Mwanamke anayetafuta faraja ya ndoa NJE YA NDOA huyo hakuwa MKE WA NDOA tangu mwanzo. Ndio maana ni muhimu sana kwa kijana kuchunguza binti urakaye awe mke wako, kuna mke na mwanamke. Sio kila mwanamke ni mke wa ndoa, wengine wamezaliwa kuipamba dunia na kutumika na kila mwanamume. Mke wa ndoa anajua jinsi ya kuipata furaha iliyopotea kwa mumewe, wala haenendi sawa sawa na makahaba ambao ni part time, ukimkwaza kwa hiki anatafuta mwanamume mwingine. Hao wamezaliwa kwa ajili hiyo.
Wanaume, ACHENI KUOA HOUSING kwa sababu ubora wa simu uko KWENYE OPERATING SYSTEM sio housing. Kama mtabisha basi angalieni huu mfano:
Ni nani awezaye kujisifu kwamba amenunua Youtong bus na kwamba anatarajia liweze kuleta faida miaka 20 baadaye? Japokuwa laonekana zuri kwa nje lakini sote twajua limetengenezwa kwa mtindo wa kuchuma faida ndani ya muda mfupi kisha kuondolewa sokoni. Ndivyo ilivyo vya mwanamke asiye na maadili ya ndoa. Huyo ametengenezwa atumike kwa kipindi kifupi tu cha usichana wake huku akijiingizia faida. Mwanamke kama huyu hana mtazamo wa muda mrefu, long term, anachotaka ni kukitumia vema kipindi cha usichana wake.
Wako walionunua magari kama benz, leyland, scania nk. Hawa wliweza kuingiza faida hata uzeeni. Mwanamke wa ndoa thamani yake ni kubwa kumpata, lakini ukimpata atakupa faida kidogo kidogo kwa muda mrefu mno. Mtazeeka pamoja.
Sasa mleta mada anajitapa kulala na makahaba waliogeuzwa kuwa wake za watu. Pamoja na hilo ilimpasa kuwaheshimu wanaume waliowaoa. MWANAMUME MPUMBAVU HUJISIFIA KULALA NA WAKE ZA WANAUME WENZAKE. NI MJINGA AMBAYE MAANGAMIZI YAKE HAYAKO MBALI, NA SIKU YA KIAMA CHAKE INAKUJA KAMA MWIVI.