kweli mkuu yaani ukiwa upande ule utafanya unachotaka na utalindwa,kuna taarifa pia ya mbunge wa upande ule kukutwa na bunduki 11 za kuwindia wanyama pori lakini cha ajabu vyombo vyote vya habari vimeshindwa kutaja jina lake
kwani huyu ni nani? ukikamatwa na pembe za ndovu na ukikamatwa na nyama ndezi wote ni ujangili tu ...kama hawa wameweza kujinasua kwa 138 milioni haiwafanyi wao kuwa wasafi ni majangili tu otherwise mahakama ingewaacha huru kwahiyo utulie kama unanyolewa na unaposema tunatafuta umaarufu unamaanisha nini? wale wa mbarali unawajua wewe waliolipa 138 milioni?
Ni jamaa mmoja anaitwa Hasanool ni mfadhili wa timu ya simba jamaa nasikia ni jangili maarufu sana na ni mfadhili mkubwa wa chama KIBAHA aliwai kuhusishwa na wizi wa cathode toka zambia
Ni jamaa mmoja anaitwa Hasanool ni mfadhili wa timu ya simba jamaa nasikia ni jangili maarufu sana na ni mfadhili mkubwa wa chama KIBAHA aliwai kuhusishwa na wizi wa cathode toka zambia
kweli mkuu yaani ukiwa upande ule utafanya unachotaka na utalindwa,kuna taarifa pia ya mbunge wa upande ule kukutwa na bunduki 11 za kuwindia wanyama pori lakini cha ajabu vyombo vyote vya habari vimeshindwa kutaja jina lake
Hii kesi ya Padri aliyekamatwa ilimalizikia vipi ???
PADRI AKAMATWA KWA UJANGILI HUKU BUNDUKI 48, RISASI 764 ZIKIKAMATWA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, akionyesha bunduki aina ya AK47 kati ya silaha zilizokamatwa katika msako maalum wa ujangili.
Na Daniel Mbega, Namanyere
PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga (jina linahifadhiwa) ni miongoni mwa watu 50 waliokamatwa kwa ujangili na Kikosi Kazi cha Taifa katika Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa.
Padri aliyekamatwa ni wa Parokia ya Kirando katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, ambaye bunduki yake aina ya Rifle yenye darubini inadaiwa kutumika katika ujangili ndani pori hilo la Lwafi wilayani humo.
Taarifa za kipolisi zimeeleza kwamba, mbali ya kukamatwa kwa watu hao, pia jeshi hilo limekamata bunduki 48 za aina mbalimbali ikiwemo ya Padri huyo anayoimiliki kihalali, pamoja na risasi 764 na maganda ya risasi 101.
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jacob Mwaruanda amesema kuwa baadhi ya waliokamatwa silaha zao wanazimiliki kihalali lakini zinatumika kinyume na utaratibu wa kumilikishwa kwao.
"Watu hawa bado wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Kamanda Mwaruanda.
Kamanda Mwaruanda alisema kati ya bunduki 48 imo moja ya kivita aina ya AK47, bunduki 8 aina ya Rifle na risasi zake 83, Shortgun 19 na risasi zake 138, bastola 5 na risasi zake 133, magobore 15, magazine nne za bunduki aina ya Sub-Machine Gun, maganda matano ya bunduki aina ya Rifle, maganda 96 ya risasi za bunduki ya shortgun pamoja na vifaa vya kutengenezea bunduki za kienyeji na mitutu sita.
Watuhumiwa hao walikamatwa pia na nyara za serikali ambazo ni mikia sita ya tembo, nyama ya nyati kilo 20, miba ya nungunungu, ngozi moja ya paka-pori na pembe ya Nshya.
Kamanda Mwaruanda akifafanua jambo huku nyuma yake wanaonekana maofisa wa Kikosi Kazi cha Taifa pamoja na askari wa wanyamapori.
Kama Mwaruanda alitoa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa kwamba watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja kwenye vituo vya polisi au ofisi za serikali za vijiji kabla operesheni kabambe ya kuwatafuta watu hao haijaanza.
Rukwa na Katavi ni miongoni mwa maeneo ambayo ujangili kuua tembo umeshamiri sana hasa katika mapori ya akiba ya Lwafi na Hifadhi ya Taifa ya Katavi kutokana meno ya tembo kuonekana kuwa na soko katika mikoa mingine nchini na nchi jirani.
Kamanda Mwaruanda akionyesha kigudulia ambacho hutumiwa na majangili kubebea risasi.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Davies Mushi alinukuliwa hivi karibuni kuwa kuwepo kwa soko zuri la biashara haramu ya nyara za Serikali hususan meno ya tembo ni moja ya sababu zinazochangia ongezeko la ujangili katika hifadhi hizo.
"Soko zuri la meno ya tembo lililopo katika mji wa Mpanda (Katavi), Sumbawanga (Rukwa), Tabora na maeneo mengine ya nchi linachangia sana kushamiri kwa ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, lakini tunajitahidi kufanya doria ndani ya hifadhi na kukabiliana na kasi hii iliyopo ya kuua tembo inayofanywa na majangili ambao wengi wao ni kutoka nje ya nchi," alisema Mushi.
sasa kama uchunguzi unaendelea kwanini jpm amtaje ,huku ni kulindana na dalili za uwoga ,JMP unaogopa majangili,sasa wapemba wako wengi hata mtaani kwetu mpemba yupo,acha uwoga taja jina ,hatujaona tofauti yako na JK mwenzako alisema ana majina arubain ya majangili lakini mpaka anaondoka hajawai kuwataja na wewe umeanza maigizo hakuna mtanzania anayeitwa mpemba huo ni uwoga,mmezoe kuonea vitumishi vya ummaa mnakimbilia kwenye maTV kuuza sura,onyesheni ubabe wenu kwa mapapa sasa

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.