Mpango wa serikali wa kuinua ufaulu kwa kidato cha nne mwaka 2013 hadi 2015....

Kimetah

JF-Expert Member
May 8, 2013
1,049
188
Nadhani mmeshasikia mpango wa serikali wa BIG RESULT NOW, ambao unatekelezwa kwenye wizara nne,yan
wizara ya elimu,nishati ,kilimo na fedha
Sasa mpago katika wizara ya elimu ili kuhakikisha big result now inafanikishwa,wameupa jina la
STEP yani Student Teachers Enrichment Program,ulotungwa na ofisi ya raisi na kutoa maelekezo kwa wizara ya elimu kwa utekelezaji
katika kutekeleza STEP,serikali umechagua masomo manne,yan MATHEMATICS,BIOLOGY,KISWAHILI na ENGLISH,wakilenga kila mwanafunzi apate daraja"D" kwa masomo mawili kati ya hayo wanne ili asipate div.zero
Na walimu wa masomo hayo wamekuwa wakipatiwa semina jinsi ya kufundisha wanafunzi wa kidato cha nne ili wapate div.1 hadi div.4 na si zero tena.
Pia ahadi lukuki zimetolewa kwa shule na mwalimu atakaye faulisha kwa kiwango cha juu zaidi.mfano ni zawadi ya tsh.mil7 hadi 10
Sasa katika semina hizo walimu wanaulizana na kuhoji maswali mengi mmo,mfano
1.Tumekuja kupewa semina,wakati hakuna malipo yoyote tulioahidiwa
2.Kama serikali inahitaji matokeo mazuri,je hi ndo njia mwafaka?kama ndio wasubiri necta 2013 waone
3.Mwanafunzi hajafundishwa vema toka chekechea leo hii ndo afaulu kwa miez mi3 iliyobaki?
4.Tulishasema tupewe mishahara minono tufanye kazi hawataki,kama wamebuni mtindo huu kutupooza wasubiri majanga mendine
5.Ahadi tulishazoea kutoka kila kona lakini hawatimizi,nadhani huu ndo muda mwafaka wa kupata pesa kwa njia ya semina vivyo ili semina nyingi ziwepo nilazima watoto wafeli.
6.ili haya yatekelezwe tunasubiri mshahara wa mwezi wa saba ndo tujue chakufanya

WASIWASI WANGU WANA JAMVI

  • Je elimu yetu itakuwa bora?wakati watendaji yan walimu hawataki mabadiliko kama hayo ya BIG RESULT NOW
  • Kama serikali inataka wanafunzi wapate ufaulu kwa njia yoyote ile pasipo wanafunzi kupata ufahamu wa mada husika,ni sawa na kufanya mauaji?
wakuu hili mwalionaje?mnashauri nini kwa waalimu hao?
 
Napiga tempo hapa nimeshangaa kuona mtihan umeandikwa BRN na wanafunzi wamesimamiwa na walimu wao wa madarasa,kilichofanyika walimu ni kuwapatia majibu wanafunzi ili kupata BIG RESULTS NOW!
 
Napiga tempo hapa nimeshangaa kuona mtihan umeandikwa BRN na wanafunzi wamesimamiwa na walimu wao wa madarasa,kilichofanyika walimu ni kuwapatia majibu wanafunzi ili kupata BIG RESULTS NOW!

Ha ha ha ha ha.
 
Back
Top Bottom