Kwa upande wangu mimi ni mtu wa kiroho sana, nimekwisha acha kila tabia za kidunia ili tu niyafikie malengo yangu, sipo interested na tabia ya kubadili wanawake kwani mimi ni wa kiroho zaidi.
Kwa sasa tupo kwenye mzozo kuwa nitakamilisha lini process za kumuoa na tuishi nyumba moja na huku mimi hatua niliyofikia nina kitanda na godoro peke yake, na anataka endapo atakuwa mkoa ambao mimi nipo anataka nimtafutie na shuguli ambayo yeye atakuwa anafanya.
Kanipa majukumu hayo yote huku pia akidai mimi kukaa mbali na yeye ni tatizo kwani anakumbana na vishawishi vingi, nilijaribu kumueleza kuwa anipe miezi 6 ili nikamilishe maswala hayo yote lakini hataki na anadai kuwa miezi 6 ni mingi na malengo yetu itakuwa ngumu kutimia.
Naomba ushauri wenu nifanye nini na kwa sasa kazi za private zote maslahi ni madogo pande zote mbili, na pia familia zetu si familia tajiri, zote zinapambana na kusomesha watoto.
Kwa upande wangu mimi pia nampenda sana na sitaki kumpoteza, naweza kutafuta mwanamke mwingine lakini nahofia sitapata atakayenifaa zaidi yake kwani naelewa kiundani umuhimu wake na upekee wake. Pia najua yeye pia ananipenda, lakini naona swala la pesa linataka kuwa kikwazo kwetu, na yeye anashindwa kuwa mvumilivu.
Ushauri wenu wakuu, kama kuna lingine la kueleza kuhusu mimi na yeye nitaendelea kuelezea...