Mpenzi wako wa kwanza kabisa yuko wapi?

Mpenzi wako wa kwanza kabisa yuko wapi?

Yupo ana watoto watatu na ndoa yake yenye furaha. Huwa tunasalimiana kimtandao coz tupo marafiki. Last time nilikutana nae MNH nikiwa nasubiri wife ajifungue, we hugged na kupiga stories mbili tatu. Hatuna hard feelings na heshima mbele kama tai.

Wengine hapo wakikutana wanawaza kupasha kiporo tu
 
Mkuu inaonekana ulikua unampenda sana yeye T,
"Nje" unamanisha wapi?
Ulikua unajua viwanja vyake huko nje?
Daa! mkuu kitu kimepanda kinyamwezi ni ile mbaya, kwao Tabora, mawazoo! alikuwa na ka hekima fulani hivi!
Nje na maana ya, Western Maseru- Kingdom of Lesotho, baadaye akahamishiwa Libreville- Sao tome and Principe! na Reunion, UNICEF.
 
Yupo ameolewa,watoto wawili,anaishi nyumba ya familia,maisha yamemchapa kweli kweli,mumewe mkorofi,mlevi na malaya.mwaka jana alinitafuta,nakiri nilimnunulia simu,pia namsaidia shida ndogo ndogo.
Mara nyingi tukiongea kwenye simu huwa analia.Sio siri nakua namwurumia sana.
Msaidie tu mkuu, ilà usimle. Najua hiyo huruma inaweza kuleta mambo ilà ukisimamia hivyo utaona vile atakuheshimu.
 
Wakuu Salaam;

Kila mmoja hupitia mambo kadhaa katika mahusiano na mojawapo ni hili la mahusiano kuvunjika kwasababu mbalimbali.

Binafsi Mpenzi wangu wa kwanza tuliachana kwasababu kadhaa baada ya yeye kumaliza kidato cha sita na mimi kwenda Chuo. Alikua akisoma huo ukanda ulipo mkoa wa Dar Kwa upande wa elimu ya sekondari ngazi ya A level.

Baadaye alichaguliwa kwenda Chuo morogoro maana aliniambia hadi fani aliyochaguliwa kwenda kusoma. Kwa kipindi tulichoachana hakukua na mawasiliano ya karibu tena.

Mwaka huu 2020 niliambiwa na rafiki yake kwa sasa yuko Dar na ameajiriwa na kampuni moja hivi kwenye kitengo kizuri tu. Kuna Nickname alikua akiipenda sana nimwite hivyo nimemtafuta instagram nimempata na kuona picha zake. Binafsi nimeshawishika sana kurudiana naye sema kwa sasa haiwezekani maana tayari kaolewa na ana watoto watatu.

Mme wake ana kazi ya kawaida tu hapo mjini ila huyo dada ndiyo ana kazi nzuri.

Niko nabungaa tu sahivi, sijajaribu hata kumtafuta kupitia instagram nimsalimie zaidi ya kucheki posts zake. Kuna siku niliona kaposti yuko na mmewe na watoto wao, nilikula kwa macho tuu.

Wakati mwingine naona posts yuko kwenye seminars, vikao mbalimbali n.k

Huenda tungekua mbali kimaisha kama tungekua pamoja. Nalolitambua ni kua kwenye maisha hamna haja ya kulalamika au kuhuzunika. Ni kuchukua ustaarabu tu.

Vipi upande wako, unafahamu alipo mpenzi wako wa kwanza kwa sasa na ungetamani kurudiana naye?
Endelea Kula tu kwa macho hata ucjaribu kumvurugia ndoa yake
Toto lilikuwa lako ukalipoteza kizembeeee
 
Daa! mkuu kitu kimepanda kinyamwezi ni ile mbaya, kwao Tabora, mawazoo! alikuwa na ka hekima fulani hivi!
Nje na maana ya, Western Maseru- Kingdom of Lesotho, baadaye akahamishiwa Libreville- Sao tome and Principe! na Reunion, UNICEF.
Huyo unatakiwa umsahau na utafute mwingine..mbn wako sana
 
Yupo ameolewa,watoto wawili,anaishi nyumba ya familia,maisha yamemchapa kweli kweli,mumewe mkorofi,mlevi na malaya.mwaka jana alinitafuta,nakiri nilimnunulia simu,pia namsaidia shida ndogo ndogo.
Mara nyingi tukiongea kwenye simu huwa analia.Sio siri nakua namwurumia sana.
Dah Anajuta hlf kuna kitu kinamuumiza sana..hapo atazidi juta kama yeye ndiyo alifanya uamuzi wa kuvunja mahusiano au alikua na tabia fln ambazo siyo zilizovunja mahusiano.
Endelea tu kumpa sapoti!
 
Back
Top Bottom