Mpango wa kutokomeza ukeketaji waendelea kushikiwa bango

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,265
5,358
Viongozi wa mila wa jamii za kifugaji, kwa kushirikiana na Mangariba Wilayani Kiteto, mkoani Manyara, wameanza kutekeleza mpango wa kitaifa wa kutomokeza ukeketaji, kwa kupiga marufuku mila hiyo

Kwa umoja wao wamewataka Mangariba kusalimisha zana zao kama njia mojawapo ya kutokomeza vitendo hivyo, ambavyo vinahatarisha afya za Wanawake na ustawi wao

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema jukumu la ulinzi na usalama la watoto ni la jamii nzima na hivyo Sheria inawataka kulinda mtoto

Chanzo: ITV

Pia soma: Manyara: Ngariba 37 wajisalimisha, wakabidhi visu vya kukeketea
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom