Mpe na cha pili weweee!!!

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Nilipokuwa ninaishi kuna mzee mmoja wa makamo ni maarufu sana maeneo yale, kazi yake ilikuwa kutengeneza Ngalawa na Mitumbwi, huo mji wanajishughulisha sana na uvuvi.

Kila eneo kuna mazeoa yake ukichulia kwa pwani wavuvi wanautani na wachuuzi lugha chafu kwa kwenda mbele, kama ni mgeni maeneo ya pwani unaweza sema mboni wanagombana kwa jinsi wanavyotukananaa?

Basi huyo mzee akavuka mpaka akafikia kujiapiza kuwa kama atatokea kijana wa maeneo hayo ya pwani hasa vijana msiokuwa na adabu, akamtongoza bint ake na akala mzigo, anaapa kuwa atastaafu kutengeneza Ngalawa.

Vijana kusikia hilo battle wakamwambia
jiandae kutafuta kazi nyingine, kwani wahuni sio watu wazuri, wakamhakikishia kumbe walivyuokuwa wanamuheshimu ndio amewadharaulisha hivyo, yeye akae Rada.

Kuna siku mzee kaenda kufanya ibada, wakati anatoka wahuni wamepita na viatu vyake, mzee alistaajabu sana akajiuliza huu uwizi umeanza lini wakati walishaukomesha?

Kumbe ni mpango mkakati uliandaliwa na vijana wa pwani, kwa mbele kuna kijana kama alikuwa anarekebisha baiskeli, kumuona mzee analalamika, yule kijana akamfuata kumuuliza kulikoni! Ndio mzee amwelezee na kumwambia aende nyumbani ( kwa mzee ) akamchukulie viatu.

Na akaapa huyo aliyechukuwa viatu vyake atamuonesha yeye ni nani? Kijana mdogomdogo hadi kwa mzee na kijana huyohuyo alishalilia mzigo bila mafanikio, kwa maelezo ya bint anamuogopa babu yake ni mkali.

Kuna siku alimuona amesimama na kijana wa pale mtaani, bint aliadhibiwa kipigo cha mbwa koko, toka siku hiyo bint muda mwingi ndani tu. Basi kijana kufika akazama ndani, moja kwa moja kwenye stuli.

Bint akahamaki "wewe haumuopi babu, ngoja akukute hapo utapigwa!"

Kijana akamwambia "huyo babu yako ndio kanituma nije ilitumalize kula tunda"

Bint akajuwa utani huku anajichekesha akasema " acha utani toka hapa usijeniletea balaa mimi"

Kijana akasema "kama hauamini nimekuja na baiskeli nikuchukue tukamuulize, nimemuacha msikitini"

Bint akashangaa babu kamtuma kweli, " kama niuongo utanipa nini,?"

Kijana "tusiandikie wino! wewe twende"
alisema kijana. Hao wamepakizana nyuma ya nyumba kuna uwanja wa mpira, msikitini na hapo sio mbali.

Kukata kona tu kijana akasimamisha baiskeli akashuka yeye na yule bint, mzee kuwaona akawauliza " mnaenda wapi?

Kijana akasema " hataki kunipa huyu mjukuu wako!!!"

Mzee "wewe nenda kampe, kumbe muda wote nasubiri alikataa kukupa haya fanya haraka"

Kijana na Bint wakapanda baiskeli kurudi nyumbani kuhembeluka, fasta fasta kijana kamaliza na katoka nje na bint akisema " twende ukamwambie umenipa ili aamini na asije akakuadhibu"

Hao hadi pale waliposimama mwanzo kijana akapaza sauti kumwambia mzee "amenipa kimoja"

Mzee akamfokea mjukuu wake "hivi wewe unaakili kweli nenda kampe chapili"

Kijana na Bint hao kwenye baiskeli kurudia raundi ingine, alivyomaliza kuhembeluka kijana akamwambia bint, chukua hivi viatu vyake halafu unipe malapa nimpelekee, bint bila kujua kulichokuwa kinafanyika akapokea viatu na kumpa malapa ampelekee.

Kumbe yule kijana ndio alikuwa amechukua viatu vya mzee akajifanya anahitaji kumsaidia mzee kwenda kuchukua viatu baada ya mzee kufikiri vimeibwa! Na kijana kacheza na akili kwamwambia bint nipe bila kutaja viatu.
 
Back
Top Bottom