Mpenzi wako akifa ndani kwako utafanyaje?

Mpenzi wako akifa ndani kwako utafanyaje?

wakuu kwema


huwa najiuliza sana mfano imetokea umekuw na mahusiano na demu alafu baada ya week akaja getho kulala

asubuh unamuamsha unataka uingie mishe mishe unashangaa haamki,unamtikisa unaona hatikisiki ,unammwagia maji haamki.unahamaki kuona anatokwa povu mdomoni,unamgusa unakuta wa baridii

unagusa kifuan unashtuka mapigo ya moyo hayadundi.


je utatoka nje uwajuze majiran?? wataamin vipi kama n bahat mbaya

je utatoroka?? hapa utakuw umejivua utu na itaonekana kama ulikusudia

ukibak tena ni msala tena msala kwel kwel

wakulungwa leo tupige story hii inshu ikitokea we utafanyaje japo hatuombei itokee.
KWA nchi ambazo zimepiga hatua kisayansi wanaheshimu na kufanyia kazi majibu ya autopsy ,pia justice system inafanya Kazi na inampa haki mwenye haki,ila kibongobongo Dr anaweza conclude natural death na ukahukumiwa vilevile
 
Yule jamaa wa dodoma mzee wa kugegeda Yuko wapi maana siku nyingi sijamuona humu
 
Ni vyema kuthibitisha afya ya demu kabla ya kumualika kulala gheto. Kama ikitokea ni kuripoti polisi na kupeleka mwili mortuary. Kama kutakuwa na kesi, basi utajitetea. Na kama ikishindwa kesi, basi unakubali matokeo, ndio dunia hiyo!
 
Nadhani kama ni kifo cha kawaida you won't be in trouble that much japo utasota sero wakati wa uchunguzi, kama umeriport mweneyewe itakusaidia zaidi maana hujaua ila amekufa kifo cha kawaida.
Friend of mine aliwahi kuchepuka na mke wa mtu kumbe bi dada anamatatizo ya moyo akazimia kwa masaa matano geto, kuanzia sa tano asubuhi mpka sa nne afu ni kijijini hakuna usafiri wa tax au bajaji useme angepeleka hospital kisiri, Alisalia akiomba Mungu amuepushe na kile kikombe.
Niliwahi muuliza askari mmoja wanamalizaje huu msala akasema kabla ya yote kisheria lazima utoe mahari kwanza ya marehemu maana ulimfanya mke wako kisiri hii mahari lazima ulipe( in case umekamatwa kwa kujipeleka au kusakwa)
Binafsi binti aliwahi kuzidiwa akiwa amelala kwangu. Nilichokifanya ni kuita tax sa nane usiku tukampleka hospital. Sikuwahi kuwa na wasiwasi kiasi kile katika maisha yangu but atleast I was confident hakuna nilichokifanya kilipelekea yeye kuumwa..
Mwisho vijana tuoe kutoka na mabinti za watu leo huyu kesho yule haileti picha nzuri.
 
Acha ujinga weww mtumbukize chooni fasta alafu chukua simu yake kaitupe sokoni huko utakuja kunishukuru
Kutupa mwili au sehemu ya mwili chooni, kwenye karo au mitaroni sikushauri. Kutupa mwili au sehemu ya mwili sehemu hizo sehemu hupeleka choo, karo na mtaro kuziba hivyo huhatarisha kuja kugundulika mapema.

Pia nature ya maeneo hayo hufanya mwili kuwahi kuharibika na harufu yake inaweza kua traced kwa urahisi.
 
Usiombe wala usitamani ikukute. Nakumbuka mwaka 2017 kama sijakosea nilikua Arusha na Ke tukalala lodge, katikati ya mechi nikahisi utofauti mtu kalegea na kaanza kuwa wa barid hata kuongea anashindwa aiseee nilishtuka sana nikamuita mara tatu bila majibu. Nikatoka nje chap nikafata dawa bila kujua hata ana tatzo gan, njiani zilinijia kumbukumbu za wimbo wa husein machozi alafu bidada ni mtoto wa mjeshi mzee wake ni mkali sana. Nilifika duka la dawa nikiwa sina utulivu hata shati sijafunga, suruali yenyewe niliivaa tu bila chochote ndani yani nilivurugwa haswa. Nilimkuta mama wa kati ya 50-60 yrs mhudumu duka la dawa akaniomba nifunge shati then nikamueleza shida yangu ndio akanisaidia dawa na ushauri chap kwa haraka nikarudi lodge nikatoa huduma baada ya kama dakika 10 hivi nikaona hali imeanza kuwa shwari. Ilivyopita kama dakika 45 yule Ke akataka tuendeleze show, sijawai kataa ila moyo uliniambia hapana acha usifanye nikamvuta kifuani yeye akalala mimi sikupata usingizi mpaka kukakucha.
 
Kama ni mke wako?? Kafa inakuaje
Kma ni natural death ur freee hakutokua na kesi coz she's ur wife jpo upelelezi utafanyika na mkeo kupimwa ikijulikana ni murderer tafuta wakili wako eleza unachojua ajue anakusaidiaje
 
Wakuu kwema?

Huwa najiuliza sana mfano imetokea umekuwa na mahusiano na mwanamke halafu baada ya wiki akaja kwako kulala halafu asubuhi unamuamsha unataka uingie mishe mishe unashangaa haamki, unamtikisa unaona hatikisiki, unammwagia maji haamki. Unahamaki kuona anatokwa povu mdomoni, unamgusa unakuta wabaridi

Unagusa kifuani unashtuka mapigo ya moyo hayadundi. Je, utatoka nje uwajuze majirani? Wataamini vipi kama ni bahati mbaya

Je, utatoroka?? Hapa utakuwa umejivua utu na itaonekana kama ulikusudia

Ukibaki tena ni msala tena msala kwelikweli

Je, utafanyaje??
Nenda polisi toa taarifa. Mwili utapimwa mkuu.. simple kabisa hiyo
 
Back
Top Bottom