Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,104
- 43,357
Sijui kwanini inaonekana kuna msukumo mkubwa kwa Rais Samia Hassan kufanya hili au kufanya like. Inawezekana katika kuonesha uhuru wake kutoka kivuli cha Magufuli anajaribu kuridhisha makundi mengi. Lengo lake la kuendeleza kutekeleza ajenda ya Magufuli-Samia2020-2025 yeye ndio anajukumu la kuipanga Serikali kwa ajili ya ufanisi, weledi, na matokeo chanya (positive outcome).
Tumpe muda wa kujipanga, na kufanya makosa, na kuyasahihisha. Ikumbukwe hata Katibu Mkuu Kiongozi ni Mpya (ndiye anahusika Sana na teuzi zote za Rais). Shida ni kuwa inawezekana CCM (kama taasisi au vigogo fulani) wanataka watu fulani wakumbukwe. Hili si jipya...la maana isijekuwa wanajaribu kumdhoofisha Rais....hili halikubaliki.