platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,366
- 11,156
Ndio, baada ya kutafakari sana mmeamua kuvunja mahusiano, kwamba hakuna mapenzi kati yenu na tofauti zenu ni kubwa. Mmoja kwenye mahusiano (Tumwite X) anajiona yeye ndiye yeye........Kifupi ujeuri mwingi na wakati mwingine hapokei hata simu anapopigiwa na mpenzi wake (Tumwite B).
Hayo yakapita majeraha yakapona na maisha yakaendelea. Katika pitapita za hapa na pale mjini mnagongana na hata kusalimiana, kimsingi hamko-close hata kirafiki. Mhanga wa mahusiano (B) haonyeshi kujali sana wala kuulizia yaliyopita, ni salamu na mwendo mdundo............
X anashangaa na anajaribu kuwauliza marafiki zake wawili "Inakuwaje B siku hizi yuko kimya hivi, sijategemea kama hatokuwa ananipigia simu hata baada ya kuachana"..........marafiki zake hata wao wanashangaa hawakutegemea yule mtu aliyekufa kaoza kwa rafiki yao X atakuwa hivyo!!
Na habari zinavuja na kumfikia B, naye anazisikiliza na kuziweka kando. Kifupi hana muda huo!...........Ingawa kadri siku zinavyokwenda X anaweweseka na Vi-SMS vya hapa na pale, lakini hajui afanye aseme nini na vipi. Taswira inayoonekana ni kuwa naye amepigika moyo, ingawa fursa kutoka kwa B haielekei kama itapatikana!
Mkasa wa kweli ambao bado uko moto...........Mimi mbea nitawafahamisha hiyo safari ya X na B kama itakoma kabisa.