Godbess lema amevuliwa ubunge halafu akawa maarufu zaidi nahisi Kitila mkumbo huenda ikawa the same maana jana lunch time niko makaburini bar(rose garden ya Arusha) alivyoingia nikaona watu wote wameweka tonge chini kumlaki mheshimiwa lemaI trust the profesors na wahadhiri wengine kuwa hawatomfanyia hiko wanachofikiri hao wavivu wa kufikiri.Dr.Kitila hata kama alivyosema juzi kuwa wao hawagombei bali majina hupendekezwa na wajumbe na mwenye sifa hupewa nafasi ya kuongoza kwa kuchaguliwa kwa kura.Naamini atapita tena kwa kishindo na watashangaa!Aliewaambia kuwa wao wanahaki miliki ya uongozi na rasilimali za UDSM nani?waache upuuzi wao wa kijinga msomi mkubwa anakuwa na majungu majungu then anataka aheshimike how?
Waniachie mbunge wangu wa Iramba Magharibi na Wazira wa Elimu 2015
Hakuna shaka kwamba kuna watu wanakerwa sana na makongamano ya Nkrumah. Hawa ni wale wanaoamini kwamba ili uweze kuongoza vizuri lazima uwafiche watu taarifa na uelewa. Wanaamini katika kuongoza wajinga, na bahati mbaya makongamano ya Nkrumah yamekuwa yakiamsha watu wengi sana nchini kwa sababu yanarushwa moja kwa moja na ITV, ambaye inaangaliwa sehemu kubwa ya Tanzania. Wengi walishanivaa mimi mwenyewe mara kadhaa na kunilaumu kwa kuandaa makongamano haya na kudai kuwa nayatumia kisiasa kuinufaisha CHADEMA. Hata hivyo, wana UDASA walio wengi wanajivunia sana makongamano yanayofanyika kwani ni sehemu muhimu ya kutoa mchango wetu moja kwa moja kwa jamii ya watanzania.
Pamoja na baadhi ya watu kukerwa na makongamano yetu, bado hawana uwezo wa kutuchaguliwa nani awe kiongozi wa UDASA. Wanachama wa UDASA wapo makini mno kiasi kwamba ni vigumu kujipenyeza kijanjakijanja katika ngazi ya uongozi kama ilivyo katika siasa za kawaida za Tanzania.
Ukweli ni kwamba muda wetu wa uongozi ulikuwa umeisha na jana tumefanya uchaguzi kama nilivyotangaza katika kongamano la Nkrumah. Mimi nilikuwa sio miongoni mwa waliopigiwa kura baada ya kuwaomba wenzangu wanipumzishe kufuatia kuteuliwa kuwa mkuu wa kitivo cha elimu katika chuo chetu cha DUCE ili kuepuka mgongano wa maslahi na ukweli kwamba sasa hivi nipo mbali na makao makuu ya UDASA, yaani Mwalimu JK Nyerere Mlimani Campus. Nashukuru wenzangu walinielewa na kuniruhusu nisiendelee na uongozi wa UDASA.
Jana tulichamchagua Dkt Francis Michael kuwa Mwenyekiti mpya wa UDASA na nafasi ya makamu imechukuliwa na Dkt Vicensia Shule. Kwa wale wanaofuatilia kwa karibu harakati za CKD watakumbuka kwamba Dkt Francis Michael alikuwa Makamu wangu mimi nilipokuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi CKD (DARUSO) 1998/1999. Ni mtu makini kabisa na naamini ataisogeza UDASA mbele zaidi.
Mimi kwa sasa naelekeza nguvu zangu katika kuchangia kuona kuwa chuo chetu cha DUCE kinakuwa miongoni mwa vyuo bora kabisa katika bara letu katika kutoa walimu na kuchangia kikamilifu katika kuboresha elimu hapa nchini kupitia ufundishaji, tafiti na mijadala ya kina juu ya maswala ya elimu nchini mwetu na katika bara la Afrika kwa ujumla.
umesomeka vizuri mkuu. Dk Francis Michael namfahamu vizuri sana. Amekuwa akihudhuria makongamano mbalimbali yanayofanyika Nkrumah japo hakuwa mchangiaji sana. Amenifundisha course inaitwa Human Resource Management(HR 201). He is objective japo anahasira akichukizwa hata kwak2 kidogo....................
Mbona Tumbiri hajitaji?Ngoja nimpigie simu Dr Kitila Mkumbo aje hapa. Lakini na wewe Kijana Msomali ungewataja kwa majina hao wahadhiri waliokuwa kwenye mazungumzo. Si unajua hapa tuna talk openly!
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Mbona TUMBIRI hajitaji?