Mpenzi anatafuna meno usiku, inaniogopesha sana

Hiyo ni hali ya kawaida sana ni mademu wengi huwa hivyo lkn ukimzoea inakaa pouwa na hamna madhara yoyote kwako kikubwa ni kero tu maana inaweza kukunyima ww uxngizi kawaida ndio maana huyo she anamaind
 
Heri ya weekend wadau!!

Iko hivi, miezi kadhaa imepita sasa Niko na uhusiano na binti mmoja hapa mjini! Sijawahi kubishana nae, yaani kwa kifupi tuko poa. Issue ni kwamba huyu binti akishtuka kidogo toka usingizin au akijigeuza tu, anatafuna meno balaa!!

Siku ya kwanza imetokea hiyo hali nililala nae kwa tahadhari lakini nilijipa moyo labda imetokea kwa muda tu.

Sasa kwa mara nyingine tena naona hali iko vile vile, nilijaribu kumashtua ndugu VP unakula nn usiku huu? Alishtuka akatulia, nilimwambia achama mdomo, sikuona kitu zaid ya meno na ulimi tu!

Asubuhi yake ali mind lakini tukayamaliza. Ukimsikiliza kwa karibu ni kama anakula rubber hivi. Yaani noma tupu. Sijui kama wenzangu mshakutana na tukio la aina hii.

Nipeni ushauri kwa sababu sijui Siku nyingine itakuwaje. Kama kuna dawa nitashukuru, nilimshauri aende hospital akasema haumwi, hivyo haoni haja ya kwenda huko.

Ni uhusiano ambao hauna muda mrefu..
Ushauri wako tafadhali.....
Sijui kama itakua ni kweli lakini nilisikia ushuhuda wa mtu mmoja alikua mchawi akasema dalili za mtu anaelishwa nyama ktk ndoto na wachawi usiku anatabia hizo za kutafuna meno so ukiona mtu wa ivo anahitaji kuombewa.
 
Mkuu mbona dizaini ulimuamsha mwenzio kutoka usingizini utadhani ni ugomvi au kama vita vile. Ndio maana alikumaindi. Kuwa romantic kidogo bro. Hiyo ni hali ya kawaida tu. Kubalianeni wote kuwa utakuwa unamstua kila ukimsikia akitafuna meno. But be very gentle and caring. Eventually ataacha tu !!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom