Mpenda kula kwa watu.

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Kuna Mama mmoja huyo mchoyo kinoma, basi unaambiwa kuna siku kapika pilau lake la nguvu na kachumbari la kumwaga. Time ya kula ilipofika yule Mama akarudishia mlango wake ili aanze kuushughulikia msosi wake. Jirani ya Nyumba ya huyo Mama kuna Maza Mwingine yeye anapenda kula kwa watu kinoma.
Muda wa kula ulipofika yule mama mpenda kula kwa watu akajifanya kwenda kumtembelea yule Mama mwingine.

Alipofika tu akagonga mlango. kuona vile yule mama mchoyo fasta sana akauchukua msosi akaufunika na ndoo halafu ndoo akaiweka mbali kabisa kwenye kona ya ukuta utafikiri hamna kitu vile. kisha akamkaribisha mgeni ndani.
Basi yule Mama mpenda kula kwa watu kuona vile akamwambia yule mama mchoyo " Mama nanihii mimi sikai sana nimekuja kuazima hiyo ndoo tu!"
 
..yake ni kumwambia hiyo ndoo imeka maruhani ndani yake hivyo hawezi kuitoa!

..baada ya hapo,hata kuja doweya ataacha!asijerushiwa jini!
 
Back
Top Bottom