Adui kwenye hili ni nani? Plan za mashirika mbona zipo kwenye website zao na report za miezi mitatu za mapato hasa kwenye kampuni zinazoendeshwa kibiashara!? hivyo huu si ukweli. Hiyo secret plan imeandaliwa na nani ? Je wameonyesha bunge la wananchi?. Sasa kama ni plan za siri za kibiashara ni nani ambaye atahakikisha pesa ya wananchi inatumika vizuri? GAG naye anaruhusiwa au ni siri kwake pia? Ukweli ni kwamba kama plan haipo mseme badala ya kujifanya mnayo na kuishia kwenye hasara maana makampuni ya ndege ni gharama sana kuendesha na faida mengi hayana
Mpango unaoulizia siyo PUBLIC DOCUMENT ni chombo cha kimkakati cha ndani cha kufanyia kazi ili kufikia malengo ambayo ndiyo hayo ya kuongeza route na kuongeza abiria. Mpango mkakati wa kibiashara au Business Strategic Plan is a "secret internal document" ambayo adui au mshindani wako wa kibiashara akiuona anaweza kuutumia kukushinda au hata kukuhujumu. How ever seen such a document for anyother airline company? Tujuze with evidence!
Naona tuna nunua ndege sio jambo baya lakini watu wengi wanapinga kwasababu hakuna mpango ambao unajulikana bado vizuri wa hili shirika. Je hizi ndege ni kusafiri Africa yote? mikoa yote? Ulaya na US? wa watafanya ushirikiano na mashirika mengine? Je wana vibali vya kusafiri nchi hizo za nje?..... . Kama kuna mtu ana plan atuwekee hapa ili tuone. Inakuwa ngumu ku support kitu bila kujua lengo maana kwa sasa kuna ndege nyingi tu zinakuja TZ!
Mkuu Kamundu, alichukujibu Mzee Mukaruka ni ukweli mtupu, strategic business plan ya biashara yoyote ni secret internal document ambayo washindani wako hawapaswi kuifahamu!.
Ila pamoja na siri hiyo, kiukweli kabisa na bila kuwaonea, hizi ndge tumenunua na pupa na papara bila business plan ili tuu kuonyesha tunaweza. Ndege zikiisha wasili ndipo tunaandaa business plan!. Hivyo ndivyo tulivyofanya kwa Bombadier na labda ndivyo tunavyofanya kwa Dreamliner, ndege imewasili siku ya Jumapili, kesho yake Jumatatu, ATCL wamekaa na TTB kusainiana MOU kupeleka ndege Ghwanzou, Mumbai na London, huku wanajua fika hutuna landing rights, na ATC haina air worthiness certificate kutoka IATA, kitu ambacho Watanzania tunachofanyiwa ni kutoelezwa ukweli bayana!, aliyetoa siri ndege yetu imeshikiliwa kwa kudaiwa, mnakijua kilichomkuta!.
Ili Dreamliner yetu ivuke mpaka wa kutua popote nje ya bara la Africa ni kwanza lazima tuikodishe kwa mashirika wenye landing rights hizo, vinginevyo tulipe deni la IATA tunadaiwa Zaidi ya US $ million!.
Ni ukweli usiofichika, kuirusha Dreamliner kwa routes za ndani ambazo zote ni short distance less than 1 hour, sio tuu kutaichosha, kuichakaza na kuishorten its life span kutokana na engine wear and tear kwa take off na landing ya short distances kunaichokesha bure engine ya mtulinga!, ila pia operational wise, it's not worth it. This will be a loss making exercise. Enzi za Mwinyi tuliibeba ATC na kuifeed kwa spoon fed while making losses. Mkapa akaruhusu ubia na SAA, JK akagoma kuendelea kuibeba na kuifeed. Sasa JPM kaifufua kwa nguvu kubwa kuliko uwezo wetu to operate haya madubwana makubwa ya long hauls. Hivyo ATC will be making losses lakini JPM will feed it, ila awamu nyingine ikija ndipo itagundua kuwa ATC is a baby that never grows, it's still sucks.
Ili kuinusuru ATCL, tunahitaji a political will ambayo tayari rais Magufuli ameishaionyesha, lakini political will pekee yake bila business viability, ni kuonyeshea just the pride of wings of Kilimanjaro on airwaves but at the expense of poor Tanzanians. Kanisome hapa
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani?
P.