Mpende sana mkeo, la sivyo...

Mpende sana mkeo, la sivyo...

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,988
Sijakuibia mkeo, nilimuokota jalalani mwa moyo wako. Unakumbuka kipindi kile ulipokuwa unashinda siku nzima bila hata kumjulia hali? OTEA? Nilikuwa namkumbuka kila saa kujua kama yupo sawa na anaendelea vizuri.

Unakumbuka kipindi kile unamdharau na kumpuuza? Aliniambia kuhusu hilo; nilijitolea kumpa muda wangu alipokuwa anahitaji kampani, nilimpa sikio langu kumsikiliza, nilimpa bega langu alipohitaji kulia na kifua changu kumfariji.

Pale ulipohisi atakufuatilia na mambo yako sisi tulikuwa bize kufurahia kampani ya kila mmoja wetu, na wewe ulikuwa mtu wa mwisho katika fikra zetu. Hivi unajua kila ulivyozidi kuumiza hisia zake ndivyo ulivyozidi kumsogeza mikononi mwangu?

Ulipodhani hatolala usiku kukuwaza na kukufikiria nilihakikisha analala bila moyo uliovunjika na kupondeka kwa kumuhadithia hadithi tamu na kumuimbia nyimbo nzuri za mapenzi.

Hivi ulidhani anakosa amani na furaha kulialia kila saa kwa ajili yako? Hapana nilikuwa mbunifu kwa kuhakikisha anacheka na kufurahia maisha muda wote kwa ajili yake niligeuka comedian na alikuwa ni fan wangu no1.

Endelea kumchukulia mkeo kama takataka sisi hatuna kinyaa tutamuokota tatamsafisha na kumpa thamani. Wengine tuna mioyo ya kike tukipenda tunapenda kweli.
 
Kati ya watu nawapenda,kuwaheshimu na kuwathamini duniani ni mke wangu aisee. Akihuzunika tu kidogo nakosa amani kabisaa.
Ni kweli lakini pia wanawake wastaarabu na heshima ni wachache, kuna mijitu ya uswahilini bana aisee!
 
mwamwala iyunga,

Labda umefanya linalokufaa lakini kama unafikiri kuchukua mke wa mtu ni ushujaa ujue unaemuumiza ni huyo unaefikiri unamliwaza maana siku akijua kuwa ni msaliti wa ndoa yake na kujuta labda utakuwa umemsaidia kweli.

Lingine ni kuwa siku unayemkoga hapa akikukamata unajua atakavokufanya ujifunze kuwa wake za watu sumu maana ninalofahamu siku hiyo utaolewa tu na kuwa mke mwenza wa huyo mama.

Lakini hautakuwa na tabu sana maana umeshaeleza kuwa tayari Una viashiria vya kike. Kwa Ivo Endelea tu.
 
Ww unaefagilia Mke wangu , bahati yako una roho ya kike sitohitaji jerry nakukaribisha Kinyerezi mama chanja umsaidie mke mwenzio
 
Mkuu acha kuhalalisha uchepukaji..
Kama unafanya hayo yote kwa sababu anayahitaji mbona wewe hukwenda kumtolea mahari nyumbani kwao wakati anahitaji wa kumuoa?
 
Yan kila siku tuwapende wao tuuuuuuuu..njoon na mada nyingne...yan nipoteze muda wangu kumridhisha yeye kila siku....yeye vip
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom