Mimi nina Mika 29 ninafanya kazi nzuri tu. Ila sasa nikawa sinamtu mda mrefu nikajikuta natuliza miwasho kwa Dereva mmoja wa bajaji.
Sasa swala linakuja kuwa tumedumu kwa muda wa mwezi na Sasa nimegundua ni mjamzito wa week mbili. Kwanzia mwanzo kabisa siku ya Kwanza aliniambia usije beba mimba yangu kua hawezi kulea Saiv.
Nimemwambia juu ya ujauzito anasema nitoe yeye hataki kulea kwani anamtoto mmoja na anashindwa kuhudumia....
Je mnanishaurije?
Pole sana.
Kosa la awali ni kukutana kimwili kabla ya kukamilisha taratibu.Ni kosa ambalo dini zote na mila haliruhusu.Inahitaji taratibu ya msamaha wa Mungu wako.
Pili,jaribu kuwaza huyo unayetaka kumtoa (kukatisha uhai wake) ni binadamu kama wewe (na si ajabu atakayekuja kuwa bora zaidi yako ama yetu sote) ambaye, si ajabu ndie kiumbe pekee utakayejaliwa.
Kutoa mimba ni ukatili usiomithilika.Infact,neno sahihi ni 'KUUA MWANANGU MWENYEWE NILIYEJAALIWA' kwa utashi,pesa na hiyari yangu tena kwa ubinafsi wangu na kutojali kwangu.
Umeshasema mwenyewe kuwa 'una kazi nzuri tu',je,hiyo haitoshi? Kukubaliwa na huyo mwanaume kuhusu malezi au wewe kuamua kumlea lipi ni jema na bora zaidi?
Kosa likishafanyika,lisifanyike kosa jingine(tena baya na kubwa zaidi) ili kulifuta au kusawazisha kosa la wali.
Huyo mtoto si ajabu ndio baraka yako ya pekee-hatuombei hilo.Nakuombea upate wengi utakavyo.Ila,nani ajuae mipango ya Mungu?Na hata ukiitoa ukaja kupata wengine,siku akili na moyo wako vikikaa sawa,utamkumbuka na huyo uliyemtoa na kujiuliza/kujilaumu kwa mengi.Ujana mara nyingine huwa una ujinga mwingi sana uliofichika,hadi utakapopevuka zaidi.
Tuwe na huruma.Haifai hata kufikiri hili la uuaji,hasa kiumbe ambeye ni too innocent,vulnerable na wanaotaraji upendo na ulinzi toka HASA kwa wanaowaleta humu duniani,yaani wazazi au mzazi,si vinginevyo.
Kuua kiumbe ambaye alishapitishwa na Muumba kuwa awepo duniani hai,nadhani pia ni kumpinga Mungu.Kuua kiumbe ambaye si ajabu angekuja kuyafurahia mno maisha yake na kuyapenda,ni sawa na kujiua mwenyewe.Kiumbe ambaye si ajabu ataleta maana,thamani,suluhisho na faraja kwa maisha ya wengi,pamoja na kwa wazazi wake.Kiumbe ambaye si ajabu maisha yake yatakuja kuwa ya maana na thamani zaidi hata kuzidi waliomzaa.
Please,usiitoe hiyo mimba!!!