''Mpemba'' wa meno ya tembo afikishwa mahakamani

''Mpemba'' wa meno ya tembo afikishwa mahakamani

Nimehifadhi Mali ya wizi nyumbani kwangu,nimelipwa dola 4000 kwa siku tano nitashangaa police mkija kunikamata kwa sababu hayo Mali siyo yangu ila nyumba ni yangu,mkithubutu nitawauliza maswali magumu kumi,mbona ile nyumba iliyohifadhi pembe za ndovu kule Vietnam mbona mwenye nyumba hakukamatwa?@abdul mananasi
 
Mhhhh mbona kachoka...,hayuko kama alivyopigiwa debe na Mr President,,naona huyu mpemba mwengine sie wa Magufuli
 
Tena wote nasikia ni wanachama wetu na uchaguzi uliopita huko Iringa na Dar walimwaga pesa ili Chama chetu kishinde kama alivyofanya Singasinga na Lugumi.
 
Nakumbuka wale waliotungua ndege na kuua rubani Mwingereza waliokamatwa walikuwa "dhaifu kimuonekano" kama hawa. Je hii biashara hawa ndiyo vigogo wenyewe? Serikali wakamate vinara wanaopata super normal profit. Sasa utauwa vipi mtandano kama utajihusisha sana na vidagaa? Rich men wanafanya haya mambo si watakodi vijana wengine tu halafu wanabadili techniques?
 
Na yule mtoto wa mbunge aliyelipa fine ya 130mln baadala ya hukumu kesi yake nae ilikuwaje??!! Na yule mbunge anayehusishwa na bunduki 13 je??!! Lema yupo ndani kwa maneno ya ndoto tu, wabunge wa chama twawala ni siri!! !
Yule mtoto wa chama chetu kinachotawala
View attachment 435213
View attachment 435216
View attachment 435217

Mtuhumiwa wa makosa ya kukamatwa na nyara za serikali, Yusuf Ali Yusuf maarufu kama Shehe Mpemba (35) kushoto kwenye picha ambaye alitajwa na Rais John Magufuli kuwa ndiye kinara wa biashara ya meno ya tembo na wenzake Charles Mrutu (37), Benedict Kungwa (40), Jumanne Chima (30), Ahmed Nyagongo (33) na Pius Kulagwa (46) wamefikishwa mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba na hawakutakiwa kujibu chochote na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba Mosi, mwaka huu itakapotajwa tena huku watuhumiwa hao wakirudishwa rumande.

Hii ni Hati ya Mashitaka.

kisutu1.jpg

kisutu2.jpg

kisutu3.jpg
 
Anaonea vidagaa tu hivi hawa wakimtaja Kinana watasema wamewehuka au? Meli nzima sembuse hawa meno 50 tu? Vipi Lugumi? Vipi sare za geshi? Vipi escrow? Vipi ile meli?......
 
Back
Top Bottom