Mpenzi wangu anasema hawezi kuolewa bila harusi

Mpenzi wangu anasema hawezi kuolewa bila harusi

Ivi ni kukwepa majukumu ni nini aswa? Mbona wanaume hampendi harusi? Ivi hela yenu mnayowachangia wenzenu haiwaumi? Shame on you men
 
Ndugu zangu wanajamiiF,

Nina mpenzi wangu yapata mwaka sasa, lakini cha kushangaza anasema hawezi kuolewa bila harusi na mimi sipo tayari kufunga harusi, na anasema anaomba Mungu apate bwana atakaye muoa kwa harusi.

Naombeni ushauri wenu

Huyo atakuwa ni mchaga....bisha!
 
Mi naamin mapenzi mnayo nyinyi na ukwel wa mapenzi mnaujua ninyi, kwahiyo ualisia wa maamuz sahihi ni wewe na mwenzie. Pia kumbuka kwamba watakao ishi ktk hiyo ndoa no ninyi....

Fanya maamuz sahihi
 
Yani hata mie tatizo hili linalomsibu mleta mada linanisumbua.Eti anataka sherehe na mbwembwe kibao.Mie sipo tayari.
 
Huyo Dada yuko sahihi kabisa mfanye sherehe kabisa tendo hilo hutokeaa mara moja maishani. Sasa kwanini muishi bila kuhalalisha ndoa
 
Ongea na mwenzio siye hata tukikupa ushauri hautawork ,mueleze kwanini hautaki kufunga harusi...NB..Kuna tofauti kati ya ndoa na harusi rudi tena!!
 
kipi hujakielewa sasa? Na wewe kwa n i ni hutaki kufunga naye ndoa? Unamwoa kama mchepuko si kumdhalilisha huko? Kwa nini unakwepa kuweka mkataba kamili hadharani?

Bila shaka yuko juu sana kimaadili na ni mwadilifu na mkweli kuliko wewe na hivyo you are not for her. Tafuta mbabaishaji mwenzako.

soma vizuri uelewe usikurupuke!
 
Sasa wewe kama unampenda na uko tayari kumuoa hutaki kufunda ndoa ili iweje sasa? huna uwezo au hutaki tuu? just expln
 
Huyo Dada yuko sahihi kabisa mfanye sherehe kabisa tendo hilo hutokeaa mara moja maishani. Sasa kwanini muishi bila kuhalalisha ndoa
tendo kutokea mara moja siyo kigezo cha sherehe. pia, kwani bila harusi ndoa inakuwa siyo halali?
 
Olaph.uk, hongera kwa hatua ya kimaamuzi uliyofikia. Hali kama hiyo imenikuta hata na me, kama umejiridhisha na hali iliyopo, kufunga ndoa ya kimila, kidini au kiserikali ndio jambo la kiungwana. Sherehe baada ya ndoa (harusi) hizo ni mbwembwe tu. Isitoshe kufanya harusi ni gharama sana.
 
sherehe muhimu kaka, yanini kuingia ndani kimya kama mwizi wakati nindoa halali? ebu mpe heshima mamawanao, mrs, mahabuba, mbona harusi hata ya milioni inawezekana, mnaandaa ndugu wapande zote mbili, na staffmates wenu basi mle, mfurahi kwa milioni tu, c lazima mamilioni bwana mpe heshima mwenzio
 
Ndugu zangu wanajamiiF,

Nina mpenzi wangu yapata mwaka sasa, lakini cha kushangaza anasema hawezi kuolewa bila harusi na mimi sipo tayari kufunga harusi, na anasema anaomba Mungu apate bwana atakaye muoa kwa harusi.

Naombeni ushauri wenu

Hebu kwanza tutofautishie hapo. Harusi ni nini na kuolewa au kuoa ni nini?
 
Mie mwenyewe nakaribia kufunga ndoa kanisani Tu nitulie...

Mimi hii bizness ya sherehe ya harusi sina kabisa...

Na hili nililiweka wazi mbele ya wazazi wake siku nalipa mahari....

mambo ya kuendeshwa na matukio sina kabisa...
 
sijaele, harusi au ndoa??? Maana hvyo ni vitu viwili tofauti.

Kama anataka ndoa yupo sahihi ila kama anataka harusi mmmh!!!

Ukishindwa waachie watakao muoa kwa harusi.
 
Back
Top Bottom