Mpemba aliyetajwa na rais ni nani?

Mpemba aliyetajwa na rais ni nani?

Wakuu naomba kufahamishwa kwa anayejua.
Juzi kati raisi alipotembelea wizara ya mali asili alimtaja mpemba kuwa anahusika na biashara ya pembe za ndovu, huyu Mpemba ni nani kwa anamjua atuambie na sisi tumjue adui huyu wa taifa.

Mpemba = Msomali
 
Wakuu naomba kufahamishwa kwa anayejua.
Juzi kati raisi alipotembelea wizara ya mali asili alimtaja mpemba kuwa anahusika na biashara ya pembe za ndovu, huyu Mpemba ni nani kwa anamjua atuambie na sisi tumjue adui huyu wa taifa.
Copied and pasted, courtesy Isambe wa JF
Hii ni kesi ya pembe zilizokamatwa HK na Kinana akatajwa tajwa, muhusika alikua Hasanoo(ndie aliepandishwa kizimbani na wenzake)

"Dalali wake ni yule "MPEMBA" Mwenye Mgahawa Wa chakula Pale Chagga street ,hata ile ya Shaba ni yeye ndiye aliye mletea wachina wa kununua, ndipo akavuta chake akaupendezesha mgahawa wake na Kujitupa kwenye JEEP NEW MODEL , pale wana chama chao na wakina IDD SIMBA cha kula Hela za Mahujaji!, na mengineyo!!

Kuna Ka Arabu kamoja kafupi kanaitwa Juma Iddi kenyewe ndio kanajitapa kamesha maliza mambo yote kwa majaji."
 
Hii kesi ya Padri aliyekamatwa ilimalizikia vipi ???

PADRI AKAMATWA KWA UJANGILI HUKU BUNDUKI 48, RISASI 764 ZIKIKAMATWA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, akionyesha bunduki aina ya AK47 kati ya silaha zilizokamatwa katika msako maalum wa ujangili.


Na Daniel Mbega, Namanyere

PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga (jina linahifadhiwa) ni miongoni mwa watu 50 waliokamatwa kwa ujangili na Kikosi Kazi cha Taifa katika Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa.
Padri aliyekamatwa ni wa Parokia ya Kirando katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, ambaye bunduki yake aina ya Rifle yenye darubini inadaiwa kutumika katika ujangili ndani pori hilo la Lwafi wilayani humo.
Taarifa za kipolisi zimeeleza kwamba, mbali ya kukamatwa kwa watu hao, pia jeshi hilo limekamata bunduki 48 za aina mbalimbali ikiwemo ya Padri huyo anayoimiliki kihalali, pamoja na risasi 764 na maganda ya risasi 101.
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jacob Mwaruanda amesema kuwa baadhi ya waliokamatwa silaha zao wanazimiliki kihalali lakini zinatumika kinyume na utaratibu wa kumilikishwa kwao.

"Watu hawa bado wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Kamanda Mwaruanda.

Kamanda Mwaruanda alisema kati ya bunduki 48 imo moja ya kivita aina ya AK47, bunduki 8 aina ya Rifle na risasi zake 83, Shortgun 19 na risasi zake 138, bastola 5 na risasi zake 133, magobore 15, magazine nne za bunduki aina ya Sub-Machine Gun, maganda matano ya bunduki aina ya Rifle, maganda 96 ya risasi za bunduki ya shortgun pamoja na vifaa vya kutengenezea bunduki za kienyeji na mitutu sita.

Watuhumiwa hao walikamatwa pia na nyara za serikali ambazo ni mikia sita ya tembo, nyama ya nyati kilo 20, miba ya nungunungu, ngozi moja ya paka-pori na pembe ya Nshya.


Kamanda Mwaruanda akifafanua jambo huku nyuma yake wanaonekana maofisa wa Kikosi Kazi cha Taifa pamoja na askari wa wanyamapori.

Kama Mwaruanda alitoa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa kwamba watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja kwenye vituo vya polisi au ofisi za serikali za vijiji kabla operesheni kabambe ya kuwatafuta watu hao haijaanza.

Rukwa na Katavi ni miongoni mwa maeneo ambayo ujangili kuua tembo umeshamiri sana hasa katika mapori ya akiba ya Lwafi na Hifadhi ya Taifa ya Katavi kutokana meno ya tembo kuonekana kuwa na soko katika mikoa mingine nchini na nchi jirani.


Kamanda Mwaruanda akionyesha kigudulia ambacho hutumiwa na majangili kubebea risasi.

Ofisa Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Davies Mushi alinukuliwa hivi karibuni kuwa kuwepo kwa soko zuri la biashara haramu ya nyara za Serikali hususan meno ya tembo ni moja ya sababu zinazochangia ongezeko la ujangili katika hifadhi hizo.

"Soko zuri la meno ya tembo lililopo katika mji wa Mpanda (Katavi), Sumbawanga (Rukwa), Tabora na maeneo mengine ya nchi linachangia sana kushamiri kwa ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, lakini tunajitahidi kufanya doria ndani ya hifadhi na kukabiliana na kasi hii iliyopo ya kuua tembo inayofanywa na majangili ambao wengi wao ni kutoka nje ya nchi," alisema Mushi.
Kama hali ndio hii, tumekwisha!
 
Nina uhakika pamoja na upemba wake lazima atakuwa ni mwanachama hai wa CCM.
Na zaidi unaweza kuta pia ni mfadhili wa chama.
 
Kumbe! Hivi ni nini kilichowavutia wakaamua kuishi sehemu hizo? Maana kule tabora wanazoa pembe za ndovu kama za kwao vile.

Serikali imeshughulika kuivamia Zanzibar ,huku Tanganyika imekuwa shamba la bibi . Wengine hata migodi wanajiuzia. Tunadumisha Muungano
 
Nahisi na nina hakika 100% kuwa huyu ni mtu anayetokea/mwenye asili ya Kisiwa cha Pemba. Vere sure.
Wapemba waarabu wengi hawapendi muungano kwa hiyo kaamua kuaangamiza tembo wa Tanganyika? Huyu sio wa kumhurumia ni mhujumu uchumi wa tanganyika ambaye ni RAIA wa nchi ya nje ya Zanzibar ambayo ni nchi kamili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya 2010.
 
Wakuu naomba kufahamishwa kwa anayejua.
Juzi kati raisi alipotembelea wizara ya mali asili alimtaja mpemba kuwa anahusika na biashara ya pembe za ndovu, huyu Mpemba ni nani kwa anamjua atuambie na sisi tumjue adui huyu wa taifa.
abdulrahman kinana
 
Back
Top Bottom