Mambo ya CHADEMA yanakuhusu nini?Baada ya sakata la kususia hotuba ya Rais Bungeni na mpasuko uliojitokeza huko, hivi sasa kuna mambo kadhaa ya ndani ya Chadema yanayo ashiri kuisambaratisha Chadema.
1) Kususia Hotuba ya Rais
Hili limetuonyeshaa ni jinsi gani Chadema inavyoendeshwa bila muelekeo, wakati wabunge wao wengi wa-kisusia hotuba ya Rais wengine wengi walisusia shinikizo la Mwenyekiti wao na kuamuwa kuto ingia kabisa bungeni siku hiyo. N awengine tukawaona, usiku huo kwenye hafla ya Rais ilhali viongozi wa Chadema walishinikiza wabunge wa Chadema wote wasiende huko.
2) Kugombea vyeo na nafasi za upendeleo.
Tumeona sakata la nafasi za upendeleo haswa za ubunge jinsi zilivyoleta mvutano ndani ya Chadema na kufikia wana Chademaa wengine kuwachia ngazi, hii ni dalili tosha kuwa utawala wa ndani wa Chadema una mapungufu makubwa.
Tukaona pia jinsi Zitto alivyopigwa chini na Mwenyekiti wake katika kuwania nafasi ya uongozi wa upinzani bungeni. Hali kadhalika tukaona Zitto alivyosulubiwa mpaka kulazwa hiospitali na kupigwa marufuku na uongozo wa Chadema kuwa asiongee na vyombo vya habari kuhusu Chadema kwani yeye si msemaji wa Chadema.
3) Sakata la Arusha:
Tumeona jinsi wengi wa viongozi wa Chadema kutokuhudhuria kwenye maadamano yaliyoshinikizwa na kushadidiwa na viongozi wachache wa Chadema. Na pia tukaona mvutano mkubwa ukitokea katika kutumia maiti kama njia ya kujipatia umaarufu Chadema, ni viongozi wachache wa Chadema walihudhuria "kuaga miili ya marehemu" hao.
Tukaona kuwa hata Fundikira ambae ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chadema mkoani Arusha kukataa kuhudhuria muago huo, akisingizia kuwa alikuwa na wageni nyumbani kwake. Wageni zaidi ya Mwenyekiti wake wa Taifaa na Katibu Mkuu wake na Kuaga "wahanga"? hilo ni la kujiuliza.
Ukitazama kwa juu juu utaona hayo si kama mambo ya kawaida, na ukiingia ndani kidooogo, utaona kuwa huo ni mpasuko na mtafuruku mkubwa ndani ya Chadema.
Wenye macho hawaambiwi tazama, na wenye masikio hawaambiwi...
Nadhani Rais kawaaibisha Chadema na juzi UDSM ndio kabisa walipowekewa bayana kuwa hii si katiba ya kwanza Tanzania na zote zilikuwa zikibadilishwa na mtu mmoja tuu, Nyerere, na kwa mara ya kwanza JMK kasema atawashirikisha wananchi, nadhani hilo nalo jambo kubwa sana hapo. Au wewe unaonaje? ikiwa hiyo ndio kulazimishwa na Chadema na akakubali, sasa unamuweka wapi mtu kama huyo? na alipokubali kuweka tume ya katiba ilikuwa kabla au baada ya maandamano yaliyouwa Arusha?
Kumbe ndo mahala pako pa kupotezea muda hapa....aaaggghrrr!!!! IF YOU'VE GOT NOTHING TO DO PLEASE DON'T DO IT HERE!!! GO DO IT S'WHERE ELSE!! Nakushauri nenda pale Lumumba kuna kijiwe flani cha kahawa na majungu kitakufaa sana mtu kama wewe...
Wewe ungekuwa na cha kufanya sijui ungeijibu vipi hii post?
Mwenzi mimi semi retired, nipo shambani kwangu, nimeshawalisha samaki, sasa napoteza wakati ifike time nipige ubwaubwa wangu kwa mbaazi za nazi. Wewe?
Nadhani wewe ni mhandisi,na ninaamini mhandisi huwa ana uwezo wa juu sana wa kufanya analysis...ana uwezo wa kuona hidden lines,..ana uwezo wa kuvisualize in more than three dimensions...au wewe sio?..Kama ndivyo naamini unaweza kuona nyuma ya mawazo ya mtoa mada ktokana na main thread na hata katika majibu ya utetezi wa idea yake...Sasa hebu niambie kwa huyu zombi,unaona kweli mchango chanya wa kuijenga chadema? Nani kasema Chadema haikosei, nani kasema kuna chama perfect duniani,nani hajui kuwa mahali penye watu makini hapakosi kuwa na kupishana kwa hoja?...na NANI hajui kuwa CCM wangependa kutumia kila sekunde kueneza propanganda za kukipaka matope chadema (of course kwa an obvious reason - ndicho chama pekee tishio kwake kwa sasa)...Nani tena hajui kuwa baada ya kushindwa kwenye mapambano ya hoja (hukumbuki waliokimbia midahalo wakati wa uchaguzi - au nalo hulioni?) CCM wamebakiza mbinu moja tuu,kununua watibuaji,wapaka matope,mamluki na wafananao na hao. They are desparate....,na recent developments ndio zina-prove hili.wanadiriki kuwagawanya watanzania kwenye lines za DINI ,sipendi kulitaja hili lakini ndio ukweli! Pathetic!!!Hapa ndipo unapoona athari za ku-replace kichwa kama cha Philip Mangula na cha makamba!! (CCM walishindwa swali jepesi tu la kitoto "identify the odd.....Kolimba,Mangula,Prof Anyang Nyong(ODM kenya,......Makamba..")! Sasa EngMtolera unataka zombi ajibiwe kwa lipi analoongea hapa?Wewe ni wa kwao au wa wakwetu mkuu?mimi nadhani umefika wakati wa kukubali makosa na kuanza kuyashughurikia mapema iwezekanavyo,sio kila jambo liwekwalo hapa juu ya chadema lina lengo la kuiyangusha ama kuichamba chadema,tuwe wenye kupima na kukubali na kuona ukweli kwa yale yatokeayo na ikiwezekana tuyatafutie dawa
kinacho nishangaza kwa chadema sisi ni kuwa hatukubali kuwa kuna tatizo na tunajifanya hatuoni yaliyotokea huu ni mwelekeo hasi kwa viongozi walio makini na walioive kisiasa
inamaanisha hata tukipewa nchi haya ndiyo majibu tutakayo kuwa tukiyatowa kwa wapiga kura wetu,kwani kila jambo linaloangukia kwetu chadema ilimradi tu limeonyesha kushindwa kwetu huwa hatuko tayari kukubaliana nalo na hata hatuko tayari kulitaftia uvumbuzi
zaidi ni kimtusi mtoa mada kana kwamba alichokitowa hakikufanyika ARUSHA.
Tubadilike kama kweli tunataka kuwaongozi WTZ tuondoe fikra hasi na mgando tulizonazo juu mada zote hasi kwa chadema,si kila siku CDM Tuko safi some times kunamatatizo na nilazima tuyakubali na kuyataftia ufumbuziiiii
MSEMA UKWELI HAPENDWI DAIMAAAAAA
mapinduziiii daimaaaa
CCM 2005= 80.2%Waeleze hawa wasiyaona hayo, hawajuwi kama siasa ya sasa hivi ni ushindani, kama unahitaji kura zaidi lazima urekebishe makosa na kuvutia wanachama wapya wa kukupa hizo kura, kwani kwa sasa ndio hivyo tena, 20%.
The guy goes down in history as the most hopeless gentleman to ever occupy the seat of the secretary general of any ruling party in the world! Salute mzee,mwanuka zeze!
Onyesha pumba moja katika hayo!
Inanisaidia kukuza Demokrasia Tanzania.
2) Kugombea vyeo na nafasi za upendeleo.
Tumeona sakata la nafasi za upendeleo haswa za ubunge jinsi zilivyoleta mvutano ndani ya Chadema na kufikia wana Chademaa wengine kuwachia ngazi, hii ni dalili tosha kuwa utawala wa ndani wa Chadema una mapungufu makubwa. Katika hali ambayo nafasi ni chache na wagombea ni wengi, jambo hili haliwezi kukwepeka. Kwa kutojua hili, umeandika pumba.
Tukaona pia jinsi Zitto alivyopigwa chini na Mwenyekiti wake katika kuwania nafasi ya uongozi wa upinzani bungeni. Hali kadhalika tukaona Zitto alivyosulubiwa mpaka kulazwa hiospitali na kupigwa marufuku na uongozo wa Chadema kuwa asiongee na vyombo vya habari kuhusu Chadema kwani yeye si msemaji wa Chadema. Zitto angeshinda ungesema "Tazama Mbowe alivyopigwa chini na Zitto". Hii nayo ni pumba.
Bila shaka una shahada ya uzamili kutoka Urusi ya zamani (USSR).
Zomba, siamini kama umetumwa. Inawezekana umejituma mwenyewe. Hilo tuliache.
Turudi kwenye huo mpasuko. Nadhani twende kwa mifano hai;
1) Kususia Hotuba ya Rais
Hili limetuonyeshaa ni jinsi gani Chadema inavyoendeshwa bila muelekeo, wakati wabunge wao wengi wa-kisusia hotuba ya Rais wengine wengi walisusia shinikizo la Mwenyekiti wao na kuamuwa kuto ingia kabisa bungeni siku hiyo. Na wengine tukawaona, usiku huo kwenye hafla ya Rais ilhali viongozi wa Chadema walishinikiza wabunge wa Chadema wote wasiende huko.
Hapa hoja yako ni kwamba kitendo cha baadhi ya wabunge kutofautiana kimawazo kuhusu kuingia au kutokuingia bungeni ni mpasuko. Kitendo cha Shibuda kwenda kwenye hafla ya Raisi ni mpasuko. Nikitaka kukubaliana na hoja yako najiuliza, je huo ni mpasuko au dalili ya mpasuko? Hivyo ni vitu viwili tofauti. Lakini, najiuliza tena, kuna athari gani viongozi wa chama cha siasa kupingana kimawazo? Ninavyoamini mimi ni kwamba kupingana mawazo ni faida endapo mwisho wa siku muafaka utafikiwa kama ilivyotokea kwa CHADEMA. Suala la kutokuhudhuria bungeni lilijadiliwa na Kamati Kuu na uamuzi kutolewa wa nini kifanyike. Huo ni ukomavu wa kisiasa.
2) Kugombea vyeo na nafasi za upendeleo.
Tumeona sakata la nafasi za upendeleo haswa za ubunge jinsi zilivyoleta mvutano ndani ya Chadema na kufikia wana Chademaa wengine kuwachia ngazi, hii ni dalili tosha kuwa utawala wa ndani wa Chadema una mapungufu makubwa.
Hapa umepotea. Je kuna ubaya gani mtu 'kupendelewa' kutokana na uwezo, elimu na utendaji wake? hakuna dhambi kumpendelea mtu kwa vigezo hivyo ambavyo ndivyo vilivyotumika kupata wabunge wa viti maalum. Ni tofauti pale mtu anapopendelewa kwa sababu ya mzazi wake, fedha zake na mchango wake katika kuliibia taifa. sihitaji kukueleza zaidi. Kuna watu ambao kwa kiasi kikubwa waliamini kwamba CHADEMA itayumba kwa sababu ya Viti Maalumu. Lakini leo hii hali ni tofauti sana!! Angalia kabla ya wao kujitoa na sasa ili uone CHADEMA iko wapi.
Kwa kiongozi kujitoa kwenye chama kisa nafasi ya ubunge ni ishara wazi kwamba mtu huyo ana walakini. Kitendo cha mtu kutaka apewe nafasi kwa sababu tu amekaa muda mrefu kwenye chama hakikubaliki ndani ya CHADEMA. Kuondoka kwa watu wa aina hiyo ni faida kwa chama.
Tukaona pia jinsi Zitto alivyopigwa chini na Mwenyekiti wake katika kuwania nafasi ya uongozi wa upinzani bungeni. Hali kadhalika tukaona Zitto alivyosulubiwa mpaka kulazwa hiospitali na kupigwa marufuku na uongozo wa Chadema kuwa asiongee na vyombo vya habari kuhusu Chadema kwani yeye si msemaji wa Chadema.
Utaratibu uliotumika kuhusu KUB ni utaratibu unaoleweka kwa urahisi sana. Sihitaji kukufundisha kutokana na umri wako ambao umeulinganisha na Prof. Shivji. Nitakuheshimu hivyo nitaliachia hapo. Ni kweli Zitto si msemaji wa chama. Ungependa CHADEMA kila mtu aseme analojisikia kusema kama ilivyo kwa Mwakyembe, Sitta, Vuai, Makamba, Chitanda, Wassira, JK, Membe n.k kuhusu kilichotokea Arusha??? Hayo ndiyo yanayokufurahisha? Je hu ni mpasuko ndani ya CCM na Serikali??
3) Sakata la Arusha:
Tumeona jinsi wengi wa viongozi wa Chadema kutokuhudhuria kwenye maadamano yaliyoshinikizwa na kushadidiwa na viongozi wachache wa Chadema. Na pia tukaona mvutano mkubwa ukitokea katika kutumia maiti kama njia ya kujipatia umaarufu Chadema, ni viongozi wachache wa Chadema walihudhuria "kuaga miili ya marehemu" hao.
Kwa mara nyingine umepotea ila safari hii umenipoteza na mimi. Viongozi wachache ni wangapi? kwenye maandamano hayo walikuwepo wafuatao Mwenyekiti wa taifa, Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Mkoa, Katibu wa Mkoa, Mwenyekiti wa Wilaya, Katibu wa Wilaya. Wenyeviti wa Kata, Wabunge na Madiwani. Hao ni wachache???
Umaarufu?? Umati uliohudhuria mkutano siku hiyo ulienda kuona maiti?? Kulikuwa na maiti uwanjani siku ya tarehe 5?? Ni umaarufu upi CHADEMA imeupata? CHADEMA ni watu, sio chombo. Kuna watu wanashindwa kuliona hilo ndio maana anguko lao liko karibu sana. Unapolaani CHADEMA unalaani watanzania zaidi ya milioni 5 ambao ni wafuasi wa CHADEMA!
Tukaona kuwa hata Fundikira ambae ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chadema mkoani Arusha kukataa kuhudhuria muago huo, akisingizia kuwa alikuwa na wageni nyumbani kwake. Wageni zaidi ya Mwenyekiti wake wa Taifaa na Katibu Mkuu wake na Kuaga "wahanga"? hilo ni la kujiuliza.
Fundikira alihudhuria vikao vyote. Yeye ndiye aliyempigia Sheikh Mkuu wa Bakwata na viongozi wengine na kuwaambia wasiilazimishe familia ya marehemu kuacha kuaga mwili. mwenyekiti wa taifa alimshirikisha Mzee Fundikira wakati wote kwa kuona umuhimu wake kama Muislamu na kiongozi. Humjui Mzee Fundikira hivyo usipotoshe ukweli. Kusema ukweli ni sababu ya kuheshimika zaidi.
Ukitazama kwa juu juu utaona hayo si kama mambo ya kawaida, na ukiingia ndani kidooogo, utaona kuwa huo ni mpasuko na mtafuruku mkubwa ndani ya Chadema.
Hakuna mpasuko CHADEMA. Tofauti za mawazo au maoni tofauti sio mpasuko. Kwa Chama makini hu o ni mwanzo pia kipimo cha ukomavu. CHADEMA wanathibitisha hilo kila kukicha. Hauwezi kujiandaa kuongoza nchi kama haupitii katika hali hiyo ya utofauti wa mawazo.
"A smooth sea doesnt make a good swimmer"
:Cry:
Most hopeless gentleman.Luteni Makamba!